tofyo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 2,755
- 764
Habari wakuu,
Samahani kwa kuchelewesha habari, kwasababu za kiusalama.
Lakini Taarifa hii iende kwa askofu mkuu wa Jimbo la Geita na mamlaka zingine za serikali. Nyuma ya eneo la kanisa jimboni ipo njia ya mkato kwa wenyeji wa Geita kukatiza kutokea Nyankumbu mbugani kutokea Geita mjini.
Hio njia imekuwepo kwa mazoea kwa miaka mingi Sana, lakini hivi karibuni Kama mwezi hivi umepita, kanisa limeweka walinzi wenye bunduki katika hio njia na wala Hakuna tangazo lolote linalokataza au kuzuia hio njia,
Uhalifu ulipo
Ikitokea ukapita kwanza unaelekezewa mtutu wa bunduki na kuambiwa kaa chini, unaambiwa hii njia hairuhusiwi kupita, na wanakwambia wewe ni mvamizi, na hivyo unatakiwa kulipa Laki tatu(300,000)
Ukishindwa kabisa wanakuomba elfu hamsini 50,000 na ukishindwa unapata kipigo ambacho hujawahi kukutana nacho. Hio haina mahusiano yoyote na uharibifu uliotokea hivi majuzi since kwamba huo ulinzi imekuwepo zaidi mwezi mmoja Sasa. Na walinzi wanasema wapo hapo kwaajili ya kulinda mahindi.
Na Leo nimeweka hii kwasababu tayari muhalifu alieharibu Mali za kanisa amepatikana. Ningeweka kabla ingeonekana kunakitu nataka nihalalishe.
Uhalifu huo wa uharibifu Mimi nimetafsiri Kama LAANA ya kile kinachoendelea kule nyuma ya Jimbo, kanisa lime deploy manyang'anyi badala ya walinzi. Uhalifu huo upo na watu wanalia Sana Kama hamtaki watu wapite, wekeni Bango la tangazo ili watu wawe na Taarifa, na atakae kaidi Basi hatua za kisheria zifuatwe, na sio kulazimisha utoe rushwa ya 50,000 na zaidi au kipigo.
Bila ya shaka Jamii forums ipo kwa ajili ya kufichua uovu.
🤚Naapa ya kwamba ushuhuda ninao utoa NI kweli tupu. Ee Mwenyezi Mungu nisaidie.