Uraibu (addiction)

Uraibu (addiction)

samkarume

Member
Joined
Feb 27, 2009
Posts
59
Reaction score
37
URAIBU (ADDICTION)
Ni ugonjwa wa kimwili kiakili na kiimani ambao huathiri nyanja zote za maisha yetu, Ugonjwa huu unaweza kuwa ni wa kurithi, wa kupandikiza au hujitokeza na kukua kwa sababu za mazigira ya kijamii na kiuchumi

Aina za Uraibu
1. Kuna uraibu wa vitu kama vile Pombe, Madawa, Gundi, Tumbaku, Mirungi, Ugoro,Chakula, Fedha nk
2. uraibu wa shughuli/Tabia kama vile kazi, kamari, ngono, mazoezi, Kununua au kutumia hela, kufanya makosa ya jinai, Kuangalia TV, kutumia mitandao ya kijamii nk
3. kuna uraibu wa fikra ambao ni kujiona sahihi, kuktaa kukosolewa, woga, kuangazia,
4. Uraibu wa Hisia ambao ni Wivu, Hasira, chuki, hofunk
5. uraibu wa watu ambao ni kimapenzi, mahusiano, marafiki, makundi nk
Tafiti zinaonesha kuna aina zaidi ya 40 za uraibu

Madhara ya Uraibu
Endapo uraibu anakuwa hai (Active addiction) madhara yafuatayo yanaweza kujitokeza
kushindwa kufikiri kwa usahihi, msongo wa mawazo, kuchanganyikiwa, kukosa usingizi, kutumia fedha nyingi, kuacha au kuachwa na mpenzi mke au mume, kushindwa kula, kupoteza hamu ya tendo la ndoa, wizi na udokozi, jinai, ugomvi, vurugu, kushindwa kumiliki na kuishia kama watu wengine wanavyoishi, na mwisho wake huwa ni kufungwa jela, au kwenda kuta misaada ya madaktari wa afya ya akili na kufa

Nitajuaje kama mimi ni Mrabu
Dalili kubwa ya kwanza ni
Kuangazia (Obsessive behaviour) Endapo kuna vitu, watu, sehemu, au jambo ninaliwaza sana na nashindwa jinsi ya kufikia lengo hilo inaweza kuwa ni dalili mojawapo

Kulazimisha mambo ay matendo ili kufikia lengo, Ninaposhindwa kuchukuliana na jamabo la kawaida na kulamisha nifanye ninavyotaka mimi na kunisababishia maumivi ya akili mwali na nafsi pia ni dalili ya kuwa na maradhi ya kiraibu

Ubinafsi, endapo ninaharibikiwa na kila ninapoelezwa ninakataa ukweli kwamba nina tatizo mfano kuangalia mpira juda mrefu, kuchelewa kurudi nyumbani, kunywa pombe kupita kiasi na kutumia dawa za usingizi au za kulevya kama sehemu ya maisha yangu pia ianaweza kuwa ni dalili ya maradhi ya kiraibu

kushindwa kumili utumiaji wangu kama vile ngono, ulevi, kazi, fedha nakadhalia

Je nifanye Nini ili nijijue sasa lkwamba nimeathirika

Tunaweza kuwasiliana kwa simu
+255 713 806 726
 
Back
Top Bottom