Uraia pacha na Tanzania

Uraia pacha na Tanzania

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
Suala la uraia pacha, limejitokeza tena kuwa hoja nzito katika mkutano wa tatu wa uratibu wa wadau Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora), huku baadhi wakiitaka serikali kuharakisha mchakato wa kuanzisha utaratibu huo. Walisema Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapata adha kubwa na wengine wanashindwa kuwekeza, kurudi au hata kusaidia familia zao kile walichochuma kwa sababu tofauti zikiwemo za usumbufu na kupanda kwa gharama.

Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere, (Chadema), alisema suala la uraia pacha ni muhimu na kwa sasa halikwepeki. Aliitaka serikali kuharakisha utaratibu wa huo ili kuwapunguzia adha Watanzania wanaoishi nje ya nchi na ambao hawataki kuukana uraia wao.

Kuwa na uraia pacha ni muhimu, wapo Watanzania waliokwenda Marekani kwa sababu tu ya ukimbizi wa kiuchumi na wakapata watoto huko, lakini watoto wao wanakuwa ni Wamarekani, kama kungekuwa na uraia pacha, hao wangeweza kuwa raia wa Tanzania na Marekani kwa wakati mmoja, alisema.

Pia alisema Mtanzania aliyezaliwa Marekani akiwa na uraia pacha hataweza kuhatarisha vitegauchumi vyake iwapo atapenda kuwekeza nchini au hata huko Marekani. Watu wetu wa diaspora wanafanya mambo mengi na makubwa katika kuchangia uchumi wa taifa letu, lakini kwa kuwa misaada yao haijaorodheshwa na hakuna takwimu, michango yao haijulikani, alisema na kuongeza: Naiomba serikali kulitafutia ufumbuzi suala la uraia pacha mapema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, alisema suala la uraia pacha ni la Muungano na la kikatiba na kuwa lipo kwenye mchakato na litapatiwa ufumbuzi kwa kuwashirikisha Watanzania wote (Bara na Visiwani).

Alisema kutokana na vuguvugu la mchakato wa kuwa na Katiba Mpya suala hilo linaweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, Haule alisema wizara yake imezielekeza balozi zake zote kuorodhesha Watanzania wanaoishi nje, shughuli wanazozifanya na utaalamu walionao ili kuwapa nafasi nzuri ya kuwekeza nchini kama wanataka.

IPPMedia
 
Serikali yetu imekalia kula tu, kuorodhesha watu huko ughaibuni watapewa bajet au wanataka jua idadi yao ili watoe rushwa watakayonufaika ili kuruhusu hoja ya uraia pacha kujadiliwa?
 
Tanzania inapowaruhusu raia wa nchi nyingine kuasiliwa nchini hawawanyang'anyi passport zao, kwa maana nyingine wanawaruhusu hao raia wa nchi nyingine kuwa na uraia pacha. Sasa iweje wazawa kuwakomalia ambao watainufaisha zaidi nchi?
 
Na wivu huu wa viongozi na wabunge wa CCM tutafikia muafaka?
 
Nimekuwa nikiona ktk vyombo vya habari watu mbalimbali wakiwa na uraia wa nchi mbili, je, serikali ya Tanzania inaturuhusu tuwe na uraia wa nchi mbili? Kama hairuhusu ni hatua gani za kisheria mtanzania aliye na raia mbili zitachukuliwa juu yake?
 
kikubaliani na uraia wa nchi mbili uo ni uhuni kwa hao mafisad once watakapo harhabu inakua kama balali.
 
Chonde chonde katiba mpya iruhusu Uraia pacha maana watu wengi hapa Ulaya na Marekani wanaotokea Tanzania tushachukua raia za huku kutokana na sababu nyingi sana mfano:
-Uhuru wa kusafiri toka nchi moja kwenda nyingine bila visa au misururu ya kuomba visa.
- Kupata mikopo ya nyumba na kuendesha biashara hapa Ulaya
-Kusoma kwa bei ndogo na misaada mingine ya kijamii.

PAMOJA na hayo bado tuna mchango mkubwa na taifa letu la Tanzania maana kile kidogo tunapata tunapeleka kwa ndugu au wazazi wetu walioko Tanzania. Pia tunaweza kuwekeza kwa urahisi huko nyumbani kama tutapata haki ya uraia pacha.

HATUTAKI kusikia kuwa kwanini tumeukana uraia wa Tanzania kwa sababu tunazo pia sababu ambazo wewe uliyeko au ambaye hujaukana urai wa Tanzania huwezi kuzijua au hutaki kuzijua mfano tumeoa au kuolewa huku, tunaishi huku na kufanya kazi huku, tunapata fursa mabazo tusingezipata na pia tuna haki za kikatiba katika nchi hizi tulipo kwa sasa. Wakati kubadilisha pasi ya Tanzania inaweza kuchukua miezi 4 ukiwa hapa Ulaya, ukirenew pass hapa Ulaya unaletewa kwa posta ndani ya siku 3 au 4- unakuwa huru kusafiri ulaya yote bila visa na USA unaenda pia bila visa kwa siku zisizozidi 90. Pia unagonga visa DAR,Kia na sehemu ingine bila shida...so tuna sababu lakini tunahitai uraia pacha pia ili tuijenge Tanzania.
 
Naunga mkono hoja asilimia 100. Rwanda wameshaanza angalia nchi inavyoendelea kwa kasi. Wanyarwanda wengi wana uraia pacha, wakikusanya nje wanapeleka kwao kujenga nchi.
 
Rafiki, we jiachie na fanya kwa sehemu yako. Hakuna atakayekufukuza ukija kwenu. "Mwenda kwao si mtoro".
 
DIASPORA IN USA TELECONFERENCE MARCH 20, 2014, 8PM EASTERN STD TIME

Waheshimiwa Wanadiaspora,

Viongozi wa Jumuiya za Watanzania za Marekani wakishirikiana, ZADIA na DICOTA, wanapenda kuwatangazia kuwa kutakuwa na teleconference siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi kuanzia saa mbili usiku(8:00PM) kwa saa za Eastern Time.

Lengo ni kuwapa muhtasari wa masuala yanayoendelea kule Dodoma kwenye Bunge Maalum la Katiba na kuwafahamisha mpaka sasa tumefikia wapi katika kuhakikisha suala la uraia pacha linaingizwa kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanzania na Watu wenye asili ya Kitanzania wanaoishi Marekani wote mnaombwa kuudhuria.

Ili uweze kushiriki kwenye Teleconference hii piga namba 712-432-1500 halafu ingiza pin namba ikifuatiwa na alama ya reli kama ifuatavyo: 465228#.

Wote mnakaribishwa!

Diaspora Constitution Petition- FUNDING:

Diaspora Constitution Petition- FUNDING by Tanzania Diaspora - GoFundMe

Imetolewa na:
Viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Marekani, ZADIA na DICOTA.
Tarehe 18 Machi 2014

Source: CHADEMA DIASPORA : DIASPORA IN USA TELECONFERENCE MARCH 20, 2014, 8PM
 
Leo nimeangua kilio cha kufa mtu baada ya kusoma gazeti la ippmedia ,nipashe warioba amesema kwenye hiyo rasimu hakuna uraia pacha ,nashaangaa sana wakati viongozi wanapotembelea ulaya na marekani wanasema wataweka uraia pacha ,hao viongozi bhana hawatabiriki, wanataka wakija Amerika na Ulaya wanakutana na jamiii ya watanzania wanaoishi hapo na kula chakula chao , na kuwaahidi watalishughukia Hilo swala ,hawa watu bhana wakija hapa uk or USA achanena nao wanatupotezea muda .wanaongelea tuu mambo ya muungano kwenye hiyo katiba mpya ,what the hell bout muungano ,sisi wabara tuwaachie zanzabar Yao bhana ,mbona Kenya ,Uganda ,Mexico na Nchi nyingi sana wa uraia pacha .viongozi wa Tanzania achane blabla ,mkija hapa uk or USA hamana kukutana na jumuiya ya watanzania maana mnawauza kwa kiswahili kirefu , mkitoka hapo mmeshawasahu ,viongozi wa tanzania kuweni makini wakati mnapokuja kutembelea uk or USA na kuwaahidi mtawapatia uraia pacha ,tunaacha kazi zetu na kuja kuwazikiliza mkitoka hapo nje tu mmeshasahau Kila kitu ,viongozi wa Tanzania kuweni wakweli Kama kitu hakiwezekani Si useme tu ,Kila mtu achape lapa or kusepa.nachukia sana hawa waongo ,
 
Mlikuwa hamuwajui hawa magamba kuwa ni waongo? Sasa ndio mtawajua vizuri !!!!
 
yeah, hata mimi nimeshangaa kuhusu hili, ila nadhani kilichopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba kinarandana na matakwa ya waliokuwa wanataka uraia pacha.
Kwa kuwa nina asili ya Tanzania, lakini nimechukua uraia wa nchi nyingine, sitaacha kupata haki zote muhimu anazopata raia wa Tanzania kama kumiliki ardhi n.k.
Kitakachoshindikana ni kufanya kazi katika sehemu nyeti za Tanzania, sehemu kama Usalama wa Taifa, Idara ya Uhamiaji n.k.

Hivyo ndivyo nilivyoielewa.
 
Wakuu ni wazi kuwa swala la uraia pacha kama vile limezimwa rasmi katika mchakato huu wa katiba mpya...

JK ambae ni miongoni mwa waliokua wapiga upatu wakubwa wa uraia pacha ameshindwa kabisa kushawishi wajumbe wa bunge maalum la katiba walikubali tofauti na lilivyoachwa kwenye rasimu...

Nimemsikiliza JK kuanzia mwanzo mpaka mwisho na kama ilivyokua mategemeo ya diplomats wengi waliotoa ushauri kabla ya hotuba yake bungeni ikitegemewa atashawishi wajumbe walitazame swala hilo alikacha na hakuzungumzia kabisa..

JK amegusia mambo mengi lakini kitendo cha kutozungumzia kabisa suala la uraia pacha kinavunja moyo wa wapiganaji wa sera hii kuendelea nalo...
Na hapo inaonesha kushindwa kupenyezwa kwa swala hili kwenye mchakato huu wa katiba mpya unaoelekea ukingoni ni matumaini yaliyofifia kama si kutoweka....

Ndugu zetu wana diaspora wameachwa kando ni wakati wa kuamua hoja mbadala... Naomba kuwasilisha,,,
CC: Chadema Diaspora .. Chris Lukosi.... Tuko ...@w .c. malecela chama OLESAIDIMU et al
 
Mmeshajaribu kuwahonga hao wajumbe wa bunge maalumu? Au mmesahau hii nchi inaendeshwaje? Mkono mtupu haulambwi.
 
Jk kanyamaza tu we subirii utaona baadaee ndio utamjua Jk
 
Amezungumzia kero na pia kasema kuna mambo mengi sana ya kujadili kwenye hii katiba, sio mambo ya muungano tu.

Hakutakuwa na uraia wa nchi mbiliu bali kutakuwa na haki ya wazawa kupewa haki za uraia ili kupunguza usumbufu.

Ngoma itakuwa pale kwa wale watakaoambiwa walete passport zao halafu zinaandikwa place of birth Afghanistan, hapo unakuwa umepoteza haki ya kuzaliwa .
 
Nadhani juhudi chache zilizofanywa na wanadiadpora zilifanyika too late...
Laiti kungekuwa na juhudi za makusudi ambazo zingelenga wakati wa mchakato wa kukusanya maoni, pengine zingezaa matunda
 
Nadhani juhudi chache zilizofanywa na wanadiadpora zilifanyika too late...
Laiti kungekuwa na juhudi za makusudi ambazo zingelenga wakati wa mchakato wa kukusanya maoni, pengine zingezaa matunda

Mkuu ni kweli suala hili naona halijapewa uzito unaostahili..
 
Back
Top Bottom