Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Watu wawe huru kwenda kusaka maisha ko kote wanakotaka bila kuogopa kupoteza uraia wao. Nchi kama Marekani kuna fursa nyingi sana huwezi kuzipata bila kuwa raia. Watajikomboa huko na wewe huku utakuwa umejipunguzia mzigo na nchi yako itapumua.sasa uraia pacha utazuia vipi hiyo kadhia unayisema> Uraia pacha utazuia vipi kukua kwa matabaka hayo? hamna hoja za maana aisei.
Kuwarundika tu hapa hao vijana huku hawana cho chote cha kufanya eti unaogopa wakienda huko sijui watakuwa magaidi ni mawazo finyu sana maana visababishi vya ugaidi vipo na vinajulikana.
1. Tupambane na ufisadi ili raslimali zetu ziwafaidie Watanzania wote. Hii ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia ugaidi wa ndani (na hata wa nje)
2. Tuunde programu na mifumo mizuri itakayowasaidia vijana wetu kujiajiri na kufanikiwa (mf. Kuwafutia kodi kwa miaka miwili ya mwanzo wakianzisha kibiashara...)
3. Tuwaache waende huko nje wakatafute maisha bila kuogopa kupoteza uraia wao