Uraia pacha na Tanzania

Uraia pacha na Tanzania

Amezungumzia kero na pia kasema kuna mambo mengi sana ya kujadili kwenye hii katiba, sio mambo ya muungano tu.

Hakutakuwa na uraia wa nchi mbiliu bali kutakuwa na haki ya wazawa kupewa haki za uraia ili kupunguza usumbufu.

Ngoma itakuwa pale kwa wale watakaoambiwa walete passport zao halafu zinaandikwa place of birth Afghanistan, hapo unakuwa umepoteza haki ya kuzaliwa .

Mkuu Lukosi miongoni mwa mambo ambayo JK alishauriwa na ilitegemewa ayatamke wazi ni pamoja na hili la uraia pacha but hajafanya hivyo...

Vigogo wengi wa foreign affairs wamepigania hili mpaka wamekata tamaa sasa ilitegemewa kete ya mwidho JK amalize kalikalia kimya sasa je nani atamfunga paka kengele?
 
Wewe ulitaka aseme wapeni uraia kila mtu?

JK hakwenda pale kupiga kampeni...
 
Wewe ulitaka aseme wapeni uraia kila mtu?

JK hakwenda pale kupiga kampeni...

Mbona wakati wote wa speech yake alikua anapiga debe tu juu ya misimamo ya chama chake dhidi ya rasimu ya katiba.
Juu ya hili la DUAL CITIZENSHIP basi alipaswa aoneshe msimamo wake pia.
 
Wanadiaspora wameshindwa kutoa sababu mathubuti za kwanini wanataka uraia-pacha, wengi ukiwauliza wanasema tunatuma hela bongo, mara wanatuonea wivu na sababu kibao zisizo za msingi

Tuweke hoja za kueleweka mezani, uraia pacha utamnufaisha vipi mwanadiaspora na nchi kwa ujumla sio kuomba uraia-pacha kama tunaagiza pombe kwenye kilabu
 
Jambo la uraia pacha si moja ya mambo muhimu sana kwa Tanzania..ikumbukwe kwamba watanzania walioko nje ni kiduchuu sana mpaka kulifanya hili jambo eti rais wa JMT nchi yenye population ya watu millioni 45 aongelee watu wa ughaibuni wanaotaka uraia pacha ambao hawazidi hata 3m...kuna mambo makubwa ya kujadili sio hili...please, give him a break!!!
 
Amezungumzia kero na pia kasema kuna mambo mengi sana ya kujadili kwenye hii katiba, sio mambo ya muungano tu.

Hakutakuwa na uraia wa nchi mbiliu bali kutakuwa na haki ya wazawa kupewa haki za uraia ili kupunguza usumbufu.

Ngoma itakuwa pale kwa wale watakaoambiwa walete passport zao halafu zinaandikwa place of birth Afghanistan, hapo unakuwa umepoteza haki ya kuzaliwa .
​Hivi unajua huko Tabora kuna kijiji kinaitwa Muscat??na unajua pia kuna kijiji kinaitwa Dubai???kwa hio suala lako limekosa mashiko...mtanzania ni mtanzania tu yuko tofauti na wanigeria,wakenya,waganda nk...haki yake apewe haijalishi imeonesha kazaliwa wapi.
 
Wewe ulitaka aseme wapeni uraia kila mtu?

JK hakwenda pale kupiga kampeni...

Mkuu si hivyo..

JK angesema walitazame kama alivyotumia muda mwingi kukazia kwenye muungano...ukomo wa ubunge n.k n.k
Ikumbukwe hili ni suala nyeti sana ambalo linahitaji msukumo mkubwa wa viongozi..
 
Jambo la uraia pacha si moja ya mambo muhimu sana kwa Tanzania..ikumbukwe kwamba watanzania walioko nje ni kiduchuu sana mpaka kulifanya hili jambo eti rais wa JMT nchi yenye population ya watu millioni 45 aongelee watu wa ughaibuni wanaotaka uraia pacha ambao hawazidi hata 3m...kuna mambo makubwa ya kujadili sio hili...please, give him a break!!!

Mkuu hata angekuepo mmoja bado anahaki ya uzawa ktk nchi yake
 
​Hivi unajua huko Tabora kuna kijiji kinaitwa Muscat??na unajua pia kuna kijiji kinaitwa Dubai???kwa hio suala lako limekosa mashiko...mtanzania ni mtanzania tu yuko tofauti na wanigeria,wakenya,waganda nk...haki yake apewe haijalishi imeonesha kazaliwa wapi.
Mkuu sina maana kubagua ambao hawakuzaliwa Tanzania. Mimi mwenyewe wanangu wamezaliwa huku hivyo siwezi sema hivyo

Lakini serikali itabidi iwe makini wasijewapa uraia watu wasio stahili
 
Mkuu lusungo tumeongea sana juu ya hili tukaishia kukashifiwa na kuambiwa tuna wivu tu wa kijinga !!!!!!!

Hope wahusika wanajipanga ki mkakati zaid sasa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu lusungo tumeongea sana juu ya hili tukaishia kukashifiwa na kuambiwa tuna wivu tu wa kijinga !!!!!!!

Hope wahusika wanajipanga ki mkakati zaid sasa

Hahahah

Mi nikiuliza tunaona wivu wa nini hawasemi.....
 
Last edited by a moderator:
Hivi majuzi tulimsikia mwakilishi wa wanaDiaspora mheshimiwa Kadari Singo, akijitambulisha na kuwasilisha hoja wake kwenye Bunge la Katiba huko Dodoma.

Mheshimiwa Singo ni mtanzania ambae anaishi na kufanya kazi nchini Marekani na ni mmoja wa viongozi wa jumuiya ya watanzania wanaoishi huko Marekani.

Wana Diaspora ni watanzania wanaoishi nje ya nchi hio katika mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika, Asia, Ulaya na Marekani ambao kwa idadi sasa wanafikia milioni 3.

Mheshimiwa Kadari Singo alitoa mada yake juu ya umuhimu wa kuuenzi Muungano wa Tanzania na Zanzibar na pia umuhimu wa watanzania walishio nje kwenye maendeleo ya nchi hiyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Singo alizama kwa kina kwenye umuhimu wa kiuchumi zaidi akitoa takwimu za kiasi cha fedha ambazo zinatumwa kwenda katika katika mataifa mbalimbali ambayo kuna ndugu wa wana Diaspora na kwamba watanzania pia wanashiriki kuchangia uchumi wa nchi yao.

Alisisitiza kwamba watanzania waishio nje ya nchi wanahitaji kuondolewa vikwazo kwenye suala la uraia wao wa kuupata nje kwa kutengenezewa utaratibu wa kurahisishiwa uraia huo ili uende sambamba na uraia wa Tanzania.

Mimi nampongeza mheshimiwa Singo kwa utangulizi wake huo wa hoja ya kutoka kwa wanaDiaspora na kwamba huu ndio uwe mwanzo wa wana Diaspora katika kuimarisha mhimili wetu (platform) wa wana Diaspora na kwa kuwa tumepata pa kusimamia, basi tujijenge hapohapo.

Lakini hatua hii iliofikiwa ya kuweza kufika Dodoma kujitambulisha,isiwe ndio mwisho wa suala zima la malengo ya wanadiaspora. Bado kuna safari ndefu ya kuhakikisha kwamba wana diaspora wanajijengea sifa ya kuwa mfano wa kuigwa kwa watanzania wenzetu wengi waliopo nyumbani Tanzania.

Ndio maana nikasema katika kichwa cha habari kwamba hoja ya wana diaspora isiwe uraia pacha tu, bali kuwepo na masuala mengine kama ushirikishwaji wa wana diaspora katika kupiga kura katika chaguzi zote zinazofanyika nchini humo, uwepo wa kiti cha wana diasapora kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hata kuwepo na wizara kabisa inayoshughulikia masuala yote ya wana Diaspora popote pale walipo.

Pia kuna jambo jingine ambalo tuna budi kuliangalia katika mchakato mzima wa wana Diaspora wa kitanzania, jambo hilo ni kwamba inaonekana kwamba ni wanadiaspora wa Marekani tu ndio walIopo na muda wa kushughulikia suala hili la uraia pacha.

Suala la Diaspora lisiwe ni la watu au makundi ya watu fulanifulani basi liwe ni la kila mtanzaia aishie nje ya Tanzania.

Pamoja na kwamba kuna idara maalum pale Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya dada yetu Susan, idara hiyo ina wajibu wa kuwaunganisha wana diaspora wote waliopo nje ya nchi badala ya kuwashikilia wale wa Marekani tu au Uingereza pekee.

Je, wana diaspora waishio nchini Uingereza uana Diaspora wao umekuwa ni wa jina tu? Ni hivi majuzi tumeshuhudia wana diaspora wa Marekani, Uchina, Nigeria na Uchina wakisheherekea miaka 50 ya Muungano, wana diaspora wa UK wamekaa kimya kwa sababu zipi?

Huu ni wakati sasa wa wana Diapora wote kukusanyika pamoja popote pale tulipo na kuunda taasisi kamili ya wana Diapora ambayo itajumuisha wana Diaspora wote kutoka pande zote za dunia.

Pia taasisi hii ya wana Diaspora haitajihusisha na chama chochote cha siasa na itakuwa ni taasisi inayojitegemea, hivyo kuondolewa kutoka kwenye ofisi ya waziri mkuu.

Taasisi hii itakuwa na ofisi nchini Tanzania na ofisi moja ndani ya Diaspora na ambayo itashughulikia masuala yote muhimu yanayohusu wana Diaspora hasa yakilenga katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi na kijamii.

Nafahamu kwamba kutakuwa na tatizo la "co-ordination" lakini halitakuwa tatizo kama patapatikana wale watu walio na muda tayari kuwa na kazi ya Diaspora tu. Suala la uendeshaji litategemea na uwezo wa kupata vyanzo mbalimbali vya mapato.

Umuhimu wa kuwa na taasisi ya wana Diaspora ni kwamba wana Diaspora hao watakuwa na uwezo wa hata kuwekeza katika moja ya mikoa ya nchini Tanzania na kuufanya mkoa huo uwe mfano wa kuigwa na mikoa mingine hivyo kuwa chachu ya maendeleo.

Siwezi kukataa kwamba idara ya wa Diaspora itakwazwa na kujihusisha kwake na serikali au moja ya vyama vya siasa, lakini ni wajibu wa wana Diaspora kuonyesha tofauti kubwa kati ya uendeshaji wa idara hiyo kwa njia za kisasa zaidi zisizo na ufisadi wala mizengwe na ule uendeshaji wa kitanzania= Tanzania au kitanganyika -Tanganyika.

Nimalizie kwa kusema kwamba, sisi watanzania tuishio katika Diaspora tukumbuke kwamba huko ugenini tunakoishi sio nyumbani kwetu na hata hawa wenyeji sasa wamechoka na wageni. Hasira zao si tu kwamba mahali huko si kwetu bali kwamba sisi tulihamia na sasa tunahamisha fedha kurudisha huko tutokako.

Tangu ushindi wa chama cha Conservative mwaka 2010 tumeshuhudia mabadiliko makubwa kwenye sheria ya Uhamiaji na sasa kuimarika kwa chama kingine cha upinzani cha UKIP cha bwana Farage.

Ingawa bwana Farage anapiga kelele nyingi sana lakini ukweli unabaki kuwa mkewe ni Mjerumani.

Naomba kuwasilisha hoja.
 
Wana diaspora wa India, Philippines, Pakistan na wengi wengineo mimi nimetaja wachache tu.

Hao huwa wanatuma nchini mwao kwa mwezi mamilioni ya ma$s na ni moja katika njia ambazo nchi zao hupata hard currency.

Wana diaspora wa kiTZ kwa mujibu wa uzi unavyosomeka yaani wao wanataka benefits wakiwa kama ni waTZ lakini sioni kama wao wataihudumia nchi kinamna gani. 🎺
 
mleta mada,
wana diaspora wa UK si ni hivi juzi tu Chris Lukosi
alisema wao shida yao kuu ni kupata nafasi ya kupiga picha na wakuu wa tz na sio kutafuta haki ya kutambulika?.au sio hao?.
 
Last edited by a moderator:
Kwasababu Tanzania inasuasua na sheria ya uraia pacha wakati nchi wanachama Kenya, Uganda na Rwanda zikiwa tayari zinatambua Uraia pacha na wananchi wake walio nje ya nchi zao kufurahia, na Kwasababu Tanzania ni mshiriki wa east african community huku ikitambua east african citizenship na passport, Watanzania ambao wanapata ugumu na Tanzania kwasababu wamepata uraia wa nchi zingine ni vyema wakafikiria kuchukua Uraia wa Kenya, Uganda au Rwanda na wataendelea kuishi na kujiendeleza kwenye nchi yeyote ya jumuiya ya afrika mashariki bila bugudha na kukwepa adha ya siasa za nyumbani ambapo Mtanzania huyu ataishi Tanzania kama raia ama wa Kenya, Rwanda, au Uganda huku akiwa amelinda uraia wa nchi nyingine unampa kula na ajira.
 
Kwasababu Tanzania inasuasua na sheria ya uraia pacha wakati nchi wanachama Kenya, Uganda na Rwanda zikiwa tayari zinatambua Uraia pacha na wananchi wake walio nje ya nchi zao kufurahia, na Kwasababu Tanzania ni mshiriki wa east african community huku ikitambua east african citizenship na passport, Watanzania ambao wanapata ugumu na Tanzania kwasababu wamepata uraia wa nchi zingine ni vyema wakafikiria kuchukua Uraia wa Kenya, Uganda au Rwanda na wataendelea kuishi na kujiendeleza kwenye nchi yeyote ya jumuiya ya afrika mashariki bila bugudha na kukwepa adha ya siasa za nyumbani ambapo Mtanzania huyu ataishi Tanzania kama raia ama wa kenya, rwanda, au Uganda huku akiwa amelinda uraia wa nchi nyingine unampa kula na ajira.

Uraia wa nchi mbili kwa mtanzania ni bure, sisi hatuna uzalendo hata kidogo, ubinafsi na ujinga viko mbele sana, nyie mnaokaa nje ndio mnahamasisha suala hilo lakini Tanzania tuna mambo mengi sana muhimu na si uraia pacha, sijui ooo ukiwa na urai pacha utaleta maendeleo nchini mwako thubutu!!!!! mtanzania au nani?. Wakenya wenyewe ndio hao wanaotaka uingereza wahalalishe mirungi ili wao wafanye biashara, ujinga huu wa mwafrika unatupeleka wapi?hivi wamekosa biashara nyingine bali kulazimisha vijana wa uingereza kutunisha misuli ya kichwa kwa kuila mirungi? Naomba tujenge utamaduni wa kujitegemea kimawazo sio kwa kuwa Kenya au Uganda wanatekelza suala hilo la uraia pach basi na sisi tufuate tuuuuuuu, huo ni upuuzi, kwa kweli dual citizenship is not our priority at all!!!!, we have people living in abroad but they have not done anything, instead complaining about luck of dual citizenship as reasons for their not serving the country, you are hopeless people if you reealy wish to contribute for your country's development don't wait for dual citizenship please.
 
Wasiwasi wengi walionao si kweli kabisa, Nchi ya wayahudi Israel imejengwa na inanguvu kubwa duniani kwasababu ya wayahudi zaidi ya 7m waliosambaa duniani.

Nchi ya Singapore imeimarishwa uchumi na diaspora, Nchi ya Ethiopia imefaidika sana na diaspora kiuchumi, Nchi ya Ghana, nk nk. Si kweli kwamba watanzania waliolazimika kufanya kazi nje ya Tanzania sio wazelando, na si kweli kwamba hawasaidii Tanzania msaada wao ni mkubwa kuliko bajeti ya wizara mbili za serikali.

Miaka kumi au ishirini baadaye kutakuw na zaidi ya watanzania 10m duniani wenye biashara, ajira nzuri, elimu, utaalamu nk. Vile viloe kutakuwa na watanzania zaidi ya 4M waliostaafu nje wenye malipo mazuri ya uzeeni wangependa kuja na kuishi nyumbani na kutumia hizi fedha ambazo zitatengeneza ajira zaidi ya 5M.

Ukiangalia leo na sasa na matukio ya kiuchumi mabovu, utawala mbovu, sheria gandamizi na za upendeleo, wizi wa kukimbia nchi na kukimbiza fedha utahisi hakuna faida. Wezi unaowaogopa wewe hawahitaji uraia pacha , wana fedha za kununua uraia popote duniani. Nchi ya marekani ukiwa na zaidi ya $500,000 unapewa ukazi, mwizi wa bot au mhujumu anaweza kuishi popote bila kuhitaji uraia pacha kwani hahitaji ajira ana fedha.

Wazalendo masikini ndio wanahangaika. Hakuna tajiri mwenye haja ya kuishi nchi masikini kama zetu wala kuwekeza kwa kudumu.

Wengi wazawa wa kweli wanapenda nchi zao.
 
Uraia wa nchi mbili kwa mtanzania ni bure, sisi hatuna uzalendo hata kidogo, ubinafsi na ujinga viko mbele sana, nyie mnaokaa nje ndio mnahamasisha suala hilo lakini Tanzania tuna mambo mengi sana muhimu na si uraia pacha, sijui ooo ukiwa na urai pacha utaleta maendeleo nchini mwako thubutu!!!!! mtanzania au nani?. Wakenya wenyewe ndio hao wanaotaka uingereza wahalalishe mirungi ili wao wafanye biashara, ujinga huu wa mwafrika unatupeleka wapi?hivi wamekosa biashara nyingine bali kulazimisha vijana wa uingereza kutunisha misuli ya kichwa kwa kuila mirungi? Naomba tujenge utamaduni wa kujitegemea kimawazo sio kwa kuwa Kenya au Uganda wanatekelza suala hilo la uraia pach basi na sisi tufuate tuuuuuuu, huo ni upuuzi, kwa kweli dual citizenship is not our priority at all!!!!, we have people living in abroad but they have not done anything, instead complaining about luck of dual citizenship as reasons for their not serving the country, you are hopeless people if you reealy wish to contribute for your country's development don't wait for dual citizenship please.
Wewe umechangia nini kuliko mimi niliye nje ya nchi? Suara la uraia wa nchi mbili ni suala la mtu kua proud na nchi anayo toka na kupata haki sitahiki kwa nchi anayoishi na kufanya kazi. Ata tukiishi nje ya nchi miaka 50 bado tutakua watanzania tu sasa kwa nini watunyang'anye uraia kisa kuna mambo mengine ya kufanya. Acheni ubinafsi bana na wewe siku ukipata nafasi ya kufanya kuishi nje ya Tanzania utajua ni kwa nini tunataka uraia wa nchi mbili
 
Back
Top Bottom