Uraia pacha huenda ndiyo sababu ya Sababu vita ya wenyewe kwa wenyewe Sudan



Hivi ni nchi ngapi za Kiafrica zina uraia pacha? Nigeria, Zimbambwe, Tunisia, Zambia, Kenya, Carpe Verde, Angola, Algeria....Na nyingine nyingi...nadhani ziko kama 12 hadi 15.

Kila tatizo la nchi zetu zinapotafutiwa majibu rahisi hatutafika fika popote! Nadhani hata uozo wa ripoti ya CAG inaweza kuwa ni Marekani.Hivi matatizo ya Nigeria/Kenya ambazo zina maelfu ya watu wake wenye uraia pacha wa nchi nyingi za ulaya unasababishwa na Marekani? Lazima tuwe serious ndugu zangu, kutotambua matatatizo kunaweza kuwa ni swala la msingi kwa nini Africa tunakwama mpaka leo! Matatizo mengi sasa hivi katika nchi zetu, ni kwetu sisi wenyewe, hakuna mkono wa mtu toka nje! Na hata kama upo ni sisi wenyewe kwa ujinga na njaa zetu tumefungulia mlango!

Kama kweli ni Marekani ndi sababu, basi katuzidi akili waafrika! Kwa nini basi angalau tusijifunze kutoka kwa hyo Marekani kwa nini ana uwezo wa kutungombanisha!
 
Mkuu kakae Khartoum ndio utajua nimewezaje kuwatofautisha waarabu,wanubi na waabeshi kule Sudani.
 
American phobia
 
Hivi kwanini Tanzania haijafata Raia wake?
 
Diplomats na familia zao ndo walikuwa wa muhimu na ndo maana cease fire imelazimishwa.
Hao wengine watajijua
Thamani yao kwa Marekani si kubwa sana.Kama wameleta fitna nchini humo wacha wale matunda ya fitna zao.
 
Madhara yao usiyaangalie kwa upande mmoja tu.Wengine wanashughulika na kuleta vurugu wapate mali na wengine wanapenda watu wawe mashoga.Nini alichokuwa akipambana nacho Robert Mugabe wa Zimbabwe na mwishowe wajinga wakasahau uzalendo wake katika kuleta uhuru wa nchi hiyo huku wakiweka mbele maslahi ya nchi za Ulaya.
 
Amii: Nadhani jamaa yangu ndiye aliyeangalia upande mmoja.....Kwamba ni Marekani....Je ameiangalia Historia ya Sudan kwa ndani wake? Nimeonyesha mifano ya Nchi nyingi yenye uraia pacha, matatizo ya ndani ni mengi mno! Africa naona bado tunakwama kwenye blame other factors.....kwenye kila kitu! Hiyo inaanza kuwa ni tatizo jingine! Tunakosa kabisa ujasiri wa kukabiliana na matatizo tunayo yazaa sisi wenyewe!

Mtazamo wangu binafsi matatizo mengi ya Nchi za Kiafrica ( almost 70%) Hayana mkono wa nchi za nje!
 
Itakuwa hujaweza kuwatofautisha.Wahabeshi ni kutoka Ethiopia.
Mkuu hadi wasomali na koo zao zote ni jamii za wahabeshi na wamesambaa mpaka Sudani ya sasa,Erteria ya sasa na Dijbout ya sasa.Tofauti ilianza walipopokea ujio wa wageni katika himaya zao miaka zaidi ya 3000 ndio wakagawanyika.Kabla hata Ethiopia haijawa miliki kubwa na falme yenye nguvu na kabla maeneo yao hayajavamiwa na Wamisiri wa kale na Wanubi na Warumi na Waarabu na Waajemi.
 
Itakuwa hujaweza kuwatofautisha.Wahabeshi ni kutoka Ethiopia.
wapo pia Sudan na Somalia , Djibout na hata Eritrea ingawaje kwao ni Ethiopia
 
Hapo umeonesha ukubwa wa tatizo.Pale unaposema waarabu kwa waafrika ndipo ninapoona umejichanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…