DOKEZO Uporwaji wa ardhi unaoendelea katika maeneo Iyumbu, Dodoma

DOKEZO Uporwaji wa ardhi unaoendelea katika maeneo Iyumbu, Dodoma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

ABBAS75

New Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1
Reaction score
0




BARUA YA WAZI KWA WAZIRI MHE.ANGELA MABULA NA WATENDAJI WAKE.
KILIO CHA WATANZANIA KWA OFISI ZA ARDHI DODOMA – WATU WANAPORWA HAKI ZAO​

Tunawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni kilio, majozi na damu kwa Wananchi wa Iyumbu – Dodoma juu ya uporwaji wa ardhi unaoendelea katika maeneo yetu na hakuna msaada uliopo kwenye taasisi husika hivyo tumeona ni vyema kuandika barua hii ya wazi iweze kufika kwa Waziri mwenye dhamana ajue kile kinaendelea katika wizara yake na jinsi watanzania wanavyopoteza haki zao wakati mamlaka zote zipo na zinatazama tu hata mamlaka zingine kushiriki wizi huu uliopindukia tena wa wazi wazi.

Mhe. Angela Mabula pole na majukumu, tunapenda kukuelezea juu ya uwepo wa watendaji wako wanaoshirikiana na Ndugu Saimoni Gerald Manyara kupitia kampuni yake inayoitwa TANMARK COMPANY LIMITED kupora viwanja na maeneo ya watanzania kinyume na taratibu za nchi.

Kwa nyakati tofauti tumefuatilia mtu mmoja mmoja kutaka kupata haki zetu lakini kuna baadhi wamefanikiwa kwa kutumia njia ngumu sana ili tu kupata haki zao lakini asilimia kubwa changamoto hii bado ipo na Bwana Saimoni akiendelea kuuza viwanja vya watu huku akishirikiana na watendaji baadhi wa vijiji akiwemo Ndugu. Joseph Julius Remy kutengeneza mikataba feki kuchukua viwanja vya watanzania huku wakipeleka kesi polisi na kuwatisha wananchi kupitia Askari anayejulikana kwa jina la Chalamila yuko ofisi za mkoa na bado Ndugu Saimoni ana mtandao wake wa majizi wenzake pale ofisi za JIJI hawa tutakutajia Mhe. Waziri na taasisi za uchunguzi zifanye kazi zake maana pale JIJI unaweza kuuziwa kiwanja mara mbili na wale watendaji bila hata kujali kuwa kuna migogoro, hawa watu tutakupa majina yao kamili sasa wewe utaona ukweli katika hili maana tumeteseka kwa muda mrefu sana bila mafanikio, tunajua liko ndani ya uwezo wako ndio maana MAMA SAMIA akakuamini kusimamia wizara hii.

Tunaomba uchukue hatua za haraka kufuatilia jambo hili kabla hata hawajasafisha nyumba yao maana wako tayari kutengeneza nyaraka za uongo ili kupoteza ushahidi japo najua wananchi wakichoka tutawageuza mishikaki kule Iyumbu maana tukiwaona watendaji wako tunaona taswira ya wezi katika maeneo yetu maana wanashirikiana na wezi kila siku.

Mwisho kabisa tunaomba ufanye uchunguzi wa kina katika ofisi zako kote nchini tukiamini kabisa kuwa wizi unaofanyika Iyumbu karibu na makao makuu ya nchi ni mfano tu wa kile kinaendelea nchi nzima katika sekta ya Ardhi na Watanzania wengi wanapoteza haki zao huku mamlaka zikiacha kazi zake na kugeuka kutumiwa na watu kama kina Saimoni Gerald Manyara kufanya wizi kwa maslahi yao binafsi.

Mungu akufanikishe Mheshimiwa katika kutatua kero za wana Iyumbu na Tanzania kwa ujumla.

Mungu ibariki Iyumbu, Mungu ibariki Dodoma, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Wako katika kujenga Taifa,

Wananchi wa Iyumbu – DODOMA.

Okoa IYUMBU Okoa DODOMA Okoa TANZANIA.​
 
Poleni sana,na sidhani hapa nchini,kuna mahali zaidi ya Dodoma,ambako viwanja vinauzwa kwa kasi,maana duuuuh!.
Kama dhuluma imetamalaki,sijui msaada itakuaje,maana imenenwa,kila mmoja ale kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Back
Top Bottom