Baadhi ya watu wanaamini upole ni udhaifu.
Upole ni nini? Upole ni sifa muhimu inayomtafsiri mtu anaechukulia mambo kwa uzito bila kukurupuka. Mpenda haki, asiependa lawama.
Mungu mwenyewe ni mpole ndio maana hajachukua hatua ya kuwaondoa waovu mapema,amewapa muda wa kutafakari.
Musa alikua mwanadamu mpole zaidi duniani na hakujawahi kutokea tena. Upole sio udhaifu.
Upole ni sifa moja ya ajabu sana.
Wakati fulani nikiwa kwenye course fulani ya kujiendeleza kielimu,kuna siku nilichelewa kuingia kwenye kipindi.
Yule muongozaji wa kipindi alikuwa ni kijana kama mimi tu,inifokea sana kwa nini nimechelewa,nilikuwa na uwezo wa kumjibu mbovu sana tu.
Lakini nikamkaushia kila analoniambia natikisa kichwa kwamba mimi ndio nimekosea ni kweli,tena kwa ustaarabu kabisa namuitikia,kila akija juu mimi nakuja chini,tena alikuwa ananipandishia mbele ya mademu na wana darasa wengine,nikakausha nikasema mista kweli nimefanya kosa.
Akaniambia nikakae kwa hasira mimi nikaenda kwa utaratibu sana nikakaa,daah tule jamaa tokea siku hiyo ananiheshimu sana maana alijua kama ningemjibu.
Alafu hata wanadarasa wakamuona yeye ndio kilaza,wakamuona yeye ndio ana kisirani kwa nini akapanic vile.
Ila ningiamsha pangenuka sana yani.