Uraia pacha kwa taifa changa ni kifo kuliko faida

Uraia pacha kwa taifa changa ni kifo kuliko faida

Hata bila uraia pacha mali zetu zinaibwa na watanzania na viongozi wetu na kwenda kufichwa nje ya nchi (ulaya, marekani na Asia (Dubai, oman, Singapole, Malaysia, nk) itakuwaje kama wezi hawa watakuwa na fursa ya kuwa na uraia pacha?
Tatizo uraia pacha au sheria mbovu?. Mheshimiwa akiiba hafungwi wale waliosema hela ya madafu na mboga mboga hawana uraia pacha.

Tatizo lipo kwenye mkono wa sheria itungwe sheria ambayo hakuna atokuwepo juu ya sheria akifanya kosa sheria itamfika. Unajua sababu ya kuwepo Interpool?.
 
Hizo ni fikra na maoni yako
Kwanini wapitishe mali na nyie mmelala?
Unajua fika kuwepo au kusiwepo uraia pacha wizi ni kwa sababu za tamaa za wengi ambao wanakubali hata silaha ziingie au zitoke kwa thamani ndogo

Bila kupambana na Rushwa na kutokomeza nakuapia kuanzia maliasili atakula chake, uhamiaji atakugongea muhuri utoke na hata polisi atakula chake hata kama gari inaenda upande na imebeba watu 65

Uraia pacha una faida nyingi tu ila wewe umeona wizi tu wakati wizi umetamalaki hata bado hamna hata reserve za dhahabu wakati mnachimba dhahabu kila leo
Hao marais wote uliowataja ni wale wale tu
Kama watu wanachaguliwa kwa kuhonga halafu wanaenda kupiga magoti ya kinafiki makanisani unategemea nini

Nani aliehimiza katika wote hao pamoja na mawaziri wao wa fedha kuweka Dhahabu Bank kuu?
Algeria wanaongoza kwa gold reserves ya 174 metric tons ambayo ina thamani ya $10b
Sisi tuna nini cha kujivunia leo
Hela zinapigwa na hao hao viongozi na kuzipeleka China sio raia wa kawaida
Sasa hao wana uraia wa China?
Ndugu yangu wizi wa kura uko dunia nzima. Trump Na watu wake waligomea matokeo ya uchaguzi kwanini? Siku zote unadharau kwenu kwa sababu za kijinga kabisa. Mnabaguliwa kwa rangi zenu lakini mnajifanya mnayo njaa sana. Eti mmeukata!!! Upweke, ubaguzi, kqzi ngumu Na kodi kubwa ndio maisha ya kawaida ng'ambo.
 
Hizo ni fikra na maoni yako
Kwanini wapitishe mali na nyie mmelala?
Unajua fika kuwepo au kusiwepo uraia pacha wizi ni kwa sababu za tamaa za wengi ambao wanakubali hata silaha ziingie au zitoke kwa thamani ndogo

Bila kupambana na Rushwa na kutokomeza nakuapia kuanzia maliasili atakula chake, uhamiaji atakugongea muhuri utoke na hata polisi atakula chake hata kama gari inaenda upande na imebeba watu 65

Uraia pacha una faida nyingi tu ila wewe umeona wizi tu wakati wizi umetamalaki hata bado hamna hata reserve za dhahabu wakati mnachimba dhahabu kila leo
Hao marais wote uliowataja ni wale wale tu
Kama watu wanachaguliwa kwa kuhonga halafu wanaenda kupiga magoti ya kinafiki makanisani unategemea nini

Nani aliehimiza katika wote hao pamoja na mawaziri wao wa fedha kuweka Dhahabu Bank kuu?
Algeria wanaongoza kwa gold reserves ya 174 metric tons ambayo ina thamani ya $10b
Sisi tuna nini cha kujivunia leo
Hela zinapigwa na hao hao viongozi na kuzipeleka China sio raia wa kawaida
Sasa hao wana uraia wa China?
Ukiweka reserve kubwa ya Dhahabu kabatini utapata wapi fedha za kigeni zinazohitajika kuagiza bidhaa nje Na kulipa madeni? Huna unachojua kwenye hili. Kwanza migodi inamilikiwa Na wenye mitaji Na mbinu za kuchimba kuyoka ulaya Na marekani. Masoko ya Dhahabu yanamilikiwa Na wazungu.
 
Huyu hajui anachokisema. Leo hii mtu ye yote akiwa na pesa anaweza kupata kitambulisho cha NIDA, cha utaifa na hata pasipoti kabisa. Kuna mtu ana uchungu na nchi hii? Wasomali wengi tu wanapata namba za NIDA na pasipoti. Yeye eti anahangaika na diaspora! Eti wataleta ugaidi 😁

Adui mkubwa wa nchi hii ni UFISADI na kukosa uzalendo!
Binafsi sioni shida kwa mgeni kupata uraia Na kuishi Tanzania kushiri kuijenga nchi kwa kodi za kazi sake, lakini sio kodi yako unawalipa wainhereza lakini una uraia wa tanzania pia Na ufaidi matunda ya kodi za watu wengine. Sio kweli.
 
Kuna sababu dhaifu sana za kuhalalisha uraia pacha. Nchi zetu hizi zina mifumo legelege sana ya kudhibiti uhalifu na wizi wa mali na rasilimali za taifa.

Hata bila uraia pacha mali zetu zinaibwa na watanzania na viongozi wetu na kwenda kufichwa nje ya nchi (ulaya, marekani na Asia (Dubai, oman, Singapole, Malaysia, nk) itakuwaje kama wezi hawa watakuwa na fursa ya kuwa na uraia pacha?

Hata nchi ndogo/changa zenye uraia pacha hatuoni faida za maana wanazozipata kwa kuwa na uraia pacha zaidi ya kuongezeka kwa wizi na utapeli ndani ya nchi zao tu. hata nchi zilizoruhusu uraia pacha (diaspora) naazo ni masikini pia, zinapigana, na wizi mwingi na mkubwa wa rasilimali zao. hatuna cha kujifunza kutoka kwa nchi hizo.

Faida tutakayopata kama tutaruhusu uraia pacha ni ndogo sana by far kuliko hasara tutakayoingia. Sababu ziliwafanya Nyerere, karume, mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na magufuli kuukataa Uraia wa nchi mbili bado zipo hadi kesho.

Kuna watu wanatoa sababu dhaifu sana za kuruhusu uraia pacha za kupata wachezaji wa mpira na wawekezaji, ni za kipuuzi kabisa. Tutapanua lango la kupitia wezi wa mali zetu na kutumia barabara pana kuzisafirisha huko Swiss na visiwa vya Jersey kwa urahisi kabisa mchana kweupe.

Siungi mkono upuuzi huu.

Nadhani umeandika huu uzi kwa hisia sio maarifa. Emotions exceed intelligence. Zifahamu kwanza sheria na kanuni za uraia pacha. Pia zitambue obligations and duties anazokua nazo mtu mwenye uraia pacha.

Kusema kwamba uraia pacha ni chanzo cha wizi ni ufinyu wa kupambanua mambo. Kama tungetumia jicho hilo dhaifu kupambanua mambo nadhani hata investors kutoka nje tusingeruhusu.
 
Watu wawe huru kwenda kusaka maisha ko kote wanakotaka bila kuogopa kupoteza uraia wao. Nchi kama Marekani kuna fursa nyingi sana huwezi kuzipata bila kuwa raia. Watajikomboa huko na wewe huku utakuwa umejipunguzia mzigo na nchi yako itapumua.

Kuwarundika tu hapa hao vijana huku hawana cho chote cha kufanya eti unaogopa wakienda huko sijui watakuwa magaidi ni mawazo finyu sana maana visababishi vya ugaidi vipo na vinajulikana.

1. Tupambane na ufisadi ili raslimali zetu ziwafaidie Watanzania wote. Hii ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia ugaidi wa ndani (na hata wa nje)

2. Tuunde programu na mifumo mizuri itakayowasaidia vijana wetu kujiajiri na kufanikiwa (mf. Kuwafutia kodi kwa miaka miwili ya mwanzo wakianzisha kibiashara...)

3. Tuwaache waende huko nje wakatafute maisha bila kuogopa kupoteza uraia wao
Mifumo gani kaka. Taifa makini haliwezi kutengeneza mifumo inayowarahisishia vijana wake wenye nguvu, ujuzi Na maarifa (nguvukazi) iondoke nchini. Mtawala kama huyo atakuwa ni mpumbavu mkubwa. Mchi inajengwa Na vijana wake sio wazee. Tunahitaji vijana wetu jeshini, kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, viwandani Na kwenye huduma mbalimbali Na hatimae walipe kodi kwa maendeleo ya taifa lao.
 
Hivi kwa nini watanzania huwa tunafikiri kana kwamba Tanzania ndio nchi pekee yenye amani hapa duniani kiasi cha kujisifia hiyo amani?
Amani iliyoko Tanzania hats marekani haiko Na haipatikani. Hakuna amani kabisa kufa ni kitu cha kawaida kabisa, upweke (loneliness) mkubwa, madeni mengi, homeless mengi, wenye stroke na stresses wengi, kila kitu ghali sana.
 
Nadhani umeandika huu uzi kwa hisia sio maarifa. Emotions exceed intelligence. Zifahamu kwanza sheria na kanuni za uraia pacha. Pia zitambue obligations and duties anazokua nazo mtu mwenye uraia pacha.

Kusema kwamba uraia pacha ni chanzo cha wizi ni ufinyu wa kupambanua mambo. Kama tungetumia jicho hilo dhaifu kupambanua mambo nadhani hata investors kutoka nje tusingeruhusu.
Wacha ngonjera. Kwani wahindi walipotimuliwa Uganda na idd amin walienda wapi? Uraia pacha unakuwezesha kuchuma mali na kwenda kuihifadhi kwenye mabenki ya nchi nyingine kwa urahisi.
 
Aliyewaambia watanzania ni matajiri sana, kila mtu anawaonea wivu na anataka kuwaibia aliwajaza ujinga wa kiwango cha lami. Mmekua mazuzu na woga kama kunguru. Kila kitu mnaogopa
 
Huna akili.

Nimejisikia vibaya sana kukwambia “huna akili”
Ila nilikuwa sina jinsi.
 
Hivi huyu alieandika huu uzi kwamba analipwa?

Maana anajibu pumba huko, [emoji23][emoji23][emoji23]

Kama hivyo ipigwe kura watanzania wachague.
 
Tukiruhusu Uraia Pacha tunarahisisha sana shughuli za kiuchumi na kibiashara. Kwa mfano kama mimi ni Mtanzania ambaye nafanya biashara na nchi kama China, badala ya kuhangaika na uombaji wa VISA kila mara ninaposafiri, basi natumia tu Passport yangu ya Uchina nakuwa naingia na kutoka China kama ninavyotaka. Yaani nikiamka asubuhi naweza kuanza safari ya kwenda china kama vile naenda Matejoo.
 
Niambie mfano wa taifa dogo kama letu ambalo linafaidika sana na uraia pacha kiasi cha kutamani kuiga maisha na hali yao kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mnatafutia majizi njia nyepesi ya kutoroshea nje mali zetu.
Wewe ndio uonyeshe taifa lipi limeathirika sana kutokana na uraia pacha. Unakuja na hoja nyepesi eti uraia pacha unaleta majizi. Kwa hiyo kila anayetaka uraia pacha ni mwizi? Mikataba mibovu, EPA na uozo nwingine uliletwa na uraia pacha?
 
URAIA PACHA: KUUNGANISHA TANZANIA NA DIASPORA KWA MAENDELEO ENDELEVU.


UTANGULIZI

Uraia pacha ni hali ya kuwa raia wa nchi mbili kwa wakati mmoja. Inawawezesha watu kufurahia haki na huduma za kisheria, kiuchumi, kisiasa, na kijamii katika nchi zote mbili wanazohusika. Uraia pacha pia unachochea ushirikiano wa kimataifa, kukuza uhusiano wa kibalozi, na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na diaspora yake. Diaspora ya Tanzania ina jukumu muhimu katika maendeleo ya nchi yao. Wanaleta mchango mkubwa kwa njia mbalimbali, kama vile kutuma fedha za kigeni, kuwekeza katika miradi ya maendeleo, na kujenga uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi wanazoishi.

MSIMAMO WA SHERIA ZA TANZANIA KUHUSU URAIA PACHA

Sheria za uraia nchini Tanzania zinatokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Sheria hizi zinatambua aina mbili za uraia: uraia wa kuzaliwa na uraia wa kupata. Uraia wa kuzaliwa unahusu watu wanaozaliwa ndani ya mipaka ya Tanzania. Uraia wa kupata unahusu watu ambao wanaweza kupata uraia wa Tanzania kupitia taratibu za kisheria.

Hata hivyo, sheria za uraia nchini Tanzania haziruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili kwa wakati mmoja. Msimamo wa serikali ya Tanzania kuhusu uraia pacha umekuwa kwa mujibu wa sheria za uraia zilizopo. Serikali imekuwa ikisisitiza kuwa uraia pacha unaweza kusababisha usawa na mkanganyiko miongoni mwa Watanzania. Hivyo, Tanzania imeendelea kutekeleza sera ya kutokuruhusu uraia pacha, kwa lengo la kudumisha utambulisho na uhuru wake wa kitaifa.

FAIDA ZA URAIA PACHA KWA MAENDELEO YA TANZANIA

Kuwezesha diaspora kufurahia haki za raia na kuwekeza nchini: Uraia pacha unatoa fursa kwa diaspora ya Tanzania kuwa na haki kamili za raia katika nchi yao ya asili. Kwa kuwa na uraia pacha, Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanaweza kufurahia haki za kimsingi kama vile kumiliki mali, kufanya biashara, kupata huduma za afya, na kushiriki katika shughuli za kisiasa. Hii inawawezesha kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya nchi yao, kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.

Ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya Tanzania na diaspora: Uraia pacha unajenga jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya Tanzania na diaspora yake. Diaspora inayokuwa na uraia pacha inaweza kuleta ujuzi, maarifa, na mtaji wa kiuchumi kutoka nchi wanazoishi kwenda Tanzania. Hii inaweza kusaidia katika kukuza sekta mbalimbali za uchumi kama vile viwanda, kilimo, utalii, na huduma za kitaalamu. Ushirikiano huu unaweza kusaidia kuboresha uvumbuzi, teknolojia, na ubunifu, na hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

Kuchochea maendeleo ya kijamii na kiutamaduni: Uraia pacha unawezesha diaspora ya Tanzania kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiutamaduni ya nchi yao. Diaspora inayokuwa na uraia pacha inaweza kuleta michango ya kiutamaduni, mila, na desturi kutoka nchi wanazoishi, na kushirikiana na jamii za Kitanzania. Hii inasaidia kudumisha na kukuza utambulisho wa Kitanzania, kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa, na kushirikiana katika shughuli za kijamii kama vile miradi ya maendeleo ya jamii, elimu, afya, na mazingira.


UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA DIASPORA NA JUHUDI ZA KUHAMASISHA URAIA PACHA

Wito wa diaspora kuhusu uruhusu wa uraia pacha: Diaspora ya Tanzania inaona kuwa uraia pacha ni haki yao na fursa ya kuchangia maendeleo ya nchi yao. Uraia pacha utawezesha diaspora kushiriki kikamilifu katika masuala ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii nchini Tanzania. Wamekuwa wakiomba serikali kufanya mabadiliko ya sheria na katiba ili kuruhusu uraia pacha.

Kushirikiana na asasi za kiraia na vyama vya siasa katika kampeni na uhamasishaji: Diaspora ya Tanzania haijakaa kimya katika kutetea haki yao ya uraia pacha. Wamekuwa wakijenga ushirikiano na asasi za kiraia na vyama vya siasa ili kuongeza nguvu na sauti zao. Wamekuwa wakitoa taarifa na ujuzi kuhusu faida za uraia pacha kwa watanzania wote na kufanya mikutano kupitia mitandao mbalimbali ili kufikisha ujumbe wao.

Kufuatilia mchakato wa mabadiliko ya katiba na sheria za uraia: Diaspora ya Tanzania inatambua kuwa mchakato wa mabadiliko ya katiba na sheria za uraia ni fursa muhimu ya kupigania haki yao ya uraia pacha. Wamekuwa wakifuatilia hatua zote za mchakato huu, wakishiriki katika vikao vya umma, wakitoa maoni yao, na kudai mabadiliko yanayowiana na matarajio yao. Wanalenga kuhakikisha kuwa uraia pacha unajumuishwa katika rasimu ya katiba mpya na sheria mpya za uraia.


MIFANO YA NCHI NYINGINE NA MAONI YA UTAFITI

Uraia pacha katika nchi nyingine za Afrika na athari zake: Nchi kadhaa za Afrika zimeruhusu uraia pacha na zimeona athari chanya kwa maendeleo yao. Kenya, Nigeria, na Ghana zimeona ongezeko la uwekezaji, ushirikiano wa kiuchumi, na mchango mkubwa wa diaspora. Uraia pacha umewezesha diaspora kuchangia katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, miundombinu, na uvumbuzi wa kiteknolojia. Mifano hii inatoa mwongozo na ushahidi wa faida za uraia pacha katika kuunganisha Tanzania na diaspora yake kwa maendeleo endelevu.

Maoni ya watafiti na wadau kuhusu uraia pacha na maendeleo: Watafiti na wadau mbalimbali wamefanya utafiti na kutoa maoni yao kuhusu uraia pacha na jinsi inavyoathiri maendeleo ya nchi. Maoni haya yanasisitiza umuhimu wa kuruhusu uraia pacha kwa maendeleo ya nchi. Uraia pacha husaidia kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na diaspora, kuchochea uwekezaji, kuleta teknolojia na ujuzi kutoka nje, na kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Maoni haya yanasisitiza pia umuhimu wa kuweka mfumo mzuri wa udhibiti na usimamizi.


HITIMISHO.
Andiko hili limejadili umuhimu wa uraia pacha katika kuunganisha Tanzania na diaspora kwa maendeleo endelevu. Uraia pacha unawapa watu faida za kisheria, kiuchumi, kisiasa, na kijamii katika nchi zote wanazotambulika kuwa raia. Diaspora ya Tanzania inachangia maendeleo ya nchi kupitia uwekezaji, kutuma fedha za kigeni, na kukuza ushirikiano.

Sheria za uraia nchini Tanzania haziruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili kwa wakati mmoja, lakini kuna umuhimu wa kuzingatia mabadiliko ya sheria na katiba ili kuwezesha uraia pacha. Uraia pacha una faida kwa maendeleo ya Tanzania, kama vile kuwezesha diaspora kufurahia haki za raia na kuwekeza nchini, kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia, na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiutamaduni. Kuruhusu uraia pacha kutachochea ukuaji wa kiuchumi, kuongeza ajira, na kuboresha hali ya maisha. Ni muhimu pia kuzingatia maoni ya watafiti na wadau katika mchakato wa kufikia maamuzi sahihi.
 
Ukiweka reserve kubwa ya Dhahabu kabatini utapata wapi fedha za kigeni zinazohitajika kuagiza bidhaa nje Na kulipa madeni? Huna unachojua kwenye hili. Kwanza migodi inamilikiwa Na wenye mitaji Na mbinu za kuchimba kuyoka ulaya Na marekani. Masoko ya Dhahabu yanamilikiwa Na wazungu.
Kwani nyie vilema? Kwanini msichimbe?
Hata nyanya kusafirisha unahitaji utoe hongo ofisi 10 sasa hizo $ utazipataje
Dhahabu ni akiba na wanaoweka sio wajinga
Nimekupa mfano wa mwafrika mwenzio wewe unakumbilia wazungu

Akili yako unaona mzungu tu ndio anaweza ila wewe unasubiri akulishe eti
Amka
Leta hata parachichi ulaya
 
Ndugu yangu wizi wa kura uko dunia nzima. Trump Na watu wake waligomea matokeo ya uchaguzi kwanini? Siku zote unadharau kwenu kwa sababu za kijinga kabisa. Mnabaguliwa kwa rangi zenu lakini mnajifanya mnayo njaa sana. Eti mmeukata!!! Upweke, ubaguzi, kqzi ngumu Na kodi kubwa ndio maisha ya kawaida ng'ambo.
Twende kwa hoja, acha kutukana
Maisha ya nje ni bora kwa kila nyanja
Mimi situkani kwetu ila mbadilike na wizi na uongo na kubebana
Leo mna chipukizi watoto wanaanza kufundishwa bado wadogo ili waje kuiba ukubwani
Na nyie mnachekelea tu
Nje na ndani kama maisha yanalingana sawa ila ni mbingu na ardhi
 
Ugaidi unazaliwa na suppression ndugu. Ugaidi unazaliwa na uonevu hauletwi na uraia pacha be careful

Wale masheikh walihukumiwa kwa ugaidi, ni raia pacha wa nchi gani na nchi gani?

Hamza polisi walipomuua wakasema ni gaidi, alikuwa ni raia pacha wa nchi gani na nchi gani?
Wapo watu wanatoka nje,wenye uraia pacha,wanaingia nchini na kukutana na hao wanaotekeleza ugaidi,kwa kuwashawishi na kuwalipa,watekeleze huo ugaidi.
 
Kaeni hukohuko umanambani na vijisent vyenu, sisi amani kwetu ni zaidi ya fedha, hatutaki magaaidi wenye passport za nchi tofauti.
Huu ndio ukweli,magaidi huwa wanatumia sana uraia pacha kufanya ugaidi,chunguza sana.Hata huko Palestina,wale wanaofanya ugaidi,wana uraia pacha.
 
Back
Top Bottom