Upotoshwaji unaoendelea kufanywa na baadhi ya Wafamasia kumpotosha Waziri wa Afya

Nimemuelewa kwakweli, pharmacists wasitumie ya kuona Ugonjwa huu huwa wanagaiwa dawa hizi, kujifanya wao ni madaktari wanafanya diagnosis na kupendekeza madawa!

Maumivu yakizidi pata ushauri wa Daktari siyo pata ushauri wa mfamasia!
 
Unampongeza bure!! Hujajua hoja yake ya msingi!! Hoja yake ni kwamba, kwa kuwa yeye ni daktari basi afanye pia kwenye pharmacy kwa kuwa anazijua dawa anazohitaji mgonjwa na hahitaji msaada wa mfamasia. Anataka wafamasia waende viwandani kutengeneza dawa na kufanya tafiti za dawa! Dr KIoboko kimsingi anataka kuunganisha kamba yake kama daktari na ile ya mfamasia!! Hajaridhika kula kutokana na urefu wa kamba yake ya udaktari!! anataka na ile kamba ya ufamasia!! Huu ni uroho! Dr Koboko ningemwelewa kama angekuwa anasisitiza wagonjwa lazima wapate cheti cha daktari kwa baadhi ya dawa kwa mujibu wa sheria. Sasa yeye Koboko anataka mgonjwa hana haja ya kuwa na cheti cha daktari anapoenda pharmacy maana huko pharmacy atamkuta daktari pia!! Sasa hii ni dhana hatari na itavunja sheria, maana daktari akikaa pharmacy ataigeuza pharmacy kuwa dispensary au clinic au hospitali! Dr Koboko ridhika na jukumu la kumtibu mgonjwa kwa maana ya kumchunguza na kumwandikia dawa!! Sehemu iliyobaki kwa mgonjwa waachie taaluma nyingine za afya kama wauguzi na wafamasia!!
Sipingani sana nawe.Napingana kidogo tu kwa hoja hii mfamasia akatengeze dawa,kutuoza na kusambaza kwa mujibu wa taaluma ili kuwe na distribution of work,kama dokta na nesi wanajuwa magonjwa na kumuandikia dawa mgonjwa kwanini wasiruhusiwe kuuza bila cheti cha ADO?Mwisho nisaidiye ni dawa gani ambazo hazitakiwi kutolewa bila cheti cha daktari?
 
Wazee wa copy na kupaste nimeichukua sehemu kama ilivyo....​

What is a pharmacist vs. a doctor?​

Pharmacists commonly work in drugstores and retail environments where they fill prescription medications and address customer needs. Some pharmacists work in hospitals where they support physicians and medical teams in treating patient symptoms and conditions with pharmaceuticals. While pharmacists provide one type of healthcare service, doctors are the medical professionals responsible for diagnosing and treating patients, including writing prescriptions that pharmacists fill for purchase.

Another distinction between pharmacists and doctors is that doctors work directly with their patients, whereas pharmacists work in a laboratory setting and away from patients and customers. However, pharmacists sometimes advise patients and educate customers in retail settings about prescription and over-the-counter medications.
Kumekucha watu wanaoongelea taaluma za watu wakati huna taaluma hiyo muuache.
 
MAJIBU KWA MTU ANAYEJIITA JOSHUA GUYAHAMBI ANAVYOPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA KUHUSU ADDO NA USIMAMIZI WA MADUKA YA DAWA NCHINI

Na Prof Patrick Kobono (MD, MMED, MPH, MBA, PhD in Human Anatomy)

Wasalaam!

Kwa kawaida hua sipendi kabisa kujibishana na wajinga wachache wanaopotosha umma ima kwa makusudi ili kukidhi tamaa na haja zake binafsi au kikundi fulani au ni ujinga unaotokana na yeye kutoelewa kwa sababu huenda hajui chochote au kuna tatizo mahali.

Kwanza amejiita Darasa la saba B, hii inadhihirisha ni jinsi gani alivyo na uelewa finyu kuhuhusu kozi ya famasia na utabibu au Uuguzi pamoja na huduma ya utoaji dawa nchini. Huwezi kua Darasa la saba halafu ukapata Moral authority ya kufanya simple analysis kumjibu profesa na mwalimu wa chuo kikuu. Kama wewe ni darasa la saba B ndio useme darasa la saba wanasomea wapi Famasia. Huu ni ujinga mtupu kutaka kupotosha umma wa watanzania bila kujali kua tunahangaika na afya zao. Unaleta porojo badala ya kuja na Details na majibu sahihi?

UKWELI NI HUU KUHUSU KOZI YA UDAKTARI, FAMASI NA UUGUZI NA NI NANI ANASTAHILI KUTOA DAWA?
Naomba kusema kwamba silengi kutweza taaluma za watu, ninaziheshimu sana lakini propaganda na upotoshaji unapozidi unatakiwa kujibiwa kwa hoja na ukweli kwani mwisho wa siku anayeumia ni mwananchi wa kawaida.

Kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba Famasia chanzo chake ilikua ni sehemu au tawi la kozi Mama ya udaktari baada ya kuona kwamba daktari atakua na kazi nyingi za kutafiti, kutengeza dawa na kutibu, ulitolewa uamuzi baadaye kua masuala ya dawa yajitegemee ndio likaibuka somo la Pharmacology as a branch of Medicine ambaye mwanzilishi wake alikua Mjerumani Oswald Schmiedeberg. Huyu alikua ni daktari wa binadamu na ndiye mwanzilishi wa kwanza wa kozi ya Famasia karne ya 18. Unapokuja na kujitutumua kutaka kupotosha umma wa watanzania na bila kujali unamjibu nani ni utovu wa nidhamu.

Mwanzilishi na mgunduzi wa dawa Duniani Hippocrates, alikua daktari wa binadamu. He was the father of medicine. Ndiye aliyesababisha leo kuwepo na kozi ya Famasia, ndiye aliyekuja kuwazalisha kina Dr Oswald Shmiedeberg. Huwezi kupotosha umma wa watanzania bila kujali kua ushauri wangu ulijikita zaidi katika kuishauri Serikali ispotoshwe na kikundi cha watu wachache wachumia tumbo kwa maslahi yao binafsi bila kujali unyeti wa eneo hili.

ANAYETAKIWA KUTOA DAWA KWA MGONJWA NI NANI?
Ninarudia tena, kuna kitu kinaitwa drugs Administration na dispensing. Hapa ndiko hawa wanaojiita wafamasia wanajichanganya huenda ndio matatizo haya .

Hivi mtu anaposema Mfamasia anafanya drugs Administration ana akili sawa sawa? Katika routes zote za drugs Administration ukitoa oral, ni route gani ambayo wafamaia wanafundishwa darasani na kufanya practises?

Wanafundishwa kutoa sindano kwa I.V au I.M? Mimi ninataka nijue pamoja na kua hizi njia huwezi kutolea kwenye pharmacy. Ukweli ni routes zote zinafanywa na madaktari au manesi.

Miaka 6 mtu anahangaika na magonjwa na dawa leo unasema hana uhalali wa kutoa dawa kwa mgonjwa kweli?

Mfamasia anachoweza kufanya ni ni dispensing kwa maelekezo au maagizo ya daktari. Drugs Administration is not Dispensing! Wafamasia muelewe, hii ndiyo ilikua maana yangu. 👇👇

Dispensing includes all of the steps necessary to translate a medication order (prescription) into an individualized medication supply that is both safe and appropriate.

SWALI: Kama wewe ni Mfamasia upo kwenye duka la dawa, amekuja mgonjwa hana cheti cha daktari utatoaje dawa wakati wewe siyo daktari? Ni nani aliyetufundisha kufanya History taking na kutoa Diagnosisi?

Ni Pharmacy ngapi Tanzania zinauzwa dawa kwa maelekezo ya Prescriptions za madaktari?

Unafikiri ni kwanini dawa kali zote zinatakiwa kuuzwa kwa vyeti vya madaktari na wakati huo huo unasema ili daktari huyo huyo auze dawa lazima awe na ADDO? Hii ni akili ya wapi?

Yaaani Daktari huyu huyu ambaye ndiye mwanzilishi na mwasisi wa kozi ya Famasia unasema awe na ADDO ndio afanye Dispensing?

Kwahiyo narudia maelezo yangu pale pale kwamba serikali kuondoa kozi ya ADDO ilifanya vizuri kuondoa ulaji wa kikundi cha watu wachache lakini ni KOSA KUBWA sana kuwaacha wafanasi wauze na kutoa dawa wao wenyewe, ni kosa la kitaalam. Ni lazima awepo na daktari au nesi ambaye ana utaalam wa kubaini magonjwa kama alivyofundishwa.

NI KOSA KUBWA SANA kusema huyu daktari ambaye ndiye mwasisi na mwanzilishi wa kozi ya famasia eti ili auze dawa kwa mgonjwa ni lazima awe na ADDO au si ruhusa yeye kuuza dawa. Ni kosa gani la kiufundi analoweza kufanya daktari ikiwa atatoa dawa aliyoandika yeye bila uwepo wa Mfamasia kama si ukiritimba na ukuaji wa baadhi ya watu kutaka kujipa uhalali na mamlaka ya kumiliki maduka ya madawa na kutaka kufanya kila kitu nje ya uwezo wao?

Hata viwandani kwenye zile karatasi wanazoweka maelezo mwisho hua wanaandika...as directed by Physician, who is physician? Why not Pharmacist?

NI UVIVU MKUBWA WA KUFIKIRI KUA MFAMASIA ANASOMA ILI BAADAYE CHETI CHAKE KITUMIKE KUSIMSMIA PHARMACY.
Wakati
wenzetu wanasoma Pharmacy ili kwenda kufanya tafiti na kutengeneza dawa mbalibali viwandani, Tanzania kijana anayesoma Pharmacy anawaza amalize ili cheti chake kikazimamie Pharmacy. Huu ni mfumo mbovu wa elimu na ndio unaozalisha hii migongano inayotokea mara ADDO leo usikie imesitishwa.Yote haya ni kwa sababu ya uvivu wa watu kujishughulisha kutaka akae akunje nne aweke cheti chake dukani alipwe milion moja kwa mwezi maisha yaendelee. Tuendelee kuhamasishwa serikali ilete na ivujitie wawekezaji wa viwanda vya kutengeneza dawa ili kelele na njaa hizi ziishe.

HITIMISHO: Mfamasia atengeneze dawa kiwandani, ahifadhi dawa,atoe na kusambaza dawa. Si kazi yake kuchukua history na kubaini ugonjwa kisha atoe dawa. Atoe dawa kwa maelekezo ya daktari kama taratibu zinavyosema, Pharmacies ziuze dawa kwa vyeti vya madaktari. Awepo daktari au nesi katika Pharmacy yeyote ile ili wasaidie kutoa dawa moja kwa moja kwa wagonjwa, huu ndio wajibu wao. Hakuna tatizo lolote nesi au daktari kuuza dawa maana hakuna hoja ya msingi ya kuzuia hili. Hata mahospitali za Wilaya nyingi tu na vituo vya Afya nchini Tanzania Nurse assistants ndio dispensers na hawana mafunzo ya ADDO.

Prof Patrick Kobono (MD, MMED, MPH, MBA, PhD in Human Anatomy)
hoja imejieleza vyema na imeshiba hongera kwako mkuu upo sahihi sana
 
Hata kama ni kweli kuwa watu wengi wakiumwa hupenda kwenda pharmacy, hayo mazoea ni mabaya! Ukweli utabaki kuwa pharmacy si mahali pa kutolea tiba!! Hayo ni makosa makubwa ambayo jamii inapaswa kuelimishwa!! Mahali pa kupata tiba ni hospitalini na mtu sahihi wa kutoa ushauri wa kitabibu ni daktari!! Pharmacy ni mahali pa kotolea dawa!! Japo si kila dawa inahitaji prescription ya daktari! Kama dawa unayotaka haihitaji prescription ya daktari hapo ni sahihi kwenda pharmacy moja kwa moja!! Watu wanataka urahisi, japo kuendekeza urahisi kwenye suala la afya yako kunaweza kukuingiza kwenye gharama kubwa sana!!
Tunawaomba hawa wataalamu wetu wa afya wazingatie maadili ya kazi zao na kutanguliza utu badala ya fedha! Mtu wa pharmacy anakuja mtu dukani kwako nanataka madawa ya moyo tena ya bei mbaya!! lakini hana cheti! usitamani hiyo pesa bali mwelekeze mgonjwa akamwone daktari kwanza!! Na madaktari wana hulka ya kudharau kazi za kada nyingine as if wao peke yao ndio wanaweza kila kitu! hapana!! Vinginevyo tuondoe wauguzi na wafamasia hospitalini wafanye wao peke yao!! Msiendekeze njaa!!
Hili si la Tanzania tu, ni la dunia nzima. Mtu anapoumwa anajua ni kitu kidogo ambacho nitaenda kukifix pharmacy, au nitapata ushauri wa bure. Tena wagonjwa wanatakiwa kuelimishwa Kumuona kwanza community pharmacist, inapunguza na burden kwenye mfumo wa afya. Bahati mbaya labda si rahisi kumkuta pharmacist.

Na pia wafamasia wanaogopa sana dawa, hawezi kuanza kumpa mtu dawa za moyo, kisukari, za akili, baadhi ya antibiotics nk. Hata hizo Erecto wanaogopa kuwapa watu wanajua zinafanya nini kwenye mwili wa mtu. Hata diclofenac wanaziogopa. Mfamasia hawezi toa dawa kama prednisolone kirahisirahisi, lakini utakuta wengi wanatoa kirahisi tu kwa vitu kama miwasho!! Kila mtu afanye alichosomea ili mgonjwa afaidike zaidi.
 
Hii ni kosa kabisa kusema eti Pharmacist hawajui diagnosis [emoji2][emoji2][emoji2]

Shule ya Mfamasia inamtosha kufanya a rational judgement ya magonjwa mengi tuu. Ndiyo maana kuna Pharmacy Only Medicines ambazo Mfamasia anaweza kuzitoa bila ya kuhitaji cheti cha Daktari
Mkuu hapo ndio makosea nyinyi madaktari na wafamasia ...

Daktari anahisi anajua dawa kama mfamasia ...kitu ambacho sio sahihi ...hana elimu kubwa ya dawa kama mfamasia...mfamasia ametumia muda mwingi sana kwenye miaka yake minne 4 ya masomo + internship...na kuendelea.... kujifunza kuhusu dawa ...

Mfamasia anahisi anaweza kumsikiliza mgonjwa na kupata diagnosis...chap kwa haraka ...kitu ambacho sio sahihi nikitu ambacho hakiji siku moja ni unajitaji theory na kupractice mara kwa mara + kunyonywa shule wenyewe wanaita ...ile uweze kuwa compitent...hivyo...Daktari amejikita sana kwenye kufanya clinical judgment ...kwa kufanya history taking + physical examination...investigations zipi aagize zifanyike ....na kuamua management ya mgonjwa...na amefanya hivyo kuanzia MD 3,MD4,MD5 + internship.... na kuendelea ....

Mfamasia anayehisi hiyo theory aliyonayo kuhusu magonjwa ...anaweza itumia bila clinical exposure kama aliyo nayo daktari ...anaweza akakaa OPD au pharmacy ...na kupata diagnosis chap kwa haraka ...hayuko sahihi ..

Vivyo hivyo daktari anaehisi anaweza kukaa pharmacy na ku dispense dawa bila kuwa na knowledge kama ya mfamasia....anakosea sana.

KILA MTU AFANYE KAZI YAKE ....PIA KILA MTU ANAMTEGEMEA MWENZAKE ...[emoji1753]
 
Mimi nimeshangaa huyu jamaa anajiita Koboko...
Eti Pharmacist hajui diagnosis...
Na unaweza kukuta huyu ni Medical officer wa kawaida.. Anataka akae Pharmacy...
Wanaenda huko Wizarani na kuandaa research hewa na kumdanganya waziri mambo mengi tuu kuhusu hii taaluma ya famasi..
Huyo jamaa ni addo aliyechangamka

Na anatumiwa na network tu
 
Hoja yake sio kuingiliana majukumu
Hoja yake ni pale Daktari anapo onekana hawezi kutoa dawa ambazo yeye mwenyewe ndiye ameziandika.

Kutoa dawa akiwa wapi? Hospitali penyewe daktari hatoi dawa, famasi zina taratibu zake kama akitaka basi azifuate.

Hata Jaji hahudumu mahakama za mwanzo.
 
MAJIBU KWA MTU ANAYEJIITA JOSHUA GUYAHAMBI ANAVYOPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA KUHUSU ADDO NA USIMAMIZI WA MADUKA YA DAWA NCHINI

Na Prof Patrick Kobono (MD, MMED, MPH, MBA, PhD in Human Anatomy)

Wasalaam!

Kwa kawaida hua sipendi kabisa kujibishana na wajinga wachache wanaopotosha umma ima kwa makusudi ili kukidhi tamaa na haja zake binafsi au kikundi fulani au ni ujinga unaotokana na yeye kutoelewa kwa sababu huenda hajui chochote au kuna tatizo mahali.

Kwanza amejiita Darasa la saba B, hii inadhihirisha ni jinsi gani alivyo na uelewa finyu kuhuhusu kozi ya famasia na utabibu au Uuguzi pamoja na huduma ya utoaji dawa nchini. Huwezi kua Darasa la saba halafu ukapata Moral authority ya kufanya simple analysis kumjibu profesa na mwalimu wa chuo kikuu. Kama wewe ni darasa la saba B ndio useme darasa la saba wanasomea wapi Famasia. Huu ni ujinga mtupu kutaka kupotosha umma wa watanzania bila kujali kua tunahangaika na afya zao. Unaleta porojo badala ya kuja na Details na majibu sahihi?

UKWELI NI HUU KUHUSU KOZI YA UDAKTARI, FAMASI NA UUGUZI NA NI NANI ANASTAHILI KUTOA DAWA?
Naomba kusema kwamba silengi kutweza taaluma za watu, ninaziheshimu sana lakini propaganda na upotoshaji unapozidi unatakiwa kujibiwa kwa hoja na ukweli kwani mwisho wa siku anayeumia ni mwananchi wa kawaida.

Kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba Famasia chanzo chake ilikua ni sehemu au tawi la kozi Mama ya udaktari baada ya kuona kwamba daktari atakua na kazi nyingi za kutafiti, kutengeza dawa na kutibu, ulitolewa uamuzi baadaye kua masuala ya dawa yajitegemee ndio likaibuka somo la Pharmacology as a branch of Medicine ambaye mwanzilishi wake alikua Mjerumani Oswald Schmiedeberg. Huyu alikua ni daktari wa binadamu na ndiye mwanzilishi wa kwanza wa kozi ya Famasia karne ya 18. Unapokuja na kujitutumua kutaka kupotosha umma wa watanzania na bila kujali unamjibu nani ni utovu wa nidhamu.

Mwanzilishi na mgunduzi wa dawa Duniani Hippocrates, alikua daktari wa binadamu. He was the father of medicine. Ndiye aliyesababisha leo kuwepo na kozi ya Famasia, ndiye aliyekuja kuwazalisha kina Dr Oswald Shmiedeberg. Huwezi kupotosha umma wa watanzania bila kujali kua ushauri wangu ulijikita zaidi katika kuishauri Serikali ispotoshwe na kikundi cha watu wachache wachumia tumbo kwa maslahi yao binafsi bila kujali unyeti wa eneo hili.

ANAYETAKIWA KUTOA DAWA KWA MGONJWA NI NANI?
Ninarudia tena, kuna kitu kinaitwa drugs Administration na dispensing. Hapa ndiko hawa wanaojiita wafamasia wanajichanganya huenda ndio matatizo haya .

Hivi mtu anaposema Mfamasia anafanya drugs Administration ana akili sawa sawa? Katika routes zote za drugs Administration ukitoa oral, ni route gani ambayo wafamaia wanafundishwa darasani na kufanya practises?

Wanafundishwa kutoa sindano kwa I.V au I.M? Mimi ninataka nijue pamoja na kua hizi njia huwezi kutolea kwenye pharmacy. Ukweli ni routes zote zinafanywa na madaktari au manesi.

Miaka 6 mtu anahangaika na magonjwa na dawa leo unasema hana uhalali wa kutoa dawa kwa mgonjwa kweli?

Mfamasia anachoweza kufanya ni ni dispensing kwa maelekezo au maagizo ya daktari. Drugs Administration is not Dispensing! Wafamasia muelewe, hii ndiyo ilikua maana yangu. 👇👇

Dispensing includes all of the steps necessary to translate a medication order (prescription) into an individualized medication supply that is both safe and appropriate.

SWALI: Kama wewe ni Mfamasia upo kwenye duka la dawa, amekuja mgonjwa hana cheti cha daktari utatoaje dawa wakati wewe siyo daktari? Ni nani aliyetufundisha kufanya History taking na kutoa Diagnosisi?

Ni Pharmacy ngapi Tanzania zinauzwa dawa kwa maelekezo ya Prescriptions za madaktari?

Unafikiri ni kwanini dawa kali zote zinatakiwa kuuzwa kwa vyeti vya madaktari na wakati huo huo unasema ili daktari huyo huyo auze dawa lazima awe na ADDO? Hii ni akili ya wapi?

Yaaani Daktari huyu huyu ambaye ndiye mwanzilishi na mwasisi wa kozi ya Famasia unasema awe na ADDO ndio afanye Dispensing?

Kwahiyo narudia maelezo yangu pale pale kwamba serikali kuondoa kozi ya ADDO ilifanya vizuri kuondoa ulaji wa kikundi cha watu wachache lakini ni KOSA KUBWA sana kuwaacha wafanasi wauze na kutoa dawa wao wenyewe, ni kosa la kitaalam. Ni lazima awepo na daktari au nesi ambaye ana utaalam wa kubaini magonjwa kama alivyofundishwa.

NI KOSA KUBWA SANA kusema huyu daktari ambaye ndiye mwasisi na mwanzilishi wa kozi ya famasia eti ili auze dawa kwa mgonjwa ni lazima awe na ADDO au si ruhusa yeye kuuza dawa. Ni kosa gani la kiufundi analoweza kufanya daktari ikiwa atatoa dawa aliyoandika yeye bila uwepo wa Mfamasia kama si ukiritimba na ukuaji wa baadhi ya watu kutaka kujipa uhalali na mamlaka ya kumiliki maduka ya madawa na kutaka kufanya kila kitu nje ya uwezo wao?

Hata viwandani kwenye zile karatasi wanazoweka maelezo mwisho hua wanaandika...as directed by Physician, who is physician? Why not Pharmacist?

NI UVIVU MKUBWA WA KUFIKIRI KUA MFAMASIA ANASOMA ILI BAADAYE CHETI CHAKE KITUMIKE KUSIMSMIA PHARMACY.
Wakati
wenzetu wanasoma Pharmacy ili kwenda kufanya tafiti na kutengeneza dawa mbalibali viwandani, Tanzania kijana anayesoma Pharmacy anawaza amalize ili cheti chake kikazimamie Pharmacy. Huu ni mfumo mbovu wa elimu na ndio unaozalisha hii migongano inayotokea mara ADDO leo usikie imesitishwa.Yote haya ni kwa sababu ya uvivu wa watu kujishughulisha kutaka akae akunje nne aweke cheti chake dukani alipwe milion moja kwa mwezi maisha yaendelee. Tuendelee kuhamasishwa serikali ilete na ivujitie wawekezaji wa viwanda vya kutengeneza dawa ili kelele na njaa hizi ziishe.

HITIMISHO: Mfamasia atengeneze dawa kiwandani, ahifadhi dawa,atoe na kusambaza dawa. Si kazi yake kuchukua history na kubaini ugonjwa kisha atoe dawa. Atoe dawa kwa maelekezo ya daktari kama taratibu zinavyosema, Pharmacies ziuze dawa kwa vyeti vya madaktari. Awepo daktari au nesi katika Pharmacy yeyote ile ili wasaidie kutoa dawa moja kwa moja kwa wagonjwa, huu ndio wajibu wao. Hakuna tatizo lolote nesi au daktari kuuza dawa maana hakuna hoja ya msingi ya kuzuia hili. Hata mahospitali za Wilaya nyingi tu na vituo vya Afya nchini Tanzania Nurse assistants ndio dispensers na hawana mafunzo ya ADDO.

Prof Patrick Kobono (MD, MMED, MPH, MBA, PhD in Human Anatomy)
Crap!
 
Naunga mkono hoja,

Yaan hapa nchini wataalamu wote wanependa kujimilikisha majukum kwa ajil ya ulaji, Japo wafasia wamezidi

Hata MD na Co kuna majukum mmekua mkiyaingilia na SI kaz zenu kisheria,, MD wamekua wakijimilikisha kila kitu Cha afya wao ndio wahusika waku,

Tafadhal naomb wataalamu tukae chini tugawe migawanyo ya KAZI kwa kila kada ya afya, kwani nishakuta MD na CO wanapima wagonjwa vipimo yinavyopaswa kupimwa na Lab technician, Baraza la madaktari msijimilikishe kila kitu vingine hamvijuii,

MD Mnanga'nga'ana na mashirika na mnaunganishana humo so msilalamike mfamasia nae akiingilia kaz amboyo si yake mana kila mtanzania hata awe msomi vp anachoangalia yeye ni pesa inaingia,

Mwsho niseme kila mmoja ajue majukum yake Ili kuifikisha sectar ya afya mbali na ikubalike kijamii
Njaaa mbaya
 
MAKUNDI YA DAWA ZA BINADAMU 👇👇

1. Prescription Only Medicines ..(Cheti cha daktari kinahitajika )..hizo zenye "Dose;As directed by Physician".
2. Pharmacy Only Medicines(Cheti cha daktari hakihitajiki).
3. General Sale Medicines(Cheti cha daktari hakihitajiki)..hizi utazikuta hata dukani kwa mangi/mpemba n.k. mfano DAWA TATU/ACTION/HEDEX/PANADOL & PANADOL EXTRA/GLUCOSE /COFTA/TUMBOCID/ MOSQUITO (spray and repperants),CASTROL OIL/GLYCERINE/MEDICATED SOAPS /TOOTH PASTE n.k.
Fafanua iyo no 2 hacha ulagai , nyie ndo mtatakiwa fungwa maisha,
Dawa ya matumizi ya binadam lazima ipite KWa dactari ,famasia ni nani ?
 
Nafikiri wewe ndiye huna akili kabisaaa.yani mfalmacia atoe dawa kwa mgonjwa? How? Amesomea wapi anatomy? My dear friend ,dawa siyo maharage aisee!! lini mfamacia amesomea ABCD ? Yani airway, breathing, circulation and drug! Unaweza kutoa dawa kwa mgonjwa akakuzimikia !sasa unajua utamsaidiaje? Nurse na dakatari wanajua namna ya kumsaidia mgonjwa after any side effect from the admistered drug!! Addo na mfamacia wanavijulia wapi? Kitu ambacho daktari hawezi ni kutengeneza dawa na siyo kutoa dawa!! Full stop.so daktari haitaji kusoma Ado au au full pharmacy. Madakatari na manesi wanasoma pharmacology
Endelea na discussion ila kwenye ABCD pharmacist wamesoma pia
 
Wazee wa copy na kupaste nimeichukua sehemu kama ilivyo....​

What is a pharmacist vs. a doctor?​

Pharmacists commonly work in drugstores and retail environments where they fill prescription medications and address customer needs. Some pharmacists work in hospitals where they support physicians and medical teams in treating patient symptoms and conditions with pharmaceuticals. While pharmacists provide one type of healthcare service, doctors are the medical professionals responsible for diagnosing and treating patients, including writing prescriptions that pharmacists fill for purchase.

Another distinction between pharmacists and doctors is that doctors work directly with their patients, whereas pharmacists work in a laboratory setting and away from patients and customers. However, pharmacists sometimes advise patients and educate customers in retail settings about prescription and over-the-counter medications.
Ndio ndio
 
Back
Top Bottom