Uporaji pesa za mkopo za wanafunzi Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

RoadLofa

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,509
Reaction score
3,313
Imekuwa ni utaratibu wa chuo cha uhasibu Arusha kukata kiasi cha pesa cha chakula na matumizi mengine(Boom) kwa wanufaika wake kila mara wanapotakiwa kuwapa kwa muda wa kila baada ya miezi miwili, ambacho ni kiasi cha tsh 500,000 kwa kila baada ya miezi miwili.

Lakini wamekuwa wanawacheleweshea kwa kuvusha siku zaidi ya miezi miwili na wanapokuja kuwapa, huwapa kwa kuhesabu siku zilizobaki kumaliza miezi miwili, bila kujali kama wamewacheleweshea Boom zao na kuna muda wameishi kwa pesa zao.

Kwa mfano kwa mwezi huu Boom wametoa leo kwa kuwakata 70,000 Tsh kila mwanafunzi kwenye 500,000 Tsh ambazo alitakiwa kupewa kwahiyo kila mwanafunzi amepewa 433,000.

Kwanini wanashindwa kuwapa wanafunzi pesa zao wakati ni pesa za walipa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na haijulikani ni maagizo kutoka juu au wanakata pesa za students kwa ajili ya Projects zao za ujenzi chuoni.

Naomba wanafunzi wasaidiwe kupaza sauti ili taarifa iwafikie watu wanaoweza kuwatetea wanafunzi dhidi ya uonevu🙏
 
Kwa nini wanachuo wasifanye maamuzi ya kuwashitaki hao wanao fanya kitendo hicho
 
Boss hata hawaelewi wafanye nini maana hii ni mara ya pili sasa kuna kipindi baada ya kurudi kutoka likizo baada ya break ya COVID-19 kuisha na kurudi chuo wanafunzi walitaka kusainishwa 170,000 kila mwanafunzi ila wakagoma baada ya mgomo kila mwanafunzi akaongezewa 50,000 tu ndo wakakubali kusign kwa shingo upande kwa sababu ya shida.

Hilo swala limejirudia tena leo kila students katumiwa messages ya Boom 433,000 badala ya 500,000 na kusign itakuwa next week hapo ndo wanafunzi wanashindwa wafanyeje kuhusu izo 70,000 kila mwanafunzi walizokatwa, wagome au wasigome,sasa hawaelewi ni maamuzi kutoka juu HESLB au ni kutoka kwa mkuu wa chuo Prof. EliAmani Sedoyeka.
 
Dah! Huyu mpare mbona anataka kuchukua tabia za majirani zake.

Ila kwa vile habari imefika hapa naamini itafanyiwa kazi vyema.
 
Boss hata hawaelewi wafanye nini maana hii ni mara ya pili sasa kuna kipindi baada ya kurudi kutoka likizo baada ya break ya COVID-19 kuisha na kurudi chuo wanafunzi walitaka kusainishwa 170,000 kila mwanafunzi ila wakagoma baada ya mgomo kila mwanafunzi akaongezewa 50,000 tu ndo wakakubali kusign kwa shingo upande kwa sababu ya shida.

Hilo swala limejirudia tena leo kila students katumiwa messages ya Boom 433,000 badala ya 500,000 na kusign itakuwa next week hapo ndo wanafunzi wanashindwa wafanyeje kuhusu izo 70,000 kila mwanafunzi walizokatwa, wagome au wasigome,sasa hawaelewi ni maamuzi kutoka juu HESLB au ni kutoka kwa mkuu wa chuo Prof. EliAmani Sedoyeka.
Kama hawajasaini, wasisaini hadi waongezewe hicho kiasi au waelezwe kwa majibu ya kuridhisha zilizopelekwa hizo pesa.
 
Pumzika kwa Amani JPM

Boss hata hawaelewi wafanye nini maana hii ni mara ya pili sasa kuna kipindi baada ya kurudi kutoka likizo baada ya break ya COVID-19 kuisha na kurudi chuo wanafunzi walitaka kusainishwa 170,000 kila mwanafunzi ila wakagoma baada ya mgomo kila mwanafunzi akaongezewa 50,000 tu ndo wakakubali kusign
jingalao
Kwani kipindi hiko cha break ya C19 mwaka 2020 mwanzoni marehemu jiwe hakuwepo?
 
Kwanini kuna ufisadi huo.

Hela ya boom inatoka bodi moja kwamoja kupitia bank kwenda kwenye account ya mwanafunzi. Acheni kutumia makaratasi ya kusaini ombeni muanze kutumia finger prints.

#MaendeleoHayanaChama
 
jingalao
Kwani kipindi hiko cha break ya C19 mwaka 2020 mwanzoni marehemu jiwe hakuwepo?
Alikuwepo ndo kipindi ambacho wanafunzi walitaka kupewa 170,000 kutumia ndani ya miezi 2 badala ya 500,000 wakagoma kusign wakaongezewa kila mmoja 50,000 wakasign , kwa iyo kila mmoja akasign 220,000
 
Uporaji=nkajua wazee wa ngwasuma washafanya yao

Ova
 
Eti wanafunzi hawajui cha kufanya.Wasaini au wasisaini! Hii inaonesha elimu mliyoipata huko nyuma na mnayoipata sasa hapo chuoni ni dhaifu kabisa kwa sababu haiwawezeshi kujua hatua za kuchukua mnapopata changamoto hadi msaidiwe na watu wengine kwa kuwashauri cha kufanya.Mimi najua mnachotakiwa kufanya ili kupata ufumbuzi wa kudumu lakini sitawambia.
 
Back
Top Bottom