Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Hivi kwa unavyofikiri hakuna kabila lenye washamba? Na ushamba unaoongelea hapa ni upi? Kila kabila lina washamba. Na kila kabila linakujitofautisha na makabila mengine. Iwe mchaga, iwe, Mnyakyusa, Mhaya na hata mndengereko, hawa wote ukiwa unaishi maeneo yao wana hali ya kutenga kutokana na uasili. Uwezi kwenda kwa makabila haya na mengineyo wakakubali upate ubunge au udiwani katika maeneo yao.Magufuli hakuwa kiongozi wa wasukuma pia usiwakumbushe machungu na maumivu waliyoyapata Wasukuma kutokana na utawala wa magu, kuanzia bariadi, Itilima, Kisesa, Meatu, Maswa ngo'mbe za wasukuma zilitaifishwa bila huruma kwa kuwa zimekula malisho ya pori la akiba la Maswa ( Maswa Game Reserve),
Ukienda huko ziwa Victoria kuanzia mialo iliyopo huko mkoani Geita mfano NKOME jimbo la geita vijijini kwa ndugu Musukuma, Sengerema kwa ndugu Tabasamu, pamoja na maeneo mengine ya mwaloni wasukuma waliuawa, kuchomewa nyavu/makokoro, kutaifishwa kwa boti zao etc, hivyo unapotaka kujipendekeza kwa utawala wa mwenda zake uyapime maandishi yako in relation to matendo na uhalisia wa utawala wa awamu ya tano.
Hata hivyo waasukuma wana ukabila sana hasa huko NTUZU kwa joka la makengeza hawapendi kuona mgeni anapata nafasi eg madiwani wa kanda hii hawawapendi watumishi wasio na asili ya usukumani, hawapendi kuona mgeni anafanikiwa ktk eneo lao, utapigwa figisu za kila aina usifanikiwe ikiwemo ndumba, kuibiwa, dhulma, ujambazi etc. Ole wako ukumbane na mnyantuzu mwenye hela au msomi mwenye vyeo vyake wanadharau siyo ya dunia hii eg Joka la makengeza limeibeba hii trait 100%.
Usidanganye watu humu kuhusu wasukuma nimefanya kazi kuanzia Geita, Mwanza, Shinyanga kwa zaidi ya miaka 20 nawafahamu vizuri na pia kwa taarifa yako kwa picha aliyoionesha anko magu hakuna msukuma atakamata nafasi kubwa hasa urais ktk nchi hii kwani wasukuma mmefeli sana kwanza character ya ushamba ambayo mnayo kiasili imekuwa ndo sifa kuu ya uongozi wa magu hebu tazama vituko vya makonda enzi zake.
Mwisho naona unajaribu kuwashawishi wasukuma wasiikubali CDM unajidanganya bure na aliyekutuma mwambie kachelewa kuanzia shinyanga mjini, Simiyu, Mwanza hadi Geita wanaikubali sana CDM pia Wasukuma siyo wajinga kama unavyowaza kama ambavyo ccm inategemea watu mbumbumbu mambo yamebadilika hivyo ccm itaendelea kujipachika polisi, tiss, mahakamani lakini ikisema ijitokeze usano mwa watz bila hizo nyenzo itapata kipigo cha mbwa koko.
Nashukuru naifahamu Tanzania yote. ushamba huko kila sehemu. Uwezi sema wasukuma ni mwisho kushika madaraka, weye ni nani ambae utatoa hayo maamuzi?
Mwl Nyerere alishawahi kusema kabila kubwa la wasukuma si vizuri wakashika madaraka, na hata akawataja wachaga kwa ubinafsi walio nao. Lakini ikatokea Magufuli kashika madaraka hayo ambaye ni msukuma. Na nina amini ipo siku atatokea mchaga atakuwa Rais wa hii nchi. Kosa la mtu mmoja aliwezi hukumu jamii nzima.
Ila fahamu kwanza wasukuma ni wapole lakini ni wakali sana na wakorofi unapotaka kuingilia kile wao wanachokiamini. Na hawayumbi katika maamuzi yao, na siku zote ni watu wa haki. Nenda usukumani ambako bado wanashikilia mila zao za jadi na jeshi la sungusungu. Na niwachapa kazi haswa.
Swala la mifugo kuuwawa, uvuvi nyavu kuchomwa alijaanza wakati wa Magufuli. Limekuwepo kwa miaka kama unakumbuka Operation tokomeza, wakati wa Kikwete hadi ikaleteleza baadhi ya mawaziri kuachia nafasi. Watu waliteswa na kuuwawa.
Nimeishi usukumani nikafanya kazi huko mikoa yote ya kanda ya ziwa na wilaya zake. Hivyo naijua uzuri Sukumaland.