Upinzania Tanzania ujitafakari

Upinzania Tanzania ujitafakari

Nchi yenye upinzani thabiti ni imara , na nchi ikikosa upinzani madhubuti italegea. Wapinzani wa Tanzania wamekua legelege sana, Nasema haya kwa sababu hizi:-

1.Wamekua wamatukio zaidi kuliko hoja
Leo umeme ukikatika wataongea kuhusu umeme week moja, baada ya hapo ikitokea vita Israel na Palestine ,watarukia habari hizo mpaka zikose mvuto. Hapa kama watanzania upinzani wa namna hii unatukosea.

Tunataka tuone mnachukua hoja moja mpaka mwisho , hawa wapinzani wa sasa hivi ,leo watadai katiba kesho Nape akiongelea VPN hao wanahama wanaanza kutukana , kesho kutwa moto Kariakoo haooo.
Yaan hawana consistency .Badirikeni 2025 mtahangaika sana.

2.Uongozi wao una migogoro mingi sana
Kumeibuka migogoro isiyoisha ndani ya vyama vya upinzani,mfano NCCR mpaka sasa wana gombana
Chadema kuna shida kubwa sana ya uongozi wa juu ambayo inafungwa fungwa , ACT Zitto ana wamanage kidogo vijana wake.

Tatueni shida za ndani ya vyama vyenu ili muingie mtaani kama kitu kimoja, Inaumiza sana kuona vijana wadogo kama akina Lema ,Sugu ,Mnyika wapo kimya kiasi hiki ,wanasubiri uchaguzi waanze harakati .Kipindi cha JPM kuna la kusingizia kwamba mlikatazwa mikutano ,sasa mnasingizia nini?

Miezi miwili mlizunguka kanda zote kwa sababu mlikua mnahubiri mambo ya bandari na katiba mpya ,sijui mmeishia wapi, mpo kimya , polisi hawawazuii ,wananchi wapo ,majukwaa yapo ,shida nini?

3.Viongozi wenu ni wahuni
Hili nalisema kwa uchungu sana , viongozi wengi wa upinzani ni wahuni wa madaraka.
Utasikia wanawahukumu Covid 19 ,hawa ni chadema ,kuwa walijipeleka bungeni how?
katika wabunge hao wana mama 19 wabunge karibu 7 ni maahawala na wake wa viongozi wakubwa ,Benson Kigaila mke wake kabisa ni mbunge wa viti maalumu, how comes?

Mnatuaminisha hamjui? Naibu katibu mkuu Salumu mwalimu ana mchumba wake aliyezaa naye ni mbuge wa viti maalumu,mnatuumiza sana wananchi na wananchama, tuwaelewe vipi?

Kaeni chini msameheane yaishe muanze upya .Watanzania wapo,majukwaa yapo njoeni na agenda safi watanzania watawapokea, CCM bila upinzani mizania itayumba , Upinzani imara unahitajika
"Viongozi wao ni wahuni",umemaliza mjadala
 
Ukimwondoa Mchungaji Christopher Mtikila na Chama chake cha D.P. yaani Democratic Party.

Binafsi naona Wapinzani Wengi wa hapa Nchini wapo kwenye vyama kwa ajiri ya Vyeo na Ruzuku tu.

Kama Wapinzani wa hii nchi wangekuwa serious na kuleta mageuzi ya Kisiasa wangesha chukua Nchi.

Jambo hilo limepunguza sana idadi ya wapiga kura. Wengi wanaopiga kura wanapigia maslahi ya uwanachama wa Chama.

Kama Baba Nyumbani ni CUF Basi familia inaipigia kura CUF, ili kukidhi haja za Baba.

Wanachi wengi wanaojiandikisha kupiga kura wanataka vitambulisho vya kujitambulisha ukichukulia uwezo hafifu wa NIDA kutoa vitambulisho vya kitaifa.
Sio kweli, tumeona watu wakiwa wamejiandikisha na kupiga kura, lakini tunachokiona ni uhayawani wa wazi ukiendeshwa na vikundi vya kikatili vya ccm, kura za wizi zikiletwa vituoni kwa uratibu wa vyombo vya Dola na tume ya uchaguzi. Tunaona wapinzani wakienguliwa kwa Hila, na wasimamizi wa uchaguzi wakitangaza kura za udanganyifu Ili kuwapa ushindi wagombea wa ccm, na ushahidi wa uchafu huu upo.

Msitake kupotosha ukweli wa wazi wa kisiasa kwa za zaidi ya miaka kumi na Tano iliyopita. Toka uchaguzi wa 2010 siasa za nchi hii zilibadilika kutoka kikazi Cha zama za ccm, na kuhamia kizazi kipya cha siasa za vyama vingi. Mabadiliko haya ya kizazi ndio yamepelekea ccm kutumia mbeleko ya vyombo vya Dola waziwazi. Kwa Sasa siasa zinaendeshwa na Dola Zaidi kuliko ushawishi wa kisiasa.
 
nikukumbushe kuhusu siasa za Kenya , angalia hizo siasa ziko kwenye mazingira magumu sana ,lakini wapinzani wa kenya wapo solid , hawa wa huku wamelegea sana ,tuukubali ukweli,CCM wamekamata Dola wasitarajie watapewa kama mkate wapinzani
 
Jibu liko sahihi kwasababu ata walioanzisha hivi vyama mnavyovishutumu sasa waliona mambo hayaendi sawasawa wakaamua kuja na chama mbadala.kwahiyo badala yakulalamikia wengine kua hawafanyi au hawatoshi kwenye hiyo nafasi ya upinzani anaweza kuichukua yeye ili azibe hayo mapungufu.
Shida ya wapinzani ndio hii,wakikosolewa wanaanza kusema anzisheni vyama nyie,
Zitto Kabwe alipambana sana kuwashauri ,wakaishia ku attempt kumpa sumu na kumfukuza pamoja na mama yake aliyekua kilema shida salumu, huu ulikua ni uhuni wa hali ya juu kabisa .
Wapinzani wanajiona wamejipata na wameridhika
 
Wanasubiri kufanyiwa.hapo alipo ukimuuliza yeye kama raia amechukua hatua gani anaweza asiwe na majibu,kazi kulalamikia wengine.
Wapinzani wakiambiwa ukweli wanasema tunalalamika, hivi anayekuamsha toka usingizini analalamika?
wapinzani mmepwaya , kuna ombwe kubwa kwenye uongozi wenu na mmeendekeza mapenzi kwenye tawala zenu amkeni
Jointhe chain mmechukua pesa za walala hoi ,badala mkawatembelee mnaishia kuzungula marekani kwa pesa za walala hoi oneni aibu
 
kwa maadili yetu Aliefariki hana nguvu ya kujitetea ,tuwaache waliolala
Maadili yenu ww na nani? Kama alijifanya mjuba akiwa hai, basi atapewa kubwa yake akiwa huko huko mapumzikoni.
 
Hizo hoja unazozitaka wapinzani waziongee mpaka mwisho ni hoja gani hizo?.Kwasababu ratiba ya chadema kupita sehemu mbalimbali ipo na inaendelea.Sio lazima wafanye kwa muda unaoutaka wewe.Lakini pia hizo hoja unataka wazioongee hadi wapi wakati tatizo ni udhaifu wa serikali iliyoko madarakani.Umetoa mfano wa swala la umeme,hebu tuambie unataka waliongelee hadi mwisho wapi angako wewe utaridhika?.Kwasababu mwisho wa swala la umeme ni kupatikana kwa umeme jambo ambalo mkuu wa nchi ameshatoa taarifa nayeye ndiye mmikiki wa tanesco.Au ulitaka wapinzani wajigeuze mabwawa yakuzalisha umeme.Mkiambiwa muandamane mnajifungia makwenu uku mkitoa maneno yakijinga kwamba mnataka na mke wa mbowe atangulie mbele kwenye maandamano mtafikiri mmeambiwa na mke wa mbowe naye ni mpinzani.Unaotakiwa uwalaumu ni walioko serikalini.upinzani unatimiza wajibu wake vinginevyo labla kama unamawazo mengine yakuharibu ambayo unayaona hayafanyiki unataka kuwasakizia wapinzani uku wewe umejifungia kwako.
Ni kweli wapinzani sio mabwawa ya umeme ,na sisi wananchi hatutaki wawe mabwawa ya umeme , tunachotaka wasilalamike bali watoe suluhisho mbadala
siku zote wanaandika vipeperushi mitandaoni ,oooh umeme hakuna serikali imeshindwa ,hatutaki mlalamike hivyo
tokeni mseme serikali ilitakiwa ifanye ABCD ,ilitakiwa ifanye haya na haya ili tuwe na umeme thabiti
wapinzani wamekua kama wananchi wa kawaida ,wanalalamika bila kutoa suluhu mbadala
 
Kasikilize Hansard za bunge ndio ujue wapinzani wamekuwa wakiongea Nini kuhusu umeme. Hizi propaganda za kitoto unazobeba toka hapo ofisi za uvccm hazina maana yoyote.
 
Usiongee mambo kwa kujifanya hujui. Upinzani ulizuiwa kufanya siasa kwa kipindi Cha miaka mitano na bado uchaguzi ulipofika serikali ikapoka uchaguzi na kupeleka CCM. Umesahau mtandao ulikatwa kwa wiki nzima kipindi Cha uchaguzi?. Usiongee kisa upinzani hauna jeshi Wala polisi, ndio maana unadharau.
upinzani wa kenya una jeshi au polisi?
wapinzani wa kenya wana hoja ambazo zina washawishi wananchi kutoka majumbani na kuandamana
wana hoja zinazo waconnect wananchi na shida zao
Ninyi shida zenu haziongelei matatizo halisia ya watu
70% ya watanzania wanaishi maisha basic kabisa , ninyi mmegeuka kusemea shida za 30% ya watu ambao ndio wenye maisha bora .
Kero za mjini na vijijini ni tofauti ,wapinzani wanazunguka zunguka mjini tu hawagusi vijijini ambako ndiko kuna watanzania wanaohitaji kusaidiwa kifikra na kimantiki.
Wapinzani shusheni siasa zenu kwenye kundi la watu wa chini.
Mobilization zenu mnafanyia mitandaoni, club house ,twitter etc , huko kuna watu wa maisha ya nafuu pekee
haakuna mtu anayetumia twitter wa kuandamana
hakuna mtu wa club house anayehudhuria mikutano physical ya chama chenu
shukeni chini mguse shida za watu
 
Uzi makini sana huu. Ila sikubaliani na wewe unavyosema wapinzani wamekosa hoja na agenda. Hapana. Kwa sasa sera yao waliyochagua kama mwelekeo wao mpya ni kupinga kila kitu kwa hoja za matusi. Nahisi kuna maelekezo waliyopeana kwamba kwa sasa tupinge kila kitu na kutukana yeyote atakayekuwa kinyume na sisi. Msigwa ni mhanga wa matusi ya wenzake.
Shida ndio hio mkuu,wapinzani hasa chadema wameamua kushambulia wao kwa wao hawako organized ,wanatukana tu ,yaani kifupi wanasikitisha
sasa hivi angalia wamemsusia hadi Maria Sarungi kushiriki twitter space zake kisa anamuunga mkono Dr Slaa
hizi ndizo akili zao ,yaani atakachosema mbowe wanashangilia ,anayeongea kinyume wanamtukana
Sugu na Lema ni wahanga wa siasa hizi pia
 
Nchi yenye upinzani thabiti ni imara , na nchi ikikosa upinzani madhubuti italegea. Wapinzani wa Tanzania wamekua legelege sana, Nasema haya kwa sababu hizi:-

1.Wamekua wamatukio zaidi kuliko hoja
Leo umeme ukikatika wataongea kuhusu umeme week moja, baada ya hapo ikitokea vita Israel na Palestine ,watarukia habari hizo mpaka zikose mvuto. Hapa kama watanzania upinzani wa namna hii unatukosea.

Tunataka tuone mnachukua hoja moja mpaka mwisho , hawa wapinzani wa sasa hivi ,leo watadai katiba kesho Nape akiongelea VPN hao wanahama wanaanza kutukana , kesho kutwa moto Kariakoo haooo.
Yaan hawana consistency .Badirikeni 2025 mtahangaika sana.

2.Uongozi wao una migogoro mingi sana
Kumeibuka migogoro isiyoisha ndani ya vyama vya upinzani,mfano NCCR mpaka sasa wana gombana
Chadema kuna shida kubwa sana ya uongozi wa juu ambayo inafungwa fungwa , ACT Zitto ana wamanage kidogo vijana wake.

Tatueni shida za ndani ya vyama vyenu ili muingie mtaani kama kitu kimoja, Inaumiza sana kuona vijana wadogo kama akina Lema ,Sugu ,Mnyika wapo kimya kiasi hiki ,wanasubiri uchaguzi waanze harakati .Kipindi cha JPM kuna la kusingizia kwamba mlikatazwa mikutano ,sasa mnasingizia nini?

Miezi miwili mlizunguka kanda zote kwa sababu mlikua mnahubiri mambo ya bandari na katiba mpya ,sijui mmeishia wapi, mpo kimya , polisi hawawazuii ,wananchi wapo ,majukwaa yapo ,shida nini?

3.Viongozi wenu ni wahuni
Hili nalisema kwa uchungu sana , viongozi wengi wa upinzani ni wahuni wa madaraka.
Utasikia wanawahukumu Covid 19 ,hawa ni chadema ,kuwa walijipeleka bungeni how?
katika wabunge hao wana mama 19 wabunge karibu 7 ni maahawala na wake wa viongozi wakubwa ,Benson Kigaila mke wake kabisa ni mbunge wa viti maalumu, how comes?

Mnatuaminisha hamjui? Naibu katibu mkuu Salumu mwalimu ana mchumba wake aliyezaa naye ni mbuge wa viti maalumu,mnatuumiza sana wananchi na wananchama, tuwaelewe vipi?

Kaeni chini msameheane yaishe muanze upya .Watanzania wapo,majukwaa yapo njoeni na agenda safi watanzania watawapokea, CCM bila upinzani mizania itayumba , Upinzani imara unahitajika
Ccm lumumba fc nilidhani ndio utafurahi ili ccm yenu itawale milele sasa kumbe unaona nongwa?
 
Shida ndio hio mkuu,wapinzani hasa chadema wameamua kushambulia wao kwa wao hawako organized ,wanatukana tu ,yaani kifupi wanasikitisha
sasa hivi angalia wamemsusia hadi Maria Sarungi kushiriki twitter space zake kisa anamuunga mkono Dr Slaa
hizi ndizo akili zao ,yaani atakachosema mbowe wanashangilia ,anayeongea kinyume wanamtukana
Sugu na Lema ni wahanga wa siasa hizi pia
Ccm umeanza lini kuwa mshauri wa chadema? Kwa manufaa gani unayopata?
 
upinzani wa kenya una jeshi au polisi?
wapinzani wa kenya wana hoja ambazo zina washawishi wananchi kutoka majumbani na kuandamana
wana hoja zinazo waconnect wananchi na shida zao
Ninyi shida zenu haziongelei matatizo halisia ya watu
70% ya watanzania wanaishi maisha basic kabisa , ninyi mmegeuka kusemea shida za 30% ya watu ambao ndio wenye maisha bora .
Kero za mjini na vijijini ni tofauti ,wapinzani wanazunguka zunguka mjini tu hawagusi vijijini ambako ndiko kuna watanzania wanaohitaji kusaidiwa kifikra na kimantiki.
Wapinzani shusheni siasa zenu kwenye kundi la watu wa chini.
Mobilization zenu mnafanyia mitandaoni, club house ,twitter etc , huko kuna watu wa maisha ya nafuu pekee
haakuna mtu anayetumia twitter wa kuandamana
hakuna mtu wa club house anayehudhuria mikutano physical ya chama chenu
shukeni chini mguse shida za watu
Mwamba upo vizuri sana kwenye kujenga hoja tunahitaji watu wa dizaini yako wengi hapa jamiiforum
 
Back
Top Bottom