Imekuwa kawaida kusikia watanzania wakiwaita watanzania wenzao kuwa ni waoga (cowards). Maajabu ya Mussa. Kwani hao wanaowaita wenzao kuwa cowards utaifa wao si ni huu huu au wao ni walamba asali?
Uhalisia wa mambo ni kuwa wanaowaita hivyo wenzao, nia yao ni kutokuwepo mstari wa mbele kunakofahamika kuwa ni hatari zaidi.
"Wako kwenye kuwasakizia wenzao kama mbwa tu, ili wakawapambanie."
Watu hao hawataki kuwa sehemu ya kulipa gharama zilizo kubwa kwenye mapambano. Nia yao, "panga pangua" wasidhurike kabisa. Kama vipi hiyo iwahusu zaidi wowote wengine. Lakini si wao wala familia zao.
Hawa ni "opportunists' tu, wenye kuangalia zaidi maslahi yao na familia zao.
Hawana taabu kujilia matunda yatakayopatikana (kwa raha zao), hata kama wote walioyapigania watakuwa walikufa au kupotelea mbali kwenye mapigano yaliyoleta matunda hayo.
Kimsingi ni watu wenye ubinafsi uliopitiliza.
Mbaya zaidi watu hawa wakiwa ni viongozi, ilikuwa hii ni vizuri wakaachia ngazi wenyewe au wakafurushwa madarakani pasipo na kuchelewa. Wa hivi ndiyo viongozi mizigo sasa. Kwa hakika viongozi wa namna hii hawatufai.
Viongozi wa hivi ni sawa tu na wale wakazi wa DRC wanaomtaka MONUSCO apigane kwa niaba yao, huku wakimlaumu kuwa hapigani kwa moyo au bidii ya kutosha.
Watu wa namna hii utawajua kwa kauli zao. Wanadhani mtanzania wa leo ni mjinga kuliko wao. Wanasema hamtokei mitaani, kama vile wao wanatokea mitaani.
"Kwanini tusitokee wote mitaani? Kwani JKNIA au Kiluvya ilikuwa je? Kwani viongozi wetu hawakuwa pale? Wafuasi hawakuwepo? Au walikuwa wao peke yao?"
Ifahamike jaribio la kuwaita watu kumwagika mitaani wakati awaye yote yuko nyumbani kwake, labda akiwa kwenye Runinga haliwezi kuwa na tija.
Tufike mahali asilaumiwe dobi. Tulipo yupi anaweza kujivua kuwajibika na tulipofikishwa?
Tukae chini kujitathmini - kutambua tulipokwamia. Mbona tulikuwa vizuri mno?