Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,457
Baada ya kuwa mywaji wa BIA kwa takribani miongo minne huwa najiuliza ni kwanini mtu anakukuta baa - hujamwalika wala hajakualika mnasalimia anakaa meza yake na baada ya muda anakuagizia kinywaji - "waiter/dada mpatie yule jamaa bia moja"! Huu utaratibu ni urafiki wa kweli au ni upumbavu au ni ishara ya nini?
Sijawahi kupata jibu - Naomba kuuliza!!!
Ni ishara ya ukarimu, kwa sababu sio watu wote wanaowanunulia wengine bia. Kuna wengine nati sana kutoa pesa yao, utawakuta wamekaa pekee yao, na akishapata moja mbili anaondoka hataki kukaa muda mrefu.
Na sie wa soda na vijoti tunaruhusiwa kuchangia pia!??
mentor, hivi vijoti vinapatikana bar? wa soda nadhani wanaruhusiwa, ngoja BE arudi
@Nyambala:
Kwahiyo kununuliana bia ni dalili ya "kuwekeza"?
Scenario ninayoongelea iko hivi:
Mimi nimekwenda kumtembelea rafiki yangu Kunduchi Mtongani, baada ya kuagana naye napitia MALANJA "Executive?" INN kusudi kujiweka sawa kwa safari yangu ya kurudi Gongo La Mboto. Nipo kaunta nimesimama, naagiza bia yangu ya kwanza, mara anakuja "rafiki wa zamani" tunasalimiana, anakwenda kuketi. Dakika tatu baadaye "waiter" ananiletea bia na kuniambia "imetoka kwa yule baba"! Dakika kumi baadaye "offer" nyingine, dakika 30 baadaye "offer" ya tatu!
Sasa huo ndiyo "ukarimu" au "ulimbukeni"? Unawezaje kutengeneza marafiki kwa njia hiyo ya "bandika bandua" kwa mtu ambaye hamjaonana for "ages"?
Hahahaha!!! Muruke yule mupe yule ahaaa yule anakunywa soda muruke mupe yule anakunywa Serengeti muruke yule anakunywa maji mupe yule anakunywa Kilimanjaro.
Baba Enock kwani wewe hutaki kununuliwa bia??