Kumekuwa na maneno na hofu kutoka kwa baadhi ya Watanzania hasa baada ya Raisi Samia kufanya juhudi za kuurejesha tena uhusiano na Kenya ambao ulidhoofika sana awamu ya Tano.
Awamu ya Tano iliona Ni muhimu zaidi kuikumbatia Rwanda ya Kagame kuliko Kenya. Ikafikia wanyarwanda hadi wanakuwa sehemu ya mfumo wetu wa ulinzi kwa kiongozi wa juu.
Naomba tujadili ni upi uhusiano wenye Kati ya haya mataifa mawili una manufaa kwetu kama nchi.
Kwanza nikulaumu kwa kuonyeshesha wazi wazi kulaumu uongozi wa awamu ya 5 na kuisifia awamu wa 6. Kama mchokonozi au mwanzilishi wa mada hukutakiwa kuonyesha upande. Hiyo ingepelekea wachangiaji kutochangia kiushabiki.
Yote kwa yote elewa kwamba kuna nchi nyingi ambazo hutegemea nchi nyingine kama vyanzo vyao vya mapato. Ni kwa mda mrefu sana Kenye imeitegemea TZ kama chanzo chake cha mapata÷
1. Kwa kutuuzia bidhaa zao za viwandani
2. Viwanda vyao kuendeshwa kutokana na law material za TZ.
3. Kuuza madini yetu kama kwamba wao ndiyo wamiliki au wachimbaji wa madini hayo (alikuwa ni No 2 kwa mauzo ya Tnite Duniani)
Baada ya JPM kuzuia huo ujanja/wizi wake ndiyo wakaanza fugisu figisu ambazo hazina maana.
Pia kumbuka Rwanda ndiyo chanzo cha machafuko ya DRC. Wanaendeleza na kufadhili machafuko hayo kwa maksudi ili waendelee kuwaibia madini yao.
Kwa hiyo hili swala la Kenya na TZ usiliangalie juu juu au kwa mapenzi ya maraisi wetu. Choko choko ya Kenya na TZ hazikuanza leo. Hata JKN na Kenyata walivurugana sana. Kwa Mwinyi ndiyo ikawa kimya kwa sababu mzee mwinyi sera yake ilikuwa ni ruksa kwa kila kitu.
Kumbuka kwa kikwete jumuia yote ya EA walimtenga. Hasa Kenya na Rwanda. Sbb ya kumtenga mimi na wewe hatuijui. Lakini pia ilikuwa wakifanya vikao bila kumhusiha Kikwete.
Wazo la Samia ni wazo sahihi. Lakini aangalie tusije ingizwa choo cha kike. Wakenye wana uweze mkubwa sana wa kucheza na fursa. Wakiona mama anawabana lazima wataanzisha ujinga wao. Kumbuka waliturudishia dhahabu ambayo hawakuwa na sababu ya msingi ya kuturudishia. Kwani waliyokuwa na dhahabu hiyo waliinunua na siyo kwamba waliiba. Na kwa habari ya chini ya capet ni kwamba waliyokuwa na dhahabu hiyo walifidiwa pesa yao na serikali yao. Je walikuwa na umuhimu gani kuturejeshea hizo dhahabu? Wakenya nenda nao kwa umakini mkubwa na siyo kiushabiki.