Upishi wa Biskuti za Tangawizi

Upishi wa Biskuti za Tangawizi

Nlipata vifungashio naanza kutengeneza, tumpiku Chaibiscuit ya Azam
 
Yasitokee tu mangumbaru yakaanza kusema eti una mikono mizuri...

Na mimi ndio wasiwasi yangu ilipo hapo kosa izungumziwe biskuti wajaa laana wataanza kutamani mikono mweupe, minene, mizuri ambayo vinyweleo ina ushirikiano na mwili achana na vinyweleo vilivokosa uelekeo,
 
Habari zenu wakuu, natumai mnaendelea vizuri. Jumamosi iliyopita niliwaletea mapishi ya wali, samaki wa nazi na mboga. Wiki hii nitapika Biskuti za Tangawizi.

Biskuti hizi zinaweza kuliwa na maji, chai, maziwa, kahawa, juisi nk. Usipomaliza kuzila muda huo unaweza kuzihifadhi kwenye kontena sehemu isiyo na jua.

Ukipenda kuangalia video ya haya mapishi unaweza kuangalia hapo chini. Ukipenda unaweza “kuilike” hiyo video, “kusubscribe” kwenye channel yangu na kuangalia video nyingine.



Mahitaji ya Biskuti za Tangawizi
350g Unga wa Ngano
1 tsp (kijiko cha chai) Magadi Soda
2 tsp tangawizi ya unga
115g siagi
175g sukari
4 tbsp (kijiko cha chakula) Golden Syrup
1 yai lililopigwa

Tunaanza kwa kuchekecha unga, magadi soda na tangawizi kwenye bakuli.

View attachment 2480746
Unga wa ngano

View attachment 2480747Magadi Soda

View attachment 2480748
Tangawizi

View attachment 2480750
Nikichekecha unga, magadi na tangawizi

Baada ya hapo unaweka siagi iliyolainika, na kuichanganya mpaka mchanganyiko ufanane na chenga za mkate. Tunamalizia mahitaji makavu kwa kuchanganyia sukari.
View attachment 2480751
Siagi laini

View attachment 2480752
Nikichanganyia siagi

View attachment 2480753
Nikiweka sukari

Tunaweka Golden Syrup (hii nilinunua supermarket) na yai liliopigwa na kuukanda mchanganyiko wetu kwa muda kidogo.
View attachment 2480755
Golden Syrup

View attachment 2480758
Nikipiga yai

View attachment 2480759
Nikikanda unga


Baada ya kukanda unga wetu, tunausukuma kama chapati na kukata vipande kwa maumbo mbalimbali.
View attachment 2480760
Nikisukuma mchanganyiko wetu

View attachment 2480762
Nikitumia kikombe cha bati kukata vipande

View attachment 2480765
Maumbo ya duara

View attachment 2480766
Nikikata umbo kama mtu

Baada ya hapo, tunachukua vipande vyetu na kuviweka kwenye tray lililopakwa mafuta au siagi kwa ajili ya kuoka.
View attachment 2480767
Nikiweka vipande kwenye tray

View attachment 2480768
Vipande vikiwa kwenye tray tayari kwa kuoka

Ukioka kwenye oven, biskuti zitatumia dakika 10-12 hadi ziive kwenye joto la 190 C. Muda utakaotumia kuoka utalingana na namna unavyopenda biskuti zako ziive. Mimi nimependa zangu ziive zaidi na zitakaa muda mrefu zaidi.
View attachment 2480769
Biskuti zikiwa kwenye oven

View attachment 2480770
Biskuti zikiwa zimeiva

View attachment 2480771
Biskuti za tangawizi

View attachment 2480772
Biskuti za Tangawizi kwa ukaribu

View attachment 2480773
Biskuti ya tangawizi kwa ndani

Nje ya Mada,,,Viganja vyako tuu,,,Mash',,llahh!!!
 
IMG_7884.png

Mi tayari
 
Back
Top Bottom