Uchaguzi 2020 Upotoshaji wa makusudi dhidi ya Tundu Lissu

ulianza vizuri umekuja kuharishia hapa yaani lissu huyuhuyu mpuuzi namba moja aliyekuwa anatetea wazungu wasivunjiwe mikataba waendelee kula madini yetu ndiyo unasema alikuwa anatetea hivyo yaani wewe ni mpumbavu kama huyo lissu yaani umechafua hali yahewa na uzi wako wa kipuuzi hujui na huna hoja ya maana kakojoe ulale
 
Sirini mabeberu hawampendi lisu!
 
Wekaga ushahidi mkuu tuupigie debe!
 
Lissu ni mpinzani sahihi kwa wakati sahihi!
 
Hatutaki mtu mwenye wazo la kuingiza watoto wa watu barabarani wavunjike miguu.

Ni kweli, kuna mgombea mmoja keshafanya tayari. Anawalazimisha walimu na wanafunzi kujipanga barabarani kumpokea.
 
Police wa Tanzania wanaiharibia CCM kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Hakuna mgombea bora wa urais 2020 kama Lissu.
Mwache aendelee kua mgombea bora wa urais, ila kuhusu kua Rais bado sana.
Watanzania bado hatuko tayari kuuza taifa letu kwa Mabeberu kisa kumfurahisha yeye (TL)
 
Naona hufuatilii anachokizungumza T.Lissu.Yeye Mwenyewe Kwa maneno yake kasema hivi..Huu uchaguzi tunaenda kushinda,ikitokea vinginevyo hatutakubali,lazima Tuingie barabarani"

Je hapo kuna upotoshaji??
Au watu wananukuu maneno yake.
 
Naona hufuatilii anachokizungumza T.Lissu.Yeye Mwenyewe Kwa maneno yake kasema hivi..Huu uchaguzi tunaenda kushinda,ikitokea vinginevyo hatutakubali,lazima Tuingie barabarani"

Je hapo kuna upotoshaji??
Au watu wananukuu maneno yake.
huyu ni chizi siyo mzimakama anauhakiaka anashinda anafanya kampeni ya nini
 
Tofauti yako na mimi ni kwamba wewe mwenzangu hoja zako zimejikita kwenye mihemko na matusi wakati mimi ninajenga hoja kwa fact.

Unasema Lissu amekuwa akiwatetea wezi wa madini yetu, hoja hiyo haina ukweli wowote zaidi ya uzushi wenye lengo la kutaka kuchafua taswira ya Lissu.

Kama ni kauli alizozitoa wakati wa sakata la makinikia wote tulizisikia na hakuna mahali popote alipotetea hao wezi zaidi ya kutoa tahadhari kwa namna tunavyotaka kudeal na hao watu.

Sasa kama kwa ufahamu wako mtu kutoa tahari wewe unamchukulia kuwa anatetea wezi basi hapo mimi sina la ziada maana uelewa hua unatofautiana.

Hebu tujiulize baada ya hatua kubwa tulizozichukua katika kukomboa raslimali zetu, je tumenufaika kwa kiasi gani?

Tuna migodi mingi sana mikubwa na midogo na yote inamilikiwa na wageni(mabeberu) je tumefanya jambo gani kubwa tunaloweza kusimama kifua mbele kwamba kwasasa nchi yetu inafaidika sana na raslimali za migodi. Hilo ni moja.

Je kwa kuonyesha kuwa sasa tumeamua kwa dhati kuhakikisha tunapambana na hawa wanyonyaji na vibaraka wao. Watanzania wenzetu ambao walituingiza kwenye unyonywaji huu kwa kusaini hiyo mikataba kwa kutanguliza tamaa zao, je tumewafanya nini? Maana hao watu tunao mpaka leo, au kwakuwa tuko nao kwenye chama basi haina shida.

Au we mwenzetu kwa ufahamu wako Lissu ndiye aliwaleta hao wawekezaji na ndiye aliyeingia nao mikataba?

Hebu jenga hoja ili unishawishi na mimi niungane nawe katika kumlaani Lissu.
 
1. Mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe
2. Lissu ndie tishio la ccm, hata 'shetani' anajua
3. Ukiona giza linakuwa kali basi kunakaribia kucha!
 
lissu ni muhuni yeye kama anajifanya anajua sheria alikuwa anatakiwa aishauri serikali kuwa ifanyeje ili iwaondoe hao mabeberu wasielndelee kuinyonya nchi sasa yeye alikuwa anaitisha serikali na kwakuwa haikumsikiliza ndiyo matokeo yake makubaliano ya kuendesha migodi ikapatikana na pesa kibao tukalipwa tungemsikiliza tusingepata kitu na uoga ungetuingia ndugu acha ushabiki wa kijinga lissu hana lolote anajifanya anajua kila kitu kumbe hakuna kitu hapo
 
Hizi ndiyo propaganda za CCM kila uchaguzi,
Mwaka 1995 na 2000 sikua mtu mzima hivyo sikujua chochote kuhusu kilichoendelea, lakini chaguzi zilizofuata nimeshuhudia na kushiriki, baada ya kuona jinsi watu hawa wanafanya ilinilazimu kutaka kujua ni vipi waliweza kuwafanya watanzania wawe na uoga kiasi hiki. Niliamua kutafuta watu walioshuhudia...
Babu yangu aliniambia kwamba Mwaka 1995 na hata mwaka 2000 watu wa CCM walikua wakienda kijijini kwetu na Sinema kuwaonesha watu Videotapes za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuwaambia kwamba "Mkichagua wapinzani wataleta hiki kilichoeakuta Wanyarwanda"

Hivyo basi nikagundua kuwa tatizo kwetu ni ujinga tu...
Hiki kifanyikacho sasa si kigeni ni maneno tu ndo wamebadilisha.
 
Binafsi nilijua na hawa wapotoshaji nao pia walipaswa wafungiwe kampeni zao kwa kutoa tuhuma zisizo thibitika! Mfano mtu mzima kabisa anasimama jukwaani anasema:-
1. Lissu akichaguliwa ataleta vita, Je alimsikia wapi Lissu kisema ataleta vita? Ana ushahidi gani na hilo wakati Lissu hana hata jeshi la mgambo?
2.Lissu akichaguliwa atauza madini yote nje! Hivi ni wapi Lissu alitamka kuuza madini nje? Alimsikia Lissu akiongea na nani kuwa atamuuzia hayo madini? lakini mbona hata sasa wateja wakuu wa madini yetu ni hayohayp mataifa ya nje??
3.Lissu ni kibara wa mabeberu! Je ni kibaraka vipi au kwa namna gani? Kwani kwenda kutibiwa nje ya nchi kunusuru maisha yake tayari ni kibaraka? Mbona Kikwete alikwenda kutibiwa Uswis, hatukusema ni kibaraka? Mbona Ndugai na Mwakyembe walitibiwa nje muda mrefu sana lakini hatukusema ni vibaraka? Mbona Mkapa(RIP) alikwenda kutibiwa nje hatukusema ni kbaraka wa mabeberu? Hivi ni kweli hawa mabeberu tunaowafahamu kwanguvu zao za kiuchumi na kiulinzi wakiamua kumtumia Lissu kutindua utawala uliopo watashindwa wapi?
Kwa bahati nzuri haya maneno yao yamezoeleka, ni watu wa kutisha na kutia hofu! Mwaka huu wananchi wameamka hawatadanganyika, October 28, kura zote kwa Lissu!
 
Na ni bahati mbaya hatu reveal identities humu. Unawezakuta wewe au wazazi wako ni watumishi wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…