Upolisi sio profession?

Upolisi sio profession?

Vichekesho

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
66
Reaction score
3,277
Nijuavyo mimi ma professional wakweli hawatakagi kupangiwa na wanasiasa hasa kama kinachopangwa ni kinyume na taaluma yao.

Kwanini polisi wakiambiwa kamata wanakamata kweli wakati wanajua wazi kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yao? Ilibidi Mkuu wa Wilaya akiamuru kamata huyu weka ndani, askari aseme sikamati mpaka nijue kosa lake.

Halafu baada ya hapo uongozi wa polisi unafanya press conference kulaani wateule wanao jichukulia sheria mkononi na kuwapnya kuwa wakirudia watatiwa nguvuni.

Mwisho wa ndoto.
 
Profession*

Naomba uzi usomeke upolisi sio profession

One could argue that a modern profession must have a protracted period of formal training in some body of abstract knowledge and a strong service orientation. This is contrary to the process that one must go through in order to become a police officer in Bongo Land.
 
Maprofesa wa jalalani?..wanasiasa ndo top kwa tz...kuna jamaa nilisoma nae sasa alinisimulia kitu mpaka nikaona aibu mm...eti mwanasiasa alienda kumkagua akakuta sehemu ya kazi ni chafu ...basi akamwambia adeki nae akadeki kweli...niliona aibu mimi
 
Jiulize kwanini mbunge akiwa kwenye ziara zake hawezi kuwaelekeza kuwa kamata huyu muweke ndani na wakatekeleza.

Wakuu wa wilaya wanatumia Sheria ya Tawala za Mkoa, Sura ya 97 na Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa Sura ya 61 ambayo inawapa power ya kutoa amri ya mtu yeyote kukamatwa na kumuweka mahabusu kwa saa 48
Kitendo cha sheria kumruhusu tu mkuu wa wilaya kutoa amri ya kukamata polisi hatakiwi kupinga amri hiyo polisi atatekeleza amri yoyote iliyo kisheria.

Sasa ili polisi akatae ni hiyo sheria ibadilishwe na wakuu wa mikoa na wilaya wanyang'anywe haki hiyo, polisi wao ni law enforcers hata ikitungwa sheria kuwa kunywa maji hadharani ni kosa kisheria na ikapitishwa bungeni yeye atakuja kukukamata , kilichopo hapo ni baadhi ya sheria kufanyiwa mabadiliko
 
Nijuavyo mimi ma professional wakweli hawatakagi kupangiwa na wanasiasa hasa kama kinachopangwa ni kinyume na taaluma yao.

Kwanini polisi wakiambiwa kamata wanakamata kweli wakati wanajua wazi kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yao? Ilibidi Mkuu wa Wilaya akiamuru kamata huyu weka ndani, askari aseme sikamati mpaka nijue kosa lake.

Halafu baada ya hapo uongozi wa polisi unafanya press conference kulaani wateule wanao jichukulia sheria mkononi na kuwapnya kuwa wakirudia watatiwa nguvuni.

Mwisho wa ndoto.
Watakuwaje professionals akili zenyewe hizi 👇

Yaani badala ulaum sheria wewe unalaum polisi . Anaempa maelekezo polisi nae hufuata sheria
 
Waganga pekee ndo wanapelekesha hadi hao wanasiasa, wakisema vua nguo, hakuna wa kupinga.
Wanasiasa wenyewe wanatembelea kario wakiwa kwa Waganga wao.
 
Nijuavyo mimi ma professional wakweli hawatakagi kupangiwa na wanasiasa hasa kama kinachopangwa ni kinyume na taaluma yao.

Kwanini polisi wakiambiwa kamata wanakamata kweli wakati wanajua wazi kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yao? Ilibidi Mkuu wa Wilaya akiamuru kamata huyu weka ndani, askari aseme sikamati mpaka nijue kosa lake.

Halafu baada ya hapo uongozi wa polisi unafanya press conference kulaani wateule wanao jichukulia sheria mkononi na kuwapnya kuwa wakirudia watatiwa nguvuni.

Mwisho wa ndoto.
Kwanza tunapaswa kujua kuwa;
POLICE -sio Jeshi
POLICE -sio Askari bali ni RAIA WAKAKAMAVU.
Huu ni ukweli wasiopenda kuusikia na wapo tayari kugombana kwaajili ya kutetea sifa wasiyo stahili.
JESHI ni;JWTZ[TPDF]
pamoja na WANAMGAMBO
Huko ndipo walipo ASKARI.
Police imejazwa sifa za kijinga na wanasiasa hadi wamejiona wao ni Security guard ya chama cha siasa.
 
Back
Top Bottom