Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,577
- 18,774
ndutu
Swala la uraia wa nchi mbili silikatai moja kwa moja nilichosema ni kwamba lazima tuangalie mambo ya msingi kwanza kama kuleta mfumo wa uwajibikaji. Hii ni kuwezesha kudhibiti uwezekano wa watu ambao siyo raia wa Tanzania (wale ambao hawakuwahi kuwa Watanzania) au ambao hawana mapenzi na Tanzania kuiharibu nchi.
Wewe mwenyewe umesema kuwa mafisadi wanauraia wa nchi mbili. Kwani unafiri sijui jinsi wanavyofanya kuingia na pasi ya Tanzania na wakati wa kutoka kupitia Nairobi na kuondokea na Pasi ya nje? Nafahamu ndiyo maana nikasema tuyadhibiti hayo kwanza. Je unafahamu kwa mfano pasi za Marekani zina kuwa tracked na GPS kwahiyo wanajua pasi iko wapi 24-7? Sasa sisi hatuna hata mfumo unao eleweka wa kutunza rekodi za vyeti vya kuzaliwa ndo tukimbilie hayo ya pasi mbili?
Ninapoongelea mfumo wa uwajibikaji nina maanisha sheria kufuata mkondo wake bila ya kuwa na bla bla. Mfano Marekani ukitaka kusajili kampuni unafuata vipengele 1, 2, 3 umemaliza, tena unaweza fanya matandaoni bila tatizo, baada ya muda unaletewa employer identification number (EIN) na IRS bila shida, unaanza kuingiza pesa.
Polisi akikukamata kwa kuendesha kasi anakupa faini (ticket), mwenyewe unakwenda kuilipa mahakamani. Usipofanya hivyo baada ya muda wanakutumia warrant, unaikuta kwenye mail box, usipolipa wanakuja kukugongea au wanakufuata unapofanya kazi. Huo ndio mfumo/utaratibu unaoeleweka. Sasa hebu nia mbie ukitaka kuanzisha kampuni bongo kwamfano utaweza kufanya kwa mlolongo unao eleweka? Si utazungushwa mpaka mwenyewe utoe kitu kidogo.
Unajua Tanzania tuna mifumo mingi mibovu lakini haya ni mambo ya ndani, sasa unapoleta mambo ya uraia wa nchi mbili unazungumzia mambo ya usalama wa Taifa. Kuna uwezekano wa nchi yetu kuingiliwa na wale ambao hawana mapenzi ya kweli na nchi yetu. Sasa hivi haya yanafanyika kama ulivyosema lakini kichini chini tukiruhusu bila ya kuwa na mfumo unaoeleweka itakuwa balaa.
Kwa Watanzania walio nje mimi sioni tatizo mbona wengi wanawekeza TZ bila ya kuwa na uraia wa nchi mbili? Kwa taarifa yako wapo wengi tu waliokataa kuukana uraia wa Tanzania japokuwa wanaweza kufanya hivyo. Mtu anayetaka kuwekeza atawekeza tuu uraia wa nchi mbili siyo kikwazo kwake.

Last edited by a moderator: