#COVID19 Upotoshaji wa Chanjo ya CoVid 19: Nusura nijeruhiwe na Wanakijiji

Mungu atusaidie! Tumefanywa wajinga pakubwa
 
Majukwa yanatawala pro chanjo tu, anti chanjo wamepotea, Sasa kama chanjo ni hiari ya nini kuparurana kati ya wanaochanjwa na wasiochanjwa? Au ni kutaka sifa tu kuwa wamechanjwa wengi covax wafurahi? Kama waliaminishwa tangawizi na malimao yana kinga tatizo liko wapi? Hiyo chanjo watachanja tu kadiri ya muda unavyoenda na hali ya maambukizi itakavyokuwa
 
Binafsi nakumbuka suala la chanjo kupingwa lilikuwepo tangu zamani! Sijajua kwa wenzangu!

Suala hili tunaliona kama dogo lakini inahitajika elimu ya kina kuhusu chanjo hii, na NAWASHANGAA SANA MNAOWAONA WANANCHI KAMA WAJINGA KWENYE HII CHANJO.


Tulitumia muda mwingi kuwaambia hazifai lakini leo tunawaambia zinafaa then tunataka watuelewe? Hebu tuwe serious, tunapaswa tuwaeleza kikichotukia kipindi hicho na sasa ndio itawafanya kuelewa chanjo. Tusiwabeze, tunapaswa kuwapa elimu kama Naibu waziri wa Afya alivyofafanua juzi kuwa ni kuwapa darasa tu na si kuwaona kama wanapinga!!


HII ISHU YA KUCHANJWA SI TU INAGOMEWA VIJIJINI HATA MJINI HAPA, NILISIKIA HABARI PIA JUZI SHULE MOJA WANAFUNZI WAMEKIMBIA SHULE BAADA YA KUONA GARI YA AMBULANCE HUKO.MKOA WA MANYARA KAMA SIKOSEI!

Tupeane elimu na si kubezana!! Tuambiwe authenticity ya msimamo wa wataalamu wetu hapo mwanzo na Sasa!!
 
Pole sana Mkuu.
 
Unakuta mzee wa miaka 70 anasema wanataka kutuchanja ili kutuharibu vizazi tusizae,unaishia kushangaa mzee wa miaka 70 anawaza kuzaa,
Taaaabu sana
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Pole mkui,Jiwe aliharibu Sana hii nchi ,pole Sana mkuu..hao ni kuwaacha hivyo hivyo siku wakigongwa na Mdude wataitafuta tuu chanjo.

Na hii nchi ilivyojaa watu wajinga ni jambo la kusikitisha sana
 
Awali walikuwa wanafundisha eti kuvaa barakoa ni kukosa imani kwa Mungu,
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Yaani hii nchi inachekesha Sana,chanjo ya mzungu inaleta vituko ,dini ya mzungu inashadidiwa haaaaa
 
Jipe muda wa kupata elimu ya chanjo ni nini,na inafanya nini,ubishi hautkufanya ujue kweli
 
Hapa ni kweli watu waliopinga njia za kisayansi inawezekana vipi leo wanadai chanjo ni sahihi? Hawa walipotosha watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…