Upinzania Tanzania ujitafakari

"Viongozi wao ni wahuni",umemaliza mjadala
 
Sio kweli, tumeona watu wakiwa wamejiandikisha na kupiga kura, lakini tunachokiona ni uhayawani wa wazi ukiendeshwa na vikundi vya kikatili vya ccm, kura za wizi zikiletwa vituoni kwa uratibu wa vyombo vya Dola na tume ya uchaguzi. Tunaona wapinzani wakienguliwa kwa Hila, na wasimamizi wa uchaguzi wakitangaza kura za udanganyifu Ili kuwapa ushindi wagombea wa ccm, na ushahidi wa uchafu huu upo.

Msitake kupotosha ukweli wa wazi wa kisiasa kwa za zaidi ya miaka kumi na Tano iliyopita. Toka uchaguzi wa 2010 siasa za nchi hii zilibadilika kutoka kikazi Cha zama za ccm, na kuhamia kizazi kipya cha siasa za vyama vingi. Mabadiliko haya ya kizazi ndio yamepelekea ccm kutumia mbeleko ya vyombo vya Dola waziwazi. Kwa Sasa siasa zinaendeshwa na Dola Zaidi kuliko ushawishi wa kisiasa.
 
nikukumbushe kuhusu siasa za Kenya , angalia hizo siasa ziko kwenye mazingira magumu sana ,lakini wapinzani wa kenya wapo solid , hawa wa huku wamelegea sana ,tuukubali ukweli,CCM wamekamata Dola wasitarajie watapewa kama mkate wapinzani
 
Shida ya wapinzani ndio hii,wakikosolewa wanaanza kusema anzisheni vyama nyie,
Zitto Kabwe alipambana sana kuwashauri ,wakaishia ku attempt kumpa sumu na kumfukuza pamoja na mama yake aliyekua kilema shida salumu, huu ulikua ni uhuni wa hali ya juu kabisa .
Wapinzani wanajiona wamejipata na wameridhika
 
Wanasubiri kufanyiwa.hapo alipo ukimuuliza yeye kama raia amechukua hatua gani anaweza asiwe na majibu,kazi kulalamikia wengine.
Wapinzani wakiambiwa ukweli wanasema tunalalamika, hivi anayekuamsha toka usingizini analalamika?
wapinzani mmepwaya , kuna ombwe kubwa kwenye uongozi wenu na mmeendekeza mapenzi kwenye tawala zenu amkeni
Jointhe chain mmechukua pesa za walala hoi ,badala mkawatembelee mnaishia kuzungula marekani kwa pesa za walala hoi oneni aibu
 
kwa maadili yetu Aliefariki hana nguvu ya kujitetea ,tuwaache waliolala
Maadili yenu ww na nani? Kama alijifanya mjuba akiwa hai, basi atapewa kubwa yake akiwa huko huko mapumzikoni.
 
Ni kweli wapinzani sio mabwawa ya umeme ,na sisi wananchi hatutaki wawe mabwawa ya umeme , tunachotaka wasilalamike bali watoe suluhisho mbadala
siku zote wanaandika vipeperushi mitandaoni ,oooh umeme hakuna serikali imeshindwa ,hatutaki mlalamike hivyo
tokeni mseme serikali ilitakiwa ifanye ABCD ,ilitakiwa ifanye haya na haya ili tuwe na umeme thabiti
wapinzani wamekua kama wananchi wa kawaida ,wanalalamika bila kutoa suluhu mbadala
 
Kasikilize Hansard za bunge ndio ujue wapinzani wamekuwa wakiongea Nini kuhusu umeme. Hizi propaganda za kitoto unazobeba toka hapo ofisi za uvccm hazina maana yoyote.
 
upinzani wa kenya una jeshi au polisi?
wapinzani wa kenya wana hoja ambazo zina washawishi wananchi kutoka majumbani na kuandamana
wana hoja zinazo waconnect wananchi na shida zao
Ninyi shida zenu haziongelei matatizo halisia ya watu
70% ya watanzania wanaishi maisha basic kabisa , ninyi mmegeuka kusemea shida za 30% ya watu ambao ndio wenye maisha bora .
Kero za mjini na vijijini ni tofauti ,wapinzani wanazunguka zunguka mjini tu hawagusi vijijini ambako ndiko kuna watanzania wanaohitaji kusaidiwa kifikra na kimantiki.
Wapinzani shusheni siasa zenu kwenye kundi la watu wa chini.
Mobilization zenu mnafanyia mitandaoni, club house ,twitter etc , huko kuna watu wa maisha ya nafuu pekee
haakuna mtu anayetumia twitter wa kuandamana
hakuna mtu wa club house anayehudhuria mikutano physical ya chama chenu
shukeni chini mguse shida za watu
 
Shida ndio hio mkuu,wapinzani hasa chadema wameamua kushambulia wao kwa wao hawako organized ,wanatukana tu ,yaani kifupi wanasikitisha
sasa hivi angalia wamemsusia hadi Maria Sarungi kushiriki twitter space zake kisa anamuunga mkono Dr Slaa
hizi ndizo akili zao ,yaani atakachosema mbowe wanashangilia ,anayeongea kinyume wanamtukana
Sugu na Lema ni wahanga wa siasa hizi pia
 
Ccm lumumba fc nilidhani ndio utafurahi ili ccm yenu itawale milele sasa kumbe unaona nongwa?
 
Ccm umeanza lini kuwa mshauri wa chadema? Kwa manufaa gani unayopata?
 
Mwamba upo vizuri sana kwenye kujenga hoja tunahitaji watu wa dizaini yako wengi hapa jamiiforum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…