Takwimu zinaweza kutumika katika nyanja mbalimbali kama vile sayansi, biashara, sera, elimu nk ili kusaidia katika kufanya maamuzi mbalimbali na ikiwa takwimu hizo zitakuwa potofu zitasababisha kupatikana kwa matokeo potofu yatakayoharibu malengo na mipango ya jambo kusudiwa.
Udanganyifu wa takwimu huweza kutokea au kufanywa katika uchambuzi wa data au utafiti. Wakati data zinakusanywa, kuchakatwa, na kuanaliziwa kunaweza kufanyika upotoshaji au udanganyifu wowote ili kutimiza lengo lolote lililokusudiwa katika upotoshaji huo.
Udanganyifu wa takwimu unaweza kusababishwa na mambo kama vile
- Kuwapa Upendeleo kundi au watu fulani kwa kusudio la kuwanufaisha au kujinufaisha.
- Makosa katika kukusanya au kuchakata data
- Kubadilisha au kuwasilisha takwimu kwa njia isiyo sahihi kwa makusudi ili kuleta matokeo yanayotakiwa na wanaofanya udanganyifu huo.
- Kuua maoni ya watu
- Kutafuta sifa na umaarufu
- Kupindisha mijadala
Mtafiti hukusanya taarifa zisizo za kweli ili kuonesha kundi fulani linakubalika na watu, au limeshinda jambo fulani au hakuna tatizo sehemu au kuna tatizo kutokana na mpotoshaji anavyokusudia. Kwa kitaalamu tatizo hili huitwa 'Sampling Bias"
Makosa katika kurekodi au kuchakata data
Data zinaporekodiwa kwa umakini mdogo zinaweza kosewa na kuleta namba tofauti na uhalisia na hivyo kusababisha upotofu wa matokeo ya data hizo.
Kubadilisha au kuwasilisha takwimu kwa njia isiyo sahihi kwa makusudi ili kuleta matokeo yanayotakiwa na wanaofanya udanganyifu huo.
Data zinaweza kusanywa zikiwa sahihi na kisha wenye lengo la udanganyifu wakaongeza au kupunguza namba ili wapate wanachokusudia.
Ili kuepuka matatizo haya, inashauriwa kuchukua takwimu kutoka katika vyanzo vya kuaminika, na kama ni taarifa kutoka kwa watu binafsi ziwe zimechapishwa kwenye jarida(journal) linloaminika kuaminika.