Kunyima watu dual citizenship ni kujirudisha nyuma. Hao matajiri wenyewe kina Marekani na Uingereza wanajua umuhimu wa hiki kitu katika biashara ya kimataifa. Mara nyingine tunajifungia milango wenyewe halafu tunalaumu mvua hazinyeshi.
Wahindi kibao wamekuja kufanya kazi/ kusoma US, wameishi, wamechukua uraia, wameona India kuna maendeleo sasa yanayohitaji mchango wao, wamerudi kwao kuendeleza nchi. Wanaipeleka India katika mashindano ya kibiashara kwa benefit zote za raia wa Marekani.
Dual Citizenship ni kama vyama vingi vya siasa, ni trend ambayo utake usitake inakuja, sasa uamuzi ni wetu kama tunaamua kuikubali leo ili tupate a leg up on it's advantages au tuikubali miaka 50 ijayo wakati wenzetu hawaongelei dual citizenship tena, bali washachafua dunia wanataka kuikimbia waende kuhamia sayari nyingine.
Wakati sie tutakuwa tumebanana Kisarawe kwa kuwa hatutaki raia wawe na dual citizenship.
Hii habari ya kuwaminyia watu dual citizenship haina tofauti na ile habari ya kukataza watu kusafiri na kuwa na passport, baadaye tutakuja kuangalia nyuma na kusema "duh, hapa tuliboogie step sana" kama hatutaikubali.
Huwezi kuniambuia mei leo nije kuwekeza Tanzania kwa terms za foreigner eti kwa sababu nimechukua uraia wa Marekani. Na Marekani kuna mi ofshore investment siwezi kui explore kama naishi kwa green card.
Kwa hiyo hiyo dual citizenship ikija poa, isipokuja napo poa vile vile, tutakuja kwa visa tu au kuchukua permanent residency ya huko.