Muungano wa Linda Mwananchi limekemea vikali taarifa za kutekwa kwa mwanaharakati kutoka Tanzania, Twaha Mwaipaya, katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos, na kutaka serikali ya Kenya ichukue hatua za haraka kubaini alipo na kuhakikisha usalama wake.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, Oktoba 26, vuguvugu hilo lilitaka kufichuliwa mara moja kwa mahali alipo Mwaipaya, uchunguzi huru kuhusu tukio hilo na uwajibikaji kwa wote watakaobainika kuhusika, bila kujali nyadhifa zao au uraia wao.
Kwa mujibu wa taarifa za Amnesty International Kenya, Mwaipaya aliripotiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana Jumapili, Oktoba 25, alipokuwa akisafiri kwa teksi kuelekea kuwatembelea marafiki. Watu hao wanadaiwa kutumia magari matatu. Hadi taarifa za awali zilipotolewa, mahali alipo na utambulisho wa waliohusika haukuwa umebainika.
Linda Mwananchi imeonya kuwa tukio hilo linazua wasiwasi kuhusu usalama wa wanaharakati na wakosoaji wa serikali kutoka nchi jirani wanaotafuta hifadhi nchini Kenya.
Vuguvugu hilo pia limetaja visa vya awali vya mwanasiasa wa upinzani wa Uganda, Kizza Besigye, aliyeripotiwa kutekwa jijini Nairobi Novemba 2024 na kupelekwa Uganda, pamoja na mwanaharakati wa Tanzania Maria Sarungi Tsehai, aliyeripotiwa kutekwa Nairobi Januari 2025 na kuachiliwa baadaye siku hiyo.
Aidha Linda Mwananchi imeitaka Serikali ya Rais William Ruto kuhakikisha Kenya inaendelea kuwa kimbilio la watu wanaokimbia mateso ya kisiasa badala ya kuwa mahali ambapo wakosoaji wa serikali wanaweza kulengwa.
Wakati huo huo, viongozi wa upinzani wa Tanzania pia wameitaka serikali ya Kenya kusaidia kuhakikisha Mwaipaya anapatikana akiwa hai na salama.
Je, Serikali ya Kenya inafanya vya kutosha kuhakikisha usalama wa wanaharakati kutoka nchi jirani wanaotafuta hifadhi nchini, au tukio hili linapaswa kuwa kichocheo cha uchunguzi mpana kuhusu usalama wao?