Jmushi, najua ni shida kidogo kwa wewe kukaa chini na kufikiria majibu ya maswali yanayoingia kichwani mwiko kwa mwendo wa kesi. Hivyo nimeona nirudie hapa pamoja na maelekezo ya kukusaidia. Huhitaji kunishukuru.
Nitarudia tena ili angalau ujifunze kujibu maswali badala ya kujibu swali kwa kwa swali.
1. ni nani mwenye mamlaka ya mwisho ya kutoa ripoti ya Kamati ya Madini? (kwenye swali hili unatakiwa kusema ni nani mwenye mamlaka ya mwisho ya kutoa ripoti, wajumbe wa kamati au Rais au mtu yeyote?)
2. Je Zitto ana ushawishi gani kwa Rais hadi Rais amsikilize na kufanya analotaka yeye Zitto? (katika sehemu hii ya swali unatakiwa ueleze ni kwa ushawishi gani Zitto anaweza kumuambia Rais afanye jambo fulani?)
3. Je, Rais asipotaka kutoa ripoti ya Kamati aliyounda hadharani wewe utafanya nini? na Zitto anatakiwa kufanya nini? (Swali hili lina sehemu mbili; a. ueleze ambacho wewe utafanya kama Rais hatotangaza hiyo ripoti hadharani. b. Unafikiri Zitto afanye nini kama Rais hatotangaza ripoti hiyo.)
4. Kamati ya Madini ina wajumbe wengi tu zaidi ya Zitto, kwanini umemkomalia Zitto badala ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji Bomani? (Katika swali hili la mwisho unatakiwa utoe sababu za kwanini Zitto ndiyo atoe habari na kufuatilia suala hili la Kamati na siyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo)
Natumaini umeelewa namna ya kujibu hayo maswali kama itakuwa vigumu nitajaribu kurudia tena kwa namna ya taratibu zaidi. Usipoweza kufikiria majibu yake unaweza kuniandikia ili nikutafute maswali zaidi ambayo ni mepesi.