Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Mods and Wachangiaji, ninachoandika hapa ni kitu kikubwa na nashauri tahadhari ichukuliwe mapema. It is very serious.
Siku ya Jana nikiwa kwenye majukumu yangu ya kutafuta riziki, nilipaswa kufika kwenye shule X huko kanda ya MAGHARIBI ili kuonana na Mkuu wa shule kwa akili issue Fulani.
Nilikua na kijana ambaye ndio aliyekua Mwenyeji wangu kwa eneo lile. Yule kijana alinipokea bag langu ambalo lilikua na laptop, kikoi cha kimasai na documents kadhaa hivyo kulifanya lionekane kutuna.
Wakati tunaingia eneo la shule ile, ni shule ya msingi ilikua ni muda wa SAA NNE asubuhi ambapo walikua mapumziko. Niseme ukweli, sikujua kitu, kumbe watoto walikua wakitimua mbio wakidhani tumeenda shuleni "kuwachanja" chanjo ya COVID-19.
Mwalimu mmoja wa kike alianza kucheka na kutujulisha kuwa watoto wale walikua wanakimbia wakidhani tumeenda pale kwa ajili ya chanjo na kwamba inaonekana Wazazi wao wamewaonya watoto wao kutokukubali kupata chanjo kwa madai kwamba watakufa.
Niliingia ofisni kwa Mkuu wa shule na nilimweleza masikitiko yangu, hata hivyo Mwalimu wa zamu aligonga kengele na kuwakusanya tena maana walishakimbilia porini.
Wakati tunaondoka pale shuleni, nje kidogo ya shule kuna Wenyeji wa pale vijana na watu wazima walikua wakippakia mizigo (nadhani ni magunia ya maharage au mahindi) basi waliitana wakaanza kuturushia maneno ya dhihaka na kejeli huku wakitutisha kwamba, Ole wetu kama tungewapa chanjo watoto wao.
Kumbe walikua wakifuatilia tukio lile kwa mbali na walikua wakiongea kilugha.
Wito wangu kwa serikali, HII BRAINWASH ni kubwa sana na huenda ikaja kuleta madhara kwa wahudumu wetu wa afya, serikali iwaelimishe watu wake na WAPOTOSHAJI wachukuliwe hatua.
Hiki nilichoandika ni serious na ni tukio halisi