Upumbavu ni hali ya kutotumia fikra vizuri na kufanya maamuzi mabaya. Je, Rais kuwaeleze ukweli watendaji wake ni wapumbavu anakosea?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Kabla ya kuanza kumhukumu mtu ni lazima kwanza mtu uwe unajihakikishia je huyu mtu amefanya kosa kweli? Na kama amefanya kosa kweli ndio unapaswa kutoa hukumu yako.

Akiwa hajafurahishwa na utendaji wa Wahandisi wasomi na tena viongozi wa vitengo muhimu Rais JPM alitumia neno upumbavu kuonyesha kuwa hawa watumishi ambao ni wasomi hawakuwa na awareness na hawakutumia weledi wao ili kutatua tatizo ambalo kwa kutumia good sense and good judgement lingeweza kutatuliwa kwa muda mfupi.

Kumeibuka mijadala sehemu mbalimbali kuwa kwa kutumia neno upumbavu eti aliwatukana na kuwadhalilisha.Je neno upambavu ni tusi? Maana ni kukosa kufikiria vyema na kuwa na maamuzi mabaya.

Hawa wasomi walishindwa vipi kutumia taaluma yao na kuona ile sehemu fupi yenye gema ambalo lingeweza kutengeneza diversion fupi na ya kudumu. Lack of good sense which leads to mistake(Foolishness) ni tusi?

Kwa maoni yangu Rais hajawatukana ila amewakumbusha kutumia akili katika kutatua matatizo. Na hili ni tatizo kubwa maana watendaji wengi wa serikali hawatumii akili ili kutatua kero za wananchi.
 
Yeye tunaposema amekosea watu wanakamatwa na kupewa kesi za uchochezi why?

ukimuita mtu mpumbavu kwa kukosea usisahau wewe ukikosea utaitwa mpumbavu pia.

Tetemeko kagera, Sakata la Sukari Makinikia, Korosho, Mbaazi ni moja ya vitu vilivyo onyesha upumbavu wa mtu fulani.
 
Hata yeye pia kuna maeneo mengi tu amefanya maamuzi ya kipumbavu so na yeye ni MPUMBAVU vilevile..
Mfano kubambikia watu kesi..mfano mwingine inakuwaje maabara ya kupima corona inakuwa moja tu nchi nzima..MPUMBAVU kabisa.
Hayo yako binafsi.
 
kwa hiyo unakubali pia kuwa wananchi (ambao ni mabosi wa rais) wapo sahihi kumuita rais ni "mpumbavu" katika masuala ya korosho, makinikia, sukari, kuporomoka kwa traditional exports, nk, nk.....right?
Kuna watu wa chini yake walifanya upumbavu...ushahidi unao
 
Vipi watu wengine wakimkumbusha pia kwa kutumia neno hilohilo mfano kwenye maamuzi yake kuhusu korosho msimu uliopita.

Mtu unaweza kueleweka vizuri tu pasipokutumia maneno ya kukera kama hayo.
 
Hata wewe umeogopa. Upumbavu wa mtu "fulani". Mtaje tumjue
 
Jiwe naye tukiona kakosea tumuite mpumbavu?Mfano kujenga uwanja wa kimataifa Chato ni upumbavu!
Ule uwanja unahudumia geita nzima wala sio chato tu. Na tena geina na mikoa jirani kama kagera. Geita nzima walikuwa wanategemea airstrip ya Ggm
 
M
Vipi watu wengine wakimkumbusha pia kwa kutumia neno hilohilo mfano kwenye maamuzi yake kuhusu korosho msimu uliopita.

Mtu unaweza kueleweka vizuri tu pasipokutumia maneno ya kukera kama hayo.
Maamuzi yapi kwenye korosho?
 
huu uzi unaonyesha wazi wazi kiwango Upumbavu uliopo
 
Upumbavu zaidi ni pale unapoteua watu wapumbavu huku ukijua nkuwa ni wapumbavu ili kukusaidia kuteleleza majukumu yako.
 
.... ukitaka kujua ni tusi au sio tusi muite yeye mpumbavu! Utapotea mazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…