Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

Swala ni Membe kutaka GF wake awe huru Tanzania na California pia. Swala la waaekazaji wazawa ni janja tu wa waziri kupitia hapa kwa masilahi binafsi.

Kwa sisi wengine tungependa kujuwa kuwa mtu akiwa na uraia wa nchi mbili anakuwa analeta hasara gani wala sio suwala la Umembe au nani? Membe ataondoka lakini hali hii ya Watanzania kunyimwa haki yao itaendelea mpaka lini?
 
MwanaFalsafa1

Kaka! Hivyo unafikiri kila kilichopitishwa hapo mwanzo kilikuwa sahihi? Kama ni hivyo basi tusingedai Katiba mpya!
Hivyo unafikiri ni sahihi kumnyanganya uraia wa kuzaliwa mtu eti kwa kuangalia maslahi? Yaani unafikiri ni dhambi mtu kupata sifa ya kuweza kuendesha maisha yake akiwa nje ya nchi yake? Hii ndiyo inayowalazimisha Watanzania wachukuwe uraia wa nchi nyengine ili wapate sifa ya kuwafanya wapate masilahi ndani ya nchi ya ugenini. Sasa iwapo wenyeji wa nchi ile hawajali wewe kubaki na uraia wa nchi yako uliyozaliwa inakuwa kichekesho kuwa wewe uliemzaa unasema huyu si mwanangu.

Hili suwala la mtu kuukana uraia wa Tanzania limewekwa katika Katiba kimakosa kama mambo mengi yaliyowekwa huko nyuma na tuikaamuwa kuyabadilisha kwa maslaha yetu. Huko nyuma ilikuwa sheria mtu asifanye kazi zaidi ya moja kujitafutia riziki, asipangishe nyumba yake na sheria chungu nzima zisizo na tija kwa mwananchi.

Hili la kumkataa raia wa Tanzania eti kwa kuangalia maslahi si sahihi halafu Kaka unasema eti mtu huyu awe na moyo wa kuekeza kwao na huku umemkataa? Nafikiri ipo haja ya kutafakari na kuondokana na ukungu tuliotandaziwa na siasa za Kijamaa.
 
Last edited by a moderator:
Kwani akiwa nao utamfanya asifanye hayo anayotaka kufanya? Pengine ungetwambia hasara za kuwa nao!

Mkuu mimi sija kataa kuwa na uraia wa nchi mbili. Ila napima hasara na faida zake. Ili kuonyesha faida zake ni lazima mtu aorideshe faida za kuwa na uraia wa nchi mbili. Huyo niliyemquote alilist yeye anazo ona ni faida za dual citizenship. Mimi nimemuuliza swali rahisi tu kwamba hivyo alivyo viorodhesha haviwezi kufanyika bila dual citizenship? Sasa mimi swali sija jibiwa tayari naulizwa swali? Tukifanya hivyo we will be going in circles. Mimi sijakataa faida zake nimeomba tu kuambiwa ni vitu gani mtu anaweza akafanya na dual citizenship chenye manufaa kwa taifa ambacho hawezi kufanya bila hiyo dual citizenship.
 
Mkuu Ngekewa,


Sheria za nchi lazima ziangalia interest za taifa kiujumla. Huwezi sema sheria ianzishwa ilimradi tu kumridisha mtu. Kwa hiyo napingana na wewe la hili la kuanzisha katiba eti bila kuangalia maslahi. Kwa hiyo unataka kusema mkuu kwenye sheria zetu tusiwe tunaangalia tena maslahi ya taifa bali tuweke tu sheria? Hili silielewi kabisa. Unless ufafanue mkuu una maanisha nini ukisema si lazima kuangalia maslahi.


Mkuu sasa una nichanganya. Hapo juu ulisema tusimnyime mtu kisa maslahi. Sasa hapa unaongelea maslahi. Which is which?

Hili la kumkataa raia wa Tanzania eti kwa kuangalia maslahi si sahihi halafu Kaka unasema eti mtu huyu awe na moyo wa kuekeza kwao na huku umemkataa? Nafikiri ipo haja ya kutafakari na kuondokana na ukungu tuliotandaziwa na siasa za Kijamaa.

Mkuu hapa nani kamtakaa nani inategemea unaangalia kwa upande gani. Kwa upande mwingine unaweza ukasema mtu huyu kaikataa Tanzania kwa kuamua kuchukua uraia wa nchi nyingine. So it depends how you look at it.
 
Mkuu Kiranga,

Nakubaliana na baadhi ya points zako ila mimi nina swali. Samahani lakini nataka tu kujua zaidi faida ya dual cizitzenship. Je mtu kuwa na dual citizenship kuta guarantee wao kuwekeza nyumbani? Je ni majority gani ya Watanzania waliopo nje wana uwezo wa kuja kuwekeza nyumbani? Wataletauwekezaji wa aina gani? Nadhani haya ni maswali muhimu kujiuliza na kujaribu kupata majibu badala ya kuassume tu kwamba kuwa na dual citizenship kuta maanisha kuongezeka kwa uwekezaji.

Sipingani na dual citizenship lakini pia kwa sasa sikubaliana nao moja kwa moja. Ndiyo maana hapa nauliza maswali mengi ili nielewe na nijifunze zaidi. Kwa bahati mbaya so far watu wengi wanajibu kwa kutumia hisia badala ya kuorodhesha ni nini kweli kinaweza kufanyika kwa maslahi ya taifa na hiyo dual citizenship ambacho hakiwezi fanyika sasa. Maana wengi wanaongea kana kwamba ukiruhusu hiyo dual citizenship tu basi uwekezaji utaongezeka maradufu.
 
Reactions: Nzi
Mjomba, India hairuhusu Dual Citizenship na Wahindi waliochukua Uraia Marekani hawana lao India.

Overseas Citizens of India:

  • You do not get Indian passport.
  • No voting rights.
  • Can not be candidate for Lok Sabha/Rajya Sabha/Legislative Assembly/Council
  • Can not hold constitutional posts such as President, Vice President, Judge of Supreme Court/High Court etc.
  • Cannot normally hold employment in the Government.
Source: KATIBA YA INDIA, na taarifa ya Ubalozi inayowatahadharisha Wahindi wabobezi kwamba mkiondoka imekula kwenu: Dual Nationality | Embassy of the United States New Delhi, India
 

Kusafiri bila kuhangaika na mambo ya kwenda kuomba visa. Uraia wa nchi mbili utapunguza kero ya msafiri baina ya hizo nchi mbili (mojawapo kati ya hizo ikiwa ni Tanzania) kwa kuepuka hicho kizingiti cha kuomba visa. Hii siyo faida?

Uraia wa nchi mbili utawapa Watanzania fursa ya UHURU wa kuwa raia wa nchi zingine ambazo hazina tatizo na wao kuwa raia wa nchi hizo. Kumbuka, uraia wa kupewa kwa sehemu nyingi unakuja na masharti na vivyo hivyo itakuwa vyema na sisi tukaambatanisha masharti yaendanayo na uamuzi wa namna hiyo.

Kwa mfano, mtu akiamua kuwa raia wa Canada basi atapoteza baadhi ya haki na fadhila zinazoambatana na uraia wa kuzaliwa. Tunaweza tukatunga sheria inayotamka kuwa Mtanzania yeyote anayeamua kuchukua uraia wa kwingine atapoteza haki yake ya kuwa mwanajeshi, jaji, au nafasi kadha wa kadha za kiuongozi za kuchaguliwa n.k.

Sasa bwana Mwanafalsafa huoni kwamba uraia wa nchi mbili utapanua wigo wa uhuru - uhuru wa kuamua kwenda kutafuta maisha kwingineko ambako wanakaribishwa bila hofu ya kupoteza uraia wao wa kuzaliwa?

Vilevile, uraia wa nchi mbili utawasaidia watu kwa kuongeza milango ya fursa huko walikoenda kutafuta maisha. Kuna baadhi ya kazi mtu ukiwa kwenye nchi za watu huwezi kuzipata hadi uwe raia. Sasa wapo watu ambao wanashindwa kuzipata kazi hizi si kwa sababu hawana sifa bali wanaogopa/ wanasita kuchukua uraia wa hizo nchi walizopo kwa sababu wanahofia kupoteza uraia wao wa kuzaliwa. Hii wewe kwako si faida? Au unadhani watu wakipata kazi kama hizi wala hawatakumbuka kwao walikotoka?

Pia, hakuna sababu yoyote ya msingi ya mtu, tena mtu ambaye ni raia mwema na mtiifu, kupoteza uraia wake wa kuzaliwa kwa sababu tu eti kachukua uraia wa nchi nyingine. Hakuna mtu mwenye haki ya kumnyang'anya raia mwema na mtiifu uraia wake wa kuzaliwa.

Watanzania wakati umefika wa sisi kwenda na wakati. Cha muhimu ni kwenda na huo wakati kwa kutumia hekima na busara na kujifunza kutoka kwenye makosa ya wengine. Ugumu uko wapi hapo?
 
Ni kakundi kadogo mno ka wa tz wenye acces na izo faida za uraia wa nchi nyingi,mnaposema kusafiri, ni wa-tz wangapi wanaoshindwa kusafiri hata nje ya mikoa yao walozaliwa?
 
jamani watanzania tusiwe wagumu kukubali maendeleo, yameshatokea na tusipoendana na hali halisi tutapata hasara. Katika enzi hizi uraia wa nchi 2 ni muhimu sana. Watanzania wote walioko nje wako kimasomo au kikazi kwa sababu kuna maslahi zaidi. Pesa wanazopata huko wakiituma nchini hua ni kubwa sana na inawezafanya vitu vikubwa mfano dola ikiwa us ni ndogo lkn ikitumwa tz ni kubwa. Watanzania hufanya kazi nje lkn wanatuma pesa kuendeleza nyumbani. Kuwanyima huu uraia ni kuwanyima haki ya msingi na kunarudisha nyuma maendeleo
 
Mimi binafsi ni raia wa Tanzania na ninaishi Tanzania! Nimekuwa nikijiuliza swali hili mara nyingi sana maana mimi si kama hao wanaotaja USA, Canada, Brazil, India Singapore na Mexico kama mifano michache ya uraia wa nchi mbili na kutuhamasisha na sisi tuige huko. Naamini sisi kama nchi tuna mifumo yetu (ambayo pia huendana na wakati), sasa tunatakiwa tuitazame, tuifanyie utafiti wa kina kweli kweli kisha tuzungumze sio kutaja tu mifano! Tofauti zetu na hao ni nyingi mno sio kuwaiga tu!

Masuala yanayotajwa kama faida ya dual citizenship hayana msingi wowote zaidi ya manufaa binafsi kwa wanaoulilia: kwa mfano mtu anasema anakosa sifa ya kugombea uongozi!!!! Sasa wenzangu jamani mtu amezaliwa ughaibuni, amekulia huko, amesomea huko, ameoa/kuolewa huko na ana uraia wa huko miaka yoote hii, leo tunahitaji Mbunge ndo anakuja Waooh! hii ni kashfa kabisa, tena ni matusi, anaelewa nini huyu kuhusu sisi?? Wengine wanadai wawe na haki ya kupiga kura nchi zote mbili! hii ni commedy kabisa.

Wawekezaji: Naomba msaada kwa hili sina data, sijawahi kusikia mwekezaji wa MAANA mtanzania anaetamba kweli kweli kiasi cha kuhitaji kuja kuwekeza hapa na akakosa nafasi ukiacha hawa wakwetu hapa tunaowafahamu. Sana sana watakwambia wanatuma pesa nyingi sana huku, wapi Bwana kumtumia pesa za matumizi mzazi wako ndo tukuite mwekezaji na kukupa dual citizenship? HAPANA!

Kwa kumalizia: Kuna mchangiaji mmoja kasema huduma za afya ni bora zaidi huko ughaibuni kuliko hapa kwetu! Sielewi ni nani aliziboresha huko aliko na yeye anazitumia tu (kama kupe) hana wazo wala mpango ni namna gani za nyumbani zitaboreshwa na anafikiria kuwapeleka hata wazazi wake wakatibiwe huko! na sie tusioweza kufika huko ndo tufe tu au ulikuwa una maana gani? Kimsingi hili suala halina MASHIKO ya jumla zaidi ya mtu mmoja mmoja na halina tija kwa taifa mpaka usawa huu.
 
Reactions: Nzi

Nyekundu: Ndugu yangu, kwa taratibu za Tanzania, kama ukishachukua passport ya nchi nyingine, automatically unakua umeukana utanzania, kwa sababu sheria haziruhusu mtu kuwa na passport ya nchi nyingine!! Hivyo si lazima kuwe na kipengele kwenye izo application procedures za nchi nyingine ndio ionekane umeukana utanzania.

Kjanii: I don't see any national interests kwenye hayo maelezo yako. Yote uliyoyaeleza yanalenga katika kufaidika wewe binafsi na familia yako!! So still naamini dual citizanshep has no national benefits.

Bluu: Kama ndio hivyo kwanini hujiangaishe kuchukua uraia wa nchi nyingine wakati bado unatamani kupata privileges za kuwa mtanzania?!?! Hapa inajidhihirisha ulivyo mbinafsi!

Njano: Ndugu yangu ingawa tunaishi katika globalised world, lakini nchi kama nchi haiwezi kua inafanya kila jambo kwavile taifa fulani linafanya. Suala la dual citizenship lazima lijadiliwe kwa kina na watanzania (kupitia a national debate) ili sisi kama watanzania tuweze kujirisha kwamba suala hilo lina faida nyingi kwa taifa kuliko faida nyingi kwa mtu binafsi. Sisi watanzania tunapenda kufananisha nchi yetu na yanatokea katika nchi zingine kwa mambo binafsi, lakini mambo ya faida kwa taifa wala. Mfano, wewe unaishi Marekani, kwanini uishauri serikali ya Tanzania itumie mfumo wa IRS katika ukusanyi wa kodi na kudhibiti money laundering na watu kutajirika bila concrete financial bases?

Nyeusi: Hapa unaendeleza kuelezea juu ya personal benefits.

Zambarua: Ndugu yangu, naona kuishi nje kumekufanya usahau hali ilivyo hapa. Kwa serikali hii ya CCM hayo uliyazungumza ni vigumu kuyaepuka. Hujasikia jinsi raia wa kigeni siku hizi wanavyojichukulia ardhi utafikiri ya kwao? Hivyo uoga wa waTZ katika suala la ardhi ni genuine kutokana na hali ilivyo sasa. Pia kama hao unaowaita watanzania walio nje wangechukua ardhi wakati ni watanzania, mimi sina shida katika hilo. Kuhusu wizi wa pesa, bado suala la mfumo mbovu uliopo sasa hautaweza kudhibiti suala hilo. Kuhusu pesa nyingi kutoka kwa hao watanzania walio nje, sidhani kama una takwimu sawa, kwanza unafahamu idadi yao? Pia pesa wangeweza kuleta nyumbani hata kama wangekua hawana passport za nchi nyingine. Mfano ,takwimu zinaonyesha kua wakenya, wanaigeria na waghana walio nje ni kati ya mataifa ya Afrika yanayoongoza katika remittances; na hao sio wenye uraia wa nchi mbili tu!!

Damu ya mzee: hizo dharau sasa. Umesahau tuna kila aina ya maliasili hapa? Kwanini ujiulizi juu ya ujio wa wazungu na makampuni yao hapa? Wanafuata nini? Hao si umeshasema wanafuata maisha bora!! Hivyo wanakimbilia mambo yao binafsi.

Bluu mpauko: Mimi binafsi simchukii mtu yeyote alieenda kutafuta maslahi mazuri, ninachochukia na suala la wao kushinikiza uwepo wa dual citizenship ili waendelee kufaidi maslahi mazuri ambayo kama taifa halifaidiki kwa kiasi kikubwa!

Asante.


 

Hayo yote uliyoyataja huwezi kuyafanya ukiendelea kua na passport ya Tanzania ukiwa nje? Yaani kufanya yote hayo ni mpaka uwe na dual citizenship?! Si kweli!
 

Nyekundu: ndugu, huyo sidhani kama ataitwa mtanzania tena..ndie maana alihitajika kupata visa kwanza. Angekua mtanzania hasingepaswa kuomba visa.

Bluu: ndugu, unataka kumaanisha kote walipotapakaa hao kuna dual citizenship???!? Mbona wachina wapo kibao hapa Bongo na wamewekeza lakini hakuna dual citizenship?!

Kijani: ndio maana nimeomba msaada wa kupata faida za suala hilo kwa taifa. Basi kama mtu unaeona kua suala hilo lina faida kwa taifa, ebu nifafanulie juu ya faida hizo.

Njano: sijui. Ebu nipatie takwimu hizo.

Asante
 

​That is what I am talking about.
 

Vyema. Niorodheshee faida na hasara za dual citizenship ili niweze kuchuja pumba na mchele.
 

What you have said can be done without dual citizenship!! Still I am asking, what is so special about dual citizenship?!
 

Hayo yote unayosema bado hayahitaji dual citizenship!!
 
Kwa sisi wengine tungependa kujuwa kuwa mtu akiwa na uraia wa nchi mbili anakuwa analeta hasara gani wala sio suwala la Umembe au nani? Membe ataondoka lakini hali hii ya Watanzania kunyimwa haki yao itaendelea mpaka lini?

Pengine donge limekupofuwa!


Faida kwa taifa je?! Maana umeorodhesha faida kwa mtu binafsi tu!!
 

Hayo yote yanawezekana bila ya kua na dual citizenship​!!
 
Kuna wapinzani na watetezi wa hoja ya uraia wa nchi mbili. Watetezi wa uraia wa nchi mbili wapo Benard Membe na wengineo wengi ambao viongozi wa serikali. Hoja yao kubwa ni kwamba tukiruhusu uraia wa hoja mbili watz walioko nje watawekeza nyumbani nasi tutainua uchumi wetu. Vile vile kuna suala la kuvutia wawekezaji wengi zaidi hasa wale ambao watawekeza kwa kujiamini kutokana na kupata uraia.

Hawana hoja nyingi sana.Wapinzani wa uraia wa nchi mbili wanadai kwamba, tukiruhusu tutawapa mafisadi mwanya wa kutokamatika maana akifanya ufisadi ktk nchi yetu anakimbia nchi nyingine( Rostam?) ambayo yeye anauraia nao pia. Pia wanadai huu upopo utapunguza uzalendo kwa sababu mtu mmoja hawezi kupenda nchi mbili kwa wakati mmoja.

Vile vile wanadai kuwa kutokana na umaskini wetu wenye hela hasa nchi za magharibi wanaweza kumweka mtu yeyote madarakani kupitia mamluki wao ambao watakuwa wamepewa uraia hapa kwetu Tanzania. Zaidi sana pengo kati ya maskini na tajiri zitaongezeka sana. Kwa kuwa matajiri toka nje ( wakipata uraia) watakuja kufanya biashara wakishirikiana na matajiri watz wachache.

Binafsi niko pagumu kuamua ni jambo gani la kuunga mkono na lipi la kupinga. Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…