Uraia pacha kwa taifa changa ni kifo kuliko faida

Hiyo ni kidogo sana, ugaidi unazaliwa na mataifa ya magharibi na marekani pale yanapotaka rasilimali zenu. Mkigungua rasilimali nyingi ambazo wao hawazifaidi basi jiandaaeni ni ugaidi wa kupandikiziwa. Osama, Sadam, Gadaffi na wengine kule DR Congo, Niger, Afrika ya kati, Sudan kusini, sudan, Msumbiji, Nigeria na kwingine kote kwenye mali nyingi wazungu watapandiza magaidi. Na sifa kuu ya mtu anaefaa kutumiwa kuwa gaidi lazima awe na uraia wa nchi husika na uraia wa nchi nyingine ya wanaomtuma. yaani ni rahisi kuingia kwenye nchi husika kwakuwa anaifahamu vizuri na hamna mashaka nae. Wanaoeneza ushoga huku kwetu ni raia wenzetu wenye passport za kwetu ambao wamerahisishiwa kuingia mataifa yanayodhamini ushoga. Yaani wao ni rahisi kupewa visa za nchi hizo na saa nyingine wamepewa passport za siri za nchi hizo.
 
Maadui wakubwa wa taifa lako wala siyo hao Watanzania wenzako walioenda nje kutafuta maisha. Nchi yako inaliwa na kutekeketezwa na viongozi wa CCM wanaojiita wazalendo na wafia nchi. Ungekazana na hao pengine ningekuelewa.

Rwanda hapa. Wana uraia pacha na diaspora wote wanatambulika kama mkoa wa sita. Na wanapiga kura na kushiriki katika michakato yote ya nchi yao. Kuna ugaidi gani pale? Zambia je? Kenya?

Mawazo yako ni sawa tu na ya serikali. Ukiritimba! Kila mwaka inafyatua wahitimu maelfu wakati haina mifumo imara ya ajira rasmi au sekta binafsi. Matokeo yake vijana hawa "wasomi" wanarundikana tu mitaani. Badala ya kuwafungulia milango waende huko duniani wakapambane inaona nongwa. Ukiritimba wa kupatiwa pasipoti ni shughuli pevu. Ona Kenya inavyofanya. Vijana wake wako duniani kote wakipambana. Na nchi inasonga mbele. Hata wakichukua uraia huko ni sawa!

Dunia ya sasa ni kijiji. Ndiyo maana nchi nyingi za Kiafrika sasa zinaachana na mambo ya viza. Nadhani litakalofuatia ni uraia pia.

Pengine tu huna exposure na/au huelewi hasa kiini cha matatizo ya nchi hii ni nini. Na msipojiangalia - ufisadi huu wa kutisha na ukosefu wa ajira ndivyo vitazaa ugaidi; na siyo diaspora!📌📌📌
 
Na ndio akina waziri wa mambo ya nje, waziri wa utalii wote wana pacha ila kwa kuwa ni ccm, haionekani.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Tutapigwa mpaka taifa liporomoke kama maporomoko ya hanang. Watanganyika hii ni agenda kubwa sana, sio mchezomchezo.
 
Nakiri kuwa sio kila raia wetu ambaye umeukana uraia wa tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine ni mbaya, no no no, wengine wanataka uraia pacha kwa nia safi kabisa na pengine ya kimaendeleo, LAKINI lazima tukumbuke kuwa unapofungua vioo nya gari lako ili upate hewa safi utaruhusu kuingia ndani pia mavumbi, moshi, kelele, inzi, manyigu na harufu usizozihitaji ndani ya gari lako. Diaspora itaruhusu watanzania safi 2000 na kuruhusu wahalifu 10,000 tusiowataaka, tutaruhusu mazuri 5 tunayoyataka na mabaya 80 tusiyoyataka.
 
Rwanda wanatumia diaspora kwa ugaidi, hasa pale wanapotaka kumkamata au kumuua Mrwanda "mhalifu" anaeishi nchi nyingine. Yule anaetumwa kumkamata mtu anaehitilafiana na kagame anaruhusiwa kuwa na Uraia wa aliko mhalifu. Acha kabisa kutoa mfano wa rwanda.
 
Hizo ni instincts zako tu unakaa unajiundia data zako kichwani.

Narudia tena! Ugaidi hapa kwetu utaletwa na kukua kwa matabaka kati ya matajiri na masikini kama tunavyoshuhudia hivi karibuni. Unapokuwa na watu wachache (1-5%) wanaoiba na kujirundikia mabilioni na tunaambiwa mpaka matrilioni huku walio wengi hawana uhakika hata wa kupata mlo mmoja wa uhakika hilo ni bomu unajiundia. Unapokuwa na maelfu ya vijana wasomi lakini hawana ajira na hutaki kuwapa pasipoti ili waende huko duniani wakapambane hilo ni bomu unajiundia maana itafika mahali watachoka tu na kukata tamaa. Na hakuna kitu cha hatari hapa duniani kama binadamu aliyekata tamaa!

Tupunguze ufisadi ili kila mtu afaidike na raslimali zetu. Tuandae mazingira mazuri na mifumo inayoeleweka kwa ajili ya ajira kwa vijana wetu. Vinginevyo kuna siku kitaumana tu! Na haitakuwa sababu ya diaspora!
 
Kenya imebemendwa na wakoloni, watu wao ni watumwa ndani ya taifa lao. Ardhi yote imeporwa na wachache tangu wakati wa ukoloni, hawana njia nyingine zaidi ya kutangatanga huku na huko duniani, sisi hapa hatujafika huko, vijana wetu wanazo options nyingi ndani ya nchi yao bado, fursa zipo, ardhi ipo, bahari ipo, madini yapo wanaweza kwenda kuchimba. kenya hakuna hiyo. hata hivyo ndio maana Kenya wanavamiwa sana kila wakati kuliko tanzania. Bro usione vinaelea vimeundwa barabara.
 
Unanifurahisha sana jinsi unavyounda hoja zako. Kwa hiyo diaspora wengi wa Rwanda (wako elfu/laki ngapi sijui) kazi yao ni hiyo tu? We jamaa bana! 😁😁😁
 
sasa uraia pacha utazuia vipi hiyo kadhia unayisema> Uraia pacha utazuia vipi kukua kwa matabaka hayo? hamna hoja za maana aisei.
 
Yule diaspora wa USA tangu amle mkeo mpaka leo unawachukia diaspora wote
 
Unanifurahisha sana jinsi unavyounda hoja zako. Kwa hiyo diaspora wengi wa Rwanda (wako elfu/laki ngapi sijui) kazi yao ni hiyo tu? We jamaa bana! 😁😁😁
Ni kama vile mtu anapopigia chapuo uraia pacha kwa wote kwaajili ya yeye mmoja aweze kupata njia ya kutiba na kwenda kuishi ughaibuni. Nia inaonekana ni njema kwa wote lakini mlengwa na niyeye na kundi lake. Sasa hivi wanaponea kwa kujipa kinga ya kutoshitakiwa hata wakimaliza kazi lakini aina hii ya kinga sio madhubuti kama ile ya uraia pacha. Kagame ili kuwapata watu wengi wa kuwafuatilia maadui zake ughaibuni alilazimika kupitisha sheria ya uraia pacha, lakini mlengwa mkuu ni yeye sio raia. Ndiyo maana anajigamba kwa kuwaambia adui zake kuwa nitakupata popote pale ule, it is a matter of time, lakini sisi tunashindwa kumpata hata Mange kimambi huko aliko.
 
Yule diaspora wa USA tangu amle mkeo mpaka leo unawachukia diaspora wote
Wakati unaukana Utanzania hukutushirikisha, endelea hivyohivyo kaka. mali kitu gani buana hadi mkatae mwanao kwasababu ana upele.
 
Ukiwa raia speed yako ya kusafirisha mali na kupita mpakani ni kubwa zaidi kuliko speep ya sauti. Kiwango chako cha kuharibu na kufanisha ni kikubwa sana. Yaani unaweza kumpiga panga mgoni wako leo na leo hiyohiyo ukatoweka nchini kabisa nje ya bara la afrika. Ukiwa raia ni rahisi sana kufikisha vilainishi hadi kule nanjilinji ndani kabisa kuliko kama sio raia.
 
sasa uraia pacha utazuia vipi hiyo kadhia unayisema> Uraia pacha utazuia vipi kukua kwa matabaka hayo? hamna hoja za maana aisei.
Watu wawe huru kwenda kusaka maisha ko kote wanakotaka bila kuogopa kupoteza uraia wao. Nchi kama Marekani kuna fursa nyingi sana huwezi kuzipata bila kuwa raia. Watajikomboa huko na wewe huku utakuwa umejipunguzia mzigo na nchi yako itapumua.

Kuwarundika tu hapa hao vijana huku hawana cho chote cha kufanya eti unaogopa wakienda huko sijui watakuwa magaidi ni mawazo finyu sana maana visababishi vya ugaidi vipo na vinajulikana.

1. Tupambane na ufisadi ili raslimali zetu ziwafaidie Watanzania wote

2. Tuunde programu na mifumo mizuri itakayowasaidia vijana wetu kujiajiri na kufanikiwa (mf. Kuwafutia kodi kwa miaka miwili ya mwanzo wakianzisha kibiashara...)

3. Tuwaache waende huko nje wakatafute maisha bila kuogopa kupoteza uraia wao
 
Yule diaspora wa USA tangu amle mkeo mpaka leo unawachukia diaspora wote
Kwani mkeo ni mali yako? akiliwa yeye ameliwa yeye hakuliwa mimi. ana haki zake zote kama binadamu. Kwani wewe mkeo ulimkuta na bikra? ulimuuliza ni nani kaila?
 
Waasisi wa Ugaidi ni nchi za Kiarabu.
 
Kwani mkeo ni mali yako? akiliwa yeye ameliwa yeye hakuliwa mimi. ana haki zake zote kama binadamu. Kwani wewe mkeo ulimkuta na bikra? ulimuuliza ni nani kaila?
Akikuletea magonjwa nayo ni haki.
Kama analiwa na wengine wasiolipia mahari ana tofauti Gani na Malaya wa kununua.
Mwanamke anaejua maana ya ndoa hawezi mvulia chupi mtu asiyemtolea mahari
 
Njia nzuri ni ukimaliza kuwa manamba huko, ukiona umezeeka na pesa unazo ukane uraia wa huku ili rudi huku uwe raia. hata hivyo utakuwa umetenda dhambi kubwa kwakuwa nguvu zako zote za ujana umezitumia kuijenga nchi nyingine ya ugenini sasa unarudi kula usichokipanda. Kodi yako imejenga barabara za marekani na kodi zetu sisi zimejenga barabara za tanzania, unarudi huku kufanya nini? fia hukohuko na uzikwe hukohuko ulikokujenga, hapo veepe??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…