Upuuzi wa Kocha Pablo wa Simba SC unavyozidi kuisafishia Yanga SC njia ya kuwa Mabingwa wa NBC Premier League kwa 75% mpaka sasa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Yaani Kocha kabisa umeshapoteza Mechi Mbeya halafu Mechi muhimu ya leo Morogoro unakuja Kumjaribu Beki Mbovu Gadiel Michael wakati Mchezaji mahiri Mohammed Hussein Tshabalala unae na hujataka Kumuanzisha?

Yaani Kocha kabisa una Wachezaji very talented and creative kama Chama na Morrison unaacha Kuwaanzisha unawaingiza baadae kabisa?

Yaani kabisa Kocha Sisi Watu wa Mpira tumeshaona kuwa John Boko tayari 'Kwishnei' Kisoka halafu Wewe unamtetea huku ukiendelea Kumpanga Kikosini wakati una Vijana au Wachezaji wengine very Competent wa Kuisadia Timu?

Tayari Kocha uko na Kikosi na umeshaona ukitoa tu Meddie Kagere huna tena Mshambuliaji mwingine unaacha kuuambia Uongozi uachane na Chris Mugalu ili haraka tusajili 'Striker' mpya unabaki kudemadema tu utafikiri Ligi Kuu ya NBC ni ya Babu zako uliowaacha huko Kijijini Kwanu Hispania?

UKWELI MCHUNGU

GENTAMYCINE mpaka sasa nawapa 75% Yanga SC kuwa Mabingwa labda tu 'Complacency' iwagharimu na wasipouchukua Ubingwa nitawadharau kuliko Maelezo kwani Kiuhalisia na Kimazingira wana dalili zote za kuwa Mabingwa.

KWENU WANA SIMBA SC WENZANGU

Ili Yanga SC isiwe Bingwa inatakiwa ama ifungwe Mechi 3 au itoke Sare Mechi 4 je, tukiacha Unafiki na Ushabiki wetu mnadhani kwa Yanga SC hii ya sasa na walivyojipanga Kimkakati ndani na nje ya Uwanja hili litawezekana?

Na kumbukeni wakati huo tunaiombea mabaya haya Yanga SC na Sisi Simba SC tunatakiwa Kushinda tu Mechi zetu zote zilizobaki je, kwa Upuuzi na Ubovu wa Kocha Pablo mnadhani Simba SC yetu hii itaweza kulifanya hili wakati tuna Wachezaji dhaifu na wasio na Uchungu na Simba SC yetu?

LAWAMA KWA VIONGOZI WA SIMBA SC

Uongozi wa Simba SC wa sasa hauko serious na umewekeza zaidi katika Mapato na Biashara lakini siyo Ushindani wa Simba SC Uwanjani.

Wenzetu ( Watani ) zetu wanasajili Majembe ili Kujiimarisha zaidi Kiushindani Sisi kutwa tunahimizwa tu Kuchangia Ujenzi wa Uwanja wetu ili Ujengwe haraka kana kwamba TFF wametufukuza katika Viwanja vilivyopo.

NANI KASEMA HAJI MANARA KWENDA YANGA SC HAKUNA MADHARA YOYOTE KWA SIMBA SC YETU?

Tena Kuondoka kwa Haji Manara Kumetuathiri pakubwa Simba SC kwani alichokifanya Manara ni kuwaambia wana Yanga SC ( Viongozi na Wadhamini ) Siri zote zilizoipa Ubingwa mara Nne ( 4 ) na Yanga SC sasa nao kupitia GSM na Pesa walizonazo wanapita mule mule alikokuwa akipita Simba SC ( hasa Tajiri Mo Dewji ) na kwa Kujidhatiti Kwao kubakia Kileleni mpaka Watangazwe Mabingwa.

MIUJIZA

Najua duniani kuna Maajabu ( Miujiza ) ya kwamba pamoja na Yanga SC kutamba hivi ila nao wanaweza Kuukosa Ubingwa huu na Simba SC akauchukua tena.

Kwa Uchezaji mbovu wa Simba SC wa sasa na Umakini wa Yanga SC ni Mwendawazimu tu pekee atakataa kuwa hadi sasa ( leo ) Yanga SC ana 75% za kuwa Mabingwa.

LAWAMA NA VISINGIZIO VYA KIPUMBAVU

Kuna Watu wanadai Simba SC inaonewa na kwamba Yanga SC wanapendelewa.

GENTAMYCINE nakataa isipokuwa ninachojua tu ni kwamba Yanga SC imesajili Wachezaji wa Matokeo na Simba SC tumesajili Wachezaji wa Maonyesho na 10% kwa baadhi ya Viongozi wa Simba SC.

Upuuzi mwingine ni huu baada ya Kufungwa na Mbeya City na Leo kutoa Suluhu na Mtibwa Sugar FC baadhi ya wana Simba SC wanadai Viwanja vilikuwa Kikwazo.

Nami nauliza kama Viwanja vya Sokoine ( Mbeya ) na Manungu ( Morogoro ) ni Vibovu na Kikwazo Kwetu Klabu yetu ya Simba SC imejenga wapi Uwanja wake?

Na kama Viwanja vilikuwa ni Vibovu vya Mbeya na Morogoro imekuwaje Wapinzani wetu wenye Miguu na Nguvu sawa na Sisi wao wameweza Kuvicheza na wala hawalalamiki au Kudeka kama Sisi?

NINI KIFANYIKE KWA SASA?

Tuache Kuiwazia Yanga SC 24/7 na Kucheza Mechi zao Kifitna ili Wafungwe au Watoke Sare tuweze Kuwakaribia bali tujitathmini wapi tumekosea kwa Msimu huu, tujisahahiihishe na tucheze Mechi zetu Kimkakati na tusiruhusu tena Kufungwa au hata kutoka Sare Mechi nyinginezo kuanzia sasa.

HITIMISHO

Wana Simba SC tukubali tu kuwa Kutesa ni kwa zamu na Watani zetu Yanga SC kwa Msimu huu wapo vyema na walijipanga vvema Kimkakati ( hasa Ndani na Nje ) ya Uwanja.

Viongozi wa Simba SC amkeni haraka!!

Cc: Daudi Mchambuzi
 
ukweli mchungu kama huu ndo unaweza kutuvusha na sio kudanganyana eti vyura wanabebwa, ukiitazama league tangu ianze kiuanamichezo utagundua simba tumebebwa mechi nyingi na uto wamebebwa mechi 1 tu ile ya namungo.

kama kweli viongozi na wapenzi wa simba tunataka kurejea ktk makali yetu ni lazima kuufanyia kazi ukweli mchungu ulioletwa na mtoa mada kwenye chapisho hili.

NB:ubingwa bado hauna mwenyewe ikiwa tutasolve matatizo yetu haraka.
 
Nakubaliana na mtoa mada moja kwa moja. Simba wanawaonea aibu wachezaji waliozeeka kama boko badala ya kuwaacha na kusajili vijana.

Pia nauona mapungufu ya uongozi. Inakuwaje simba ilishapiga hatua mbele kwa hiyo msimu huu walitakiw kusajili wachezaji hasa washambuliani wa class za juu kuliko tulionao lakin viongozi wakazembea.

Dirisha dogo pia wamezembea. Kuna wachezaji waliosajiliwa msimu huu ukiwatazama ni wazi unaziona ten percent. Kiweli kusua sua kwa simba ni matokeo ya maamuzi yao.

Pia kuna haja gani ya zile bilion 20 kama tunaendelea tunaendelea na usajili usio na malengo
 
Upuuzi mwingine ni huu baada ya Kufungwa na Mbeya City na Leo kutoa Suluhu na Mtibwa Sugar FC baadhi ya wana Simba SC wanadai Viwanja vilikuwa Kikwazo.

Nami nauliza kama Viwanja vya Sokoine ( Mbeya ) na Manungu ( Morogoro ) ni Vibovu na Kikwazo Kwetu Klabu yetu ya Simba SC imejenga wapi Uwanja wake?

Na kama Viwanja vilikuwa ni Vibovu vya Mbeya na Morogoro imekuwaje Wapinzani wetu wenye Miguu na Nguvu sawa na Sisi wao wameweza Kuvicheza na wala hawalalamiki au Kudeka kama Sisi?

Cc: Daudi Mchambuzi

Ila kiukweli kabisa uwanja wa Manungu una pitch nzuri sana kuliko hata uwanja wa jamuhuri Morogoro, sema mvua tu ndio ulioharibu pitch. Uwanja wa jamuhuri vipara kibao na pia kuna mabonde mabonde mengi.

Ruvu shooting wamechezea uwanja wa Sokoine huo huo na ulikuwa umeharibika na mvua lakini hawakulalamika. Scars
 
Yaani Kocha kabisa umeshapoteza Mechi Mbeya halafu Mechi muhimu ya leo Morogoro unakuja Kumjaribu Beki Mbovu Gadiel Michael wakati Mchezaji mahiri Mohammed Hussein Tshabalala unae na hujataka Kumuanzisha?

Yaani Kocha kabisa una Wachezaji very talented and creative kama Chama na Morrison unaacha Kuwaanzisha unawaingiza baadae kabisa?

Yaani kabisa Kocha Sisi Watu wa Mpira tumeshaona kuwa John Boko tayari 'Kwishnei' Kisoka halafu Wewe unamtetea huku ukiendelea Kumpanga Kikosini wakati una Vijana au Wachezaji wengine very Competent wa Kuisadia Timu?

Tayari Kocha uko na Kikosi na umeshaona ukitoa tu Meddie Kagere huna tena Mshambuliaji mwingine unaacha kuuambia Uongozi uachane na Chris Mugalu ili haraka tusajili 'Striker' mpya unabaki kudemadema tu utafikiri Ligi Kuu ya NBC ni ya Babu zako uliowaacha huko Kijijini Kwanu Hispania?

UKWELI MCHUNGU

GENTAMYCINE mpaka sasa nawapa 75% Yanga SC kuwa Mabingwa labda tu 'Complacency' iwagharimu na wasipouchukua Ubingwa nitawadharau kuliko Maelezo kwani Kiuhalisia na Kimazingira wana dalili zote za kuwa Mabingwa.

KWENU WANA SIMBA SC WENZANGU

Ili Yanga SC isiwe Bingwa inatakiwa ama ifungwe Mechi 3 au itoke Sare Mechi 4 je, tukiacha Unafiki na Ushabiki wetu mnadhani kwa Yanga SC hii ya sasa na walivyojipanga Kimkakati ndani na nje ya Uwanja hili litawezekana?

Na kumbukeni wakati huo tunaiombea mabaya haya Yanga SC na Sisi Simba SC tunatakiwa Kushinda tu Mechi zetu zote zilizobaki je, kwa Upuuzi na Ubovu wa Kocha Pablo mnadhani Simba SC yetu hii itaweza kulifanya hili wakati tuna Wachezaji dhaifu na wasio na Uchungu na Simba SC yetu?

LAWAMA KWA VIONGOZI WA SIMBA SC

Uongozi wa Simba SC wa sasa hauko serious na umewekeza zaidi katika Mapato na Biashara lakini siyo Ushindani wa Simba SC Uwanjani.

Wenzetu ( Watani ) zetu wanasajili Majembe ili Kujiimarisha zaidi Kiushindani Sisi kutwa tunahimizwa tu Kuchangia Ujenzi wa Uwanja wetu ili Ujengwe haraka kana kwamba TFF wametufukuza katika Viwanja vilivyopo.

NANI KASEMA HAJI MANARA KWENDA YANGA SC HAKUNA MADHARA YOYOTE KWA SIMBA SC YETU?

Tena Kuondoka kwa Haji Manara Kumetuathiri pakubwa Simba SC kwani alichokifanya Manara ni kuwaambia wana Yanga SC ( Viongozi na Wadhamini ) Siri zote zilizoipa Ubingwa mara Nne ( 4 ) na Yanga SC sasa nao kupitia GSM na Pesa walizonazo wanapita mule mule alikokuwa akipita Simba SC ( hasa Tajiri Mo Dewji ) na kwa Kujidhatiti Kwao kubakia Kileleni mpaka Watangazwe Mabingwa.

MIUJIZA

Najua duniani kuna Maajabu ( Miujiza ) ya kwamba pamoja na Yanga SC kutamba hivi ila nao wanaweza Kuukosa Ubingwa huu na Simba SC akauchukua tena.

Kwa Uchezaji mbovu wa Simba SC wa sasa na Umakini wa Yanga SC ni Mwendawazimu tu pekee atakataa kuwa hadi sasa ( leo ) Yanga SC ana 75% za kuwa Mabingwa.

LAWAMA NA VISINGIZIO VYA KIPUMBAVU

Kuna Watu wanadai Simba SC inaonewa na kwamba Yanga SC wanapendelewa.

GENTAMYCINE nakataa isipokuwa ninachojua tu ni kwamba Yanga SC imesajili Wachezaji wa Matokeo na Simba SC tumesajili Wachezaji wa Maonyesho na 10% kwa baadhi ya Viongozi wa Simba SC.

Upuuzi mwingine ni huu baada ya Kufungwa na Mbeya City na Leo kutoa Suluhu na Mtibwa Sugar FC baadhi ya wana Simba SC wanadai Viwanja vilikuwa Kikwazo.

Nami nauliza kama Viwanja vya Sokoine ( Mbeya ) na Manungu ( Morogoro ) ni Vibovu na Kikwazo Kwetu Klabu yetu ya Simba SC imejenga wapi Uwanja wake?

Na kama Viwanja vilikuwa ni Vibovu vya Mbeya na Morogoro imekuwaje Wapinzani wetu wenye Miguu na Nguvu sawa na Sisi wao wameweza Kuvicheza na wala hawalalamiki au Kudeka kama Sisi?

NINI KIFANYIKE KWA SASA?

Tuache Kuiwazia Yanga SC 24/7 na Kucheza Mechi zao Kifitna ili Wafungwe au Watoke Sare tuweze Kuwakaribia bali tujitathmini wapi tumekosea kwa Msimu huu, tujisahahiihishe na tucheze Mechi zetu Kimkakati na tusiruhusu tena Kufungwa au hata kutoka Sare Mechi nyinginezo kuanzia sasa.

HITIMISHO

Wana Simba SC tukubali tu kuwa Kutesa ni kwa zamu na Watani zetu Yanga SC kwa Msimu huu wapo vyema na walijipanga vvema Kimkakati ( hasa Ndani na Nje ) ya Uwanja.

Viongozi wa Simba SC amkeni haraka!!

Cc: Daudi Mchambuzi
Kuna kipindi huwa zinakurudia.
 
Unajua wabongo tupunguze ujuaji,,hivi katika football timu gani haifungwi??
Au nyie mlitaka kila mwaka simba achukue ubingwa itakuwa bado ni ligi au ibadilishwe iitwe Simba premier league [emoji848][emoji848]
Uwezo wako wa Akili na wa Kubishana nami katika ( Kuhusu ) Soka la Tanzania ( Bongo ) ni mdogo sana hivyo acha Kunipotezea muda tafuta wa 'level' yako tafadhali sawa?
 
Back
Top Bottom