#COVID19 Upotoshaji wa Chanjo ya CoVid 19: Nusura nijeruhiwe na Wanakijiji

Ila hayakuanza leo. Shida hii ni ya kihistoria. Ninakumbuka miaka ile tukiwa mashuleni, watu wa afya wakija kutoa chanjo inakuwa balaa. Nishawahi kuishia mwituni kukimbia hawa watu, eti, tunakimbia wanyonya damu, chinjachinja, waumiani. Kha!

Sasa hii ya UVIKO ni mbaya zaidi maaana baadhi ya watu wenye influence ndiyo wanapotosha balaa
 
Hapa kwangu nimeshawishi watu wangu tukachomwe hizo sindano...majibu nimeambiwa kuwa niende mwenyewe Mimi msaliti wa JPM...kuwa leo nimebadilika na nijiandae kuganda damu na kufa...🤣🤣
Wanaongea hadi wasomi...unashangaa sana....
 
Na mbaya zaidi, kuna jitihada ndogo sana kutoka serikalini kuelimisha watu
 
Hapa kwangu nimeshawishi watu wangu tukachomwe hizo sindano...majibu nimeambiwa kuwa niende mwenyewe Mimi msaliti wa JPM...kuwa leo nimebadilika na nijiandae kuganda damu na kufa...🤣🤣
Wanaongea hadi wasomi...unashangaa sana....
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Msimamo wa muda wote wa serikali juu ya Covid umekuwa ukiyumba yumba...

Kunawa mikono na sabuni (enzi zile twaambiwa corona ni futa tu)>> Maombi >> Nyungu seasons zote >> Chanjo...sasa huenda kuna watu bado wangali hapo namba moja na mbili...
 
Jana nimeshuhudia mzazi aliyemtandika viboko mwanaye na kumrudisha shule. Alitoroka na wenzake eti shuleni kwao wanachomwa sindano za chanjo.
Akiwa anamuelezea mwenyekiti wa mtaa, naye alimsistiza wazazi kuwaondoa hofu watoto maana hilo suala amelisikia kwa wengine pia.

Shida ipo kubwa.

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
Hapa kwangu nimeshawishi watu wangu tukachomwe hizo sindano...majibu nimeambiwa kuwa niende mwenyewe Mimi msaliti wa JPM...kuwa leo nimebadilika na nijiandae kuganda damu na kufa...[emoji1787][emoji1787]
Wanaongea hadi wasomi...unashangaa sana....
Mimi na ka elimu kangu haka,chanjo sitaki na wala sihusianishi na dini wala nani.

Ishu ni kwamba hii chanjo ni propaganda na haina impact kubwa katika kuratua tatizo,

Yani mtu unapigwa chanjo harafu barakoa unaendelea kuvaa,na unaweza pata ugonjwa,sasa hapo kuna maana gani ya chanjo?

Bora nibakie hivi hivi na niendelee kuchukua tahadhari za corona na sio kudungwa vitu ambavyo hata serikali haitahisika nikidhurika.

Nyie wasomi na waelewa chanjeni tu
 
Huyu aliyewa-brainwash alaaniwe popote pale alipo awe hai au amekufa
 
Bora nibakie hivi hivi na niendelee kuchukua tahadhari za corona na sio kudungwa vitu ambavyo hata serikali haitahisika nikidhurika.
Basi mkae kimya don't brainwash wengine kwa misimamo yako binafsi
 
Sawa mkuu.....

Ila......

Ni wapi pale Wataalam wa afya wakashauri kuwa MTU ANAPOKUWA NA VVU(UKIMWI) asitumie tena MIPIRA YA KIUME(condoms) kwa kuwa tu ameshaathirika na ANATUMIA DAWA(ARVs)?!!

Hii ni sawa na KUPATA CHANJO NA kutotumia kinga(barakoa + kunawa maji tiririka + kukaa mbali mtu na mtu).........

#TujitokezeniKuchanjwa
 
Kwani ukimwi wametoa chanjo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…