Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kila mmoja lazima ashangae kuzuka vita vya mara kwa mara nchini Sudan. Hii ni nchi ya kiislamu na ina wasomi wengi wa hali ya juu wa dini hiyo.
Kumbe ina raia jumla 16000 wa Marekani wengi wao wakiwa ni raia pacha, yaani nusu ni wamarekani na nusu ni wasudan. Wakati vita vimepamba moto raia hao wamekuwa wakipiga simu kwa ubalozi wa Marekani nchini Sudan wakitaka wapelekwe huko. Hata hivyo baada ya Marekani kuhamisha wafanyakazi wa ubalozi wao Khartoum raia hao wengine wameambiwa kila mmoja ajitafutie namna yake ya kujiokoa.Hakuna mpango wa serikali ulioandaliwa kwa ajili yao.
Majenerali wanaopigana sasa walikuwa ni washirika wakubwa wa Omar Albashir ambaye mwanzoni alitawala kwa kushirikiana na mwalimu wake Hassan Alturabi na baadae akamuweka pembeni. Mwaka 2019 baada ya chokochoko za muda mrefu dhidi ya utawala wa albashir eti unawauwa waafrika na unalazimisha sharia, hatimae majeneral Burhan na Hemedti walikula njama na kumpindua Albashir.
Mwaka 2021 baada ya mapinduzi hayo wakampindua tena kibaraka wa Marekani aitwaye Hamdouk. Mwaka huu tena majenerali hao wametiwa fitna na kupigana wenyewe kwa wenyewe kitu kinachoonekana ndio kimeimaliza kabisa Sudan. Hakuna mwelekeo wa kiislamu wala wa kidemokrasia. Wanachi wamekata tamaa kabisa.
<iframe width="400" height="500" frameborder="0" src=""></iframe>