Urafiki au Upumbavu au ? : Kununuliana BIA kwenye sehemu za Starehe!

Urafiki au Upumbavu au ? : Kununuliana BIA kwenye sehemu za Starehe!

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
7,076
Reaction score
2,457
Baada ya kuwa mywaji wa BIA kwa takribani miongo minne huwa najiuliza ni kwanini mtu anakukuta baa - hujamwalika wala hajakualika mnasalimia anakaa meza yake na baada ya muda anakuagizia kinywaji - "waiter/dada mpatie yule jamaa bia moja"! Huu utaratibu ni urafiki wa kweli au ni upumbavu au ni ishara ya nini?

Sijawahi kupata jibu - Naomba kuuliza!!!
 
Pombe zinaleta urafiki kwa haraka sana! Mimi nimepata marafiki wengi sana kupitia bar! Nimepata deals nyingi sana kupitia kwa marafiki wapya naokutana nao bar! Ukitaka kupata potential informations kutoka kwa mtu ambaye unaona una upotential fulani, wewe mnunulie bia!!
Bia is everything meen!!
 
ndo maana watu waroho utasikia tu huyu jamaa mtu safi sana yaani anaisaidia mambo mengi tu ili kesho na wewe ujeumnunulie kwani tumeumbwa na uso wahaya..
 
Hahahaha!!! Muruke yule mupe yule ahaaa yule anakunywa soda muruke mupe yule anakunywa Serengeti muruke yule anakunywa maji mupe yule anakunywa Kilimanjaro.
 
Yaani miongo yote hiyo bado kujifunza kitu? Fanya praktiko leo jioni, fanya observation afu useme umejifunza nini
 
Ni ishara ya ukarimu, kwa sababu sio watu wote wanaowanunulia wengine bia. Kuna wengine nati sana kutoa pesa yao, utawakuta wamekaa pekee yao, na akishapata moja mbili anaondoka hataki kukaa muda mrefu.
 
BE, unajua huwa najitahidi kuepuka ''holier than thou attitude''. hata wanawake tuna hizi tabia. tunajikuta tunakutana in our regular saloon especially, halafu siku mnakutana mbali kwenye kazi. yaani mnakuwa kama ndugu wenyeji wenu wanadhani mkiwa nyumbani huwa mnatafutana. toka nilipogundua hiyo silaumu tena juu ya urafiki wa bar

Baada ya kuwa mywaji wa BIA kwa takribani miongo minne huwa najiuliza ni kwanini mtu anakukuta baa - hujamwalika wala hajakualika mnasalimia anakaa meza yake na baada ya muda anakuagizia kinywaji - "waiter/dada mpatie yule jamaa bia moja"! Huu utaratibu ni urafiki wa kweli au ni upumbavu au ni ishara ya nini?

Sijawahi kupata jibu - Naomba kuuliza!!!
 
Ni ishara ya ukarimu, kwa sababu sio watu wote wanaowanunulia wengine bia. Kuna wengine nati sana kutoa pesa yao, utawakuta wamekaa pekee yao, na akishapata moja mbili anaondoka hataki kukaa muda mrefu.

Mkuu nakubaliana na wewe though sometimes this is an "old" and "rural" truth. Ukarimu wa kweli siku zote huwa ni unconditional lakini nimeshaona kuna watu huwa mpaka wanafeel guilty anapokuwa hana uwezo wa kumnunulia mtu mwingine hiyo bia. In short the practice should be done leisurely lakini uswahilini huwa inakuwa kama unwritten formula nilikununulia juzi na wewe ninunulie leo. Au kama wewe una unafuu wa maisha basi lazima uninunulie mimi, si unajua mimi KKK.

Kwa maoni yangu it's more of an appreciation say ya kufahamiana, kufanya kazi flani pamoja au kukumbwa na tatizo flani pamoja. It is good and easy when it is reciprocal though kibongobongo sometimes huwa sivyo hivyo. Kuna watu wengine huwa wanaona fahari akikununulia yeye tu au wengine anaona the'y are entitled kununuliwa tu.
 
Yaani hiyo ndo raha ya bia na raha ya kunywea bar ni ktk kuonyesha undugu,urafiki,kujali...Nakumbuka kuna rafiki zangu walikuwa wakizinguana hadi kuchuniana ukitaka kuwapatanisha fanya mpango uwakutanishe bar, wakitoka hapo 'bifu' limeisha.....ONE FOR THE ROAD PLEASE!
 
@Nyambala:

Kwahiyo kununuliana bia ni dalili ya "kuwekeza"?

Scenario ninayoongelea iko hivi:

Mimi nimekwenda kumtembelea rafiki yangu Kunduchi Mtongani, baada ya kuagana naye napitia MALANJA "Executive?" INN kusudi kujiweka sawa kwa safari yangu ya kurudi Gongo La Mboto. Nipo kaunta nimesimama, naagiza bia yangu ya kwanza, mara anakuja "rafiki wa zamani" tunasalimiana, anakwenda kuketi. Dakika tatu baadaye "waiter" ananiletea bia na kuniambia "imetoka kwa yule baba"! Dakika kumi baadaye "offer" nyingine, dakika 30 baadaye "offer" ya tatu!

Sasa huo ndiyo "ukarimu" au "ulimbukeni"? Unawezaje kutengeneza marafiki kwa njia hiyo ya "bandika bandua" kwa mtu ambaye hamjaonana for "ages"?
 
Umenena,kwangu mimi huu ni urafiki wa mashaka mara chache sana huwa nahesabu chochote kwenye urafiki wa pombe ngoja siku utangaze njaa wengi/kama sio wote huwa wanakukimbia.

@Nyambala:

Kwahiyo kununuliana bia ni dalili ya "kuwekeza"?

Scenario ninayoongelea iko hivi:

Mimi nimekwenda kumtembelea rafiki yangu Kunduchi Mtongani, baada ya kuagana naye napitia MALANJA "Executive?" INN kusudi kujiweka sawa kwa safari yangu ya kurudi Gongo La Mboto. Nipo kaunta nimesimama, naagiza bia yangu ya kwanza, mara anakuja "rafiki wa zamani" tunasalimiana, anakwenda kuketi. Dakika tatu baadaye "waiter" ananiletea bia na kuniambia "imetoka kwa yule baba"! Dakika kumi baadaye "offer" nyingine, dakika 30 baadaye "offer" ya tatu!

Sasa huo ndiyo "ukarimu" au "ulimbukeni"? Unawezaje kutengeneza marafiki kwa njia hiyo ya "bandika bandua" kwa mtu ambaye hamjaonana for "ages"?
 
Hahaaaaaaaaa umenikumbusha mbali sana mupe muruke.

Hahahaha!!! Muruke yule mupe yule ahaaa yule anakunywa soda muruke mupe yule anakunywa Serengeti muruke yule anakunywa maji mupe yule anakunywa Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom