SoC01 Uraibu wa Ngono

SoC01 Uraibu wa Ngono

Stories of Change - 2021 Competition

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Uraibu upo wa aina nyingi. Kuna uraibu wa pombe, sigara, madawa ya kulevya, na uraibu wa chakula. Leo nitajikita kwenye uraibu wa ngono.

Tofauti na uraibu wa pombe, sigara na madawa ya kulevya ambazo hazimpati yeyote, (sio kila mtu atangukia kwenye raibu hizi) uraibu wa chakula na ngono ni rahisi kumpata mtu yeyote, kwa sababu miili yetu kibayolojia imeumbwa kuhitaji vitu hivi. Uraibu huu ukiongezea na uraibu wa video za ngono za mtandaoni (nitaongelea siku nyingine) inawaharibu kabisa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa na kuhatarisha mustakabali wetu.

Dalili za uraibu huu ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi kwa wakati mmoja. Iwe mwanaume au mwanamke, kama muda wote unawaza kufanya ngono na huwezi kujizuia basi jua kwamba una shida mahali. Kama unatumia muda mwingi sana kupita na kuzunguka kwenye maeneo ambayo unajua utakutana na watu wa kulala nao au unatumia pesa nyingi kupita uwezo wako ili upate ngono basi una shida.

Kama upo tayari kufanya chochote na lolote ili kukidhi kiu yako ya ngono, bila kujali kama unavunja sheria, unaumiza watu au unajiweka katika mazingira hatarishi una shida. Kama huoni binadamu wana utu ila ni wakulala nao tu basi kuna shida. Kama upo tayari kuvumilia kudhalilishwa na kujidhalilisha ili upate ngono, kuna shida.

Je, nini kinasababisha uraibu wa ngono? Kuna sababu nyingi lakini wataalamu wengi wanakubaliana kwamba haya ni matokeo ya kudhalilishwa kingono utotoni. Kuna wanaopapaswa sehemu za siri na wafanyakazi wa ndani. Kuna wanaoambiwa na wafanyakazi wa ndani wawapapase sehemu zao za siri. Wengine wanadai walifanya mapenzi na watu wazima walivyokuwa watoto (kwa wanaume hii ni sifa). Kuna wengine wanabakwa na ndugu jamaa, marafiki na watu wa dini. Kuna wanaoadhibiwa kwa kupigwa sehemu za siri.

Kuna wanao angalia picha na video za ngono tangia wakiwa wadogo. Chochote unachomfanyia mtoto akiwa mdogo ndicho kitakaa naye mpaka atakapoingia kaburini. Rejea uzi wangu kuhusu elimu kwa watoto wadogo . Unapomzoesha mtoto mambo ya ngono unamwekea akilini kwamba upendo na mahusiano ni ngono. Binadamu tunahitaji kuwa na mahusiano mazuri na binadamu wenzetu kusaidiana na kupeana moyo. Watu wengi ni wapweke na wanafikiri kwamba ngono ndio namna ya kuondokana na upweke.

Sababu nyingine ni jamii yetu. Tangia tukiwa wadogo tunaambiwa kwamba mwanaume kazi yake ni kutafuta ngono na mwanamke kazi yake ni kuwa chombo cha ngono. Kama wewe ni mwanaume na hufanyi mapenzi muda wote au haupo mawindoni muda wote basi unaonekana una walakini kwenye maumbile yako. Kama huna wanawake wengi kwa wakati mmoja au kama haupo tayari kufanya mapenzi na mwanamke yeyote atakayekutaka basi unakuwa kituko. Utaambiwa ndio bayolojia ya mwanaume ilivyo na muda wote anahitaji kutulizwa hamu.

Kitu ambacho siyo kweli na mara nyingi mwanaume huyu anahitaji mtu wa kumsikiliza na mtu atakayeweza kumwamini ili amtegemee. Mwanamke kama hujakaa kimvuto wa kingono unaowatamanisha wanaume basi wewe thamani yako inashuka kwenye jamii. Kama ukimtega mwanaume na hajategeka basi kama mwanamke umefeli. Kama hutamaniki huna mantiki ya kuishi. Hapa inaonyesha ya kwamba hata kama mtu alikuwa asiwe mraibu wa ngono atakuwa tu kwa sababu ndivyo jamii inavyomtaka awe.

Lakini cha kuchekesha ni kwamba jamii hiyohiyo inayokutaka uwe kiumbe cha ngono muda wote inataka pia usifanye ngono. Hizi ni jumbe mbili kinzani. Ngono inafanywa kama vile ni dhambi kubwa mno na hata hisia za kufanya ni udhaifu wako wakutenda dhambi. Hii ni sababu inayopelekea watu wa dini mara nyingi kuwa waraibu wa ngono. Wanafahamu kwamba wana shida na katika harakati za kutatua shida hiyo wanafikiri kwamba wakishika sana dini na wakijinyima kabisa kufanya ngono watakuwa amejitibu.

Wanafikiri kwamba uraibu wa ngono ni udhaifu wao na wanatakiwa kuushinda kwa namna yeyote ile, kitu ambacho si kweli. Ukijinyima sana kufanya kitu basi ndio utakuwa unakiwaza muda wote. Mtu ambaye yupo kwenye diet atawaza chakula muda wote. Hii inapelekea kusikia kesi za mapadre kulawiti watoto au viongozi wa dini kuishi maisha ya aina mbili. Mchana anahubiri, usiku ananunua machangudoa au anatembea na waumini.

Madhara ya uraibu wa ngono ni mkubwa mno. Achilia mambo ya magonjwa ya zinaa yasiyo na tiba kama UKIMWI na Kaswende (haya pia ni majanga). Mzazi ambaye ana uraibu wa kutembea na watoto atawaambukiza na wao wawe na uraibu wa kutembea na watoto wao. Na kuna uwezekano mkubwa huyo mzazi alifanyiwa hivyo na wazazi wake. Hata kama mzazi hatembei na mtoto lakini kuna uwezekano mkubwa mtoto huyo akarithi tabia hizo, yaani na yeye akawa mraibu wa ngono. Kiufupi vizazi vinaharibika.

Uraibu wa ngono unasababisha watu wabake, watembee na watoto wachanga, wanyama na tabia nyinginezo ambazo zinatisha. Watu hawa wanahatarisha maisha ya watu wanaowazunguka. Pia uraibu huu unakulevya kama madawa, muda wote unakuwa kama ndio umetoka kuamka. Huwazi kufanya chochote cha maana na unawaza ngono tu. Mahusiano ya familia na wanaokuzunguka yanazorota, unakuwa mtu wa siri sana. Kibaya pia ni matatizo ya kisaikolojia. Ngono haiwezi kutatua maumivu tuliyoyapata tukiwa wadogo na kuendelea kufanya ngono kupita kiasi kunazidisha matatizo.

Watu hawa hufanya binadamu wenzio kama vyombo vya starehe na wapo tayari kuwafanyisha vitendo vya kiudhalilishaji ili kutimiza haja zao, kama vile kulazimisha kuingia au kuingiliwa kinyume cha maumbile. Au matendo ambayo sio za kawaida. Kifo cha mende kwake ni ushamba.

Je, nini kifanyike? Kutibu uraibu wa ngono sio kitu kirahisi. Kuna mwanamke anafikiri kufanya mapenzi muda wote na mumewe kutamsaidia aridhike na asichepuke. Hii ni imani potofu. Huwezi kumsaidia mraibu wa madawa kwa kumpa madawa kila anapotaka. Au kwamba kujinyima kabisa ndio suluhisho hapana. Pia kutunza siri ya uraibu huu hasa kwenye familia hakumsaidii mraibu na wanaomzunguka. Kutunza siri kunaendeleza hii laana na kuangamiza vizazi hadi vizazi. Ni bora afungwe jela asidhuru mtu tena. Na akiwa huko apate tiba.

Mtu mwenye uraibu wa ngono anatakiwa apate ushauri wa kisaikolojia. Kwa hapa Tanzania ni ngumu kidogo kwa sababu hospitali iliyobobea kwenye mambo ya akili ni moja tu ambayo ni Mirembe. Kwa sababu hiyo basi inabidi watu wenye haya matatizo watengeneze makundi yakupeana moyo. Makundi ya kuongea na kusikilizana.

Hii ni tiba inayotoa unafuu mkubwa sana na kuwapa waraibu matumaini. Hata asasi zinazoshughulika na uraibu wa madawa na pombe zinaweza kupokea pia waraibu wa ngono (hatua za kutibu raibu zote zinafanana). Inabidi muhathirika atambue sababu ya uraibu wake. Atafanya hivi kwa kupata tiba ya muda mrefu ya ushauri nasaa. Serikali iwekeze sana kwenye miundombinu ya magonjwa ya akili hasa katika kuongeza wataalamu wa saikolojia ili waweze kutibu watu ambao kwa nje wanaonekana wapo sawa na si mpaka wawehuke ndio wapate msaada.

Wazazi na walezi jamani, tunzeni watoto wenu. Usimuache mtoto akalale kwa ndugu au jamaa, usiogope kuambiwa unadekeza mtoto, au unamficha mwanao. Tuwapende watoto na tuwasikilize ili waweze kuwatengeneza mawazo mazuri ya mahusiano na binadamu wenzio waepukane na upweke. Watu wengi ni wapweke na upweke hata siku moja hautatatuliwa kwa kufanya ngono. Mwisho kila mtu kwa imani yake na kwa Mungu wake asali sana, na amini kwamba Mungu anampenda na atamsamehe kwa makosa yake hata kama ni makubwa kiasi gani.

Kitabu cha Out of the Shadows: Understanding Sexual Addiction kilichoandikwa na Patrick Carnes Ph.D kinatoa maelezo ya undani na ya ziada kuhusu uraibu wa ngono.
 
Upvote 39
Mkuu mimi nilipokuwa mdogo sikuwahi kabisa kujihusisha na haya mambo nilijizuia sana hadi nikamaliza kusoma na kuanza kufanya kazi.
Sasa nilipoanza kuzishika pesa ndio kama nimefungulia bomba na sasa hivi nimekuwa mraibu wa hii kitu.
Yaani kila mwanamke anayekatiza mbele yangu namtamani na nikiwa na pesa huwa napata kiburi fulani na kujiamini kunakuja automatic so huwa naamini mwanamke yeyote nikimtaka nampata hata bila kumtongoza.
Nikajikuta nimedate na wanawake wa kila aina,kila rika hata awe ni wa geti kali vipi,hata awe mke wa nani nikimtaka nampata na nimejikuta nimekuwa mzoefu wa saikolojia za wanawake bila kufundishwa.
Na hii hali imenifanya hata nisione umuhimu wa mke japo natamani kujenga familia.
Hii hali unaiongeleaje mkuu?na nitaiepuka vipi?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Hii kitu ni common kwa watu wengi asee, hata usiyemtarajia au unayemuheshimu sana unaweza kukuta faraghani mwake ana maswahibu haya,
its like we are fighting demons.

Kwa mimi ishanitokea hii kitu mara tu nilipoanza kufanya hii mambo ya wakubwa nikiwa form 2, baada ya hapo I never stop thinking about TO to the extent ikawa kama inaniendesha. Nikatafuta njia mbadala kutokana na uwoga wa magonjwa ya zinaa nikajiunga chama la wana mchawi soap 😀
bila kujua huko nako nilikuwa napalilia tatizo lingine ambalo baadae nilikuja kugundua lina unafuu wa madhara la sivyo ngono zembe ingenipoteza mapema, wengi wanadai masterbation inapunguza nguvu ila kwangu sijawahi kukutana na hilo tatizo, madhara ninayoweza kuyakiri ni ya kisaikolojia kama vile kutokuwa na hisia na wanawake really tofauti na character wako wa masterbation na kuwa muoga kutongoza au kutokuwa na mazoea na wanawake kiujumla.

Kwa mtazamo wangu tatizo lipo hapa, jamii yetu ya sasa imelifanya tendo hili kuwa kama ni tendo la siri sanasana kwa watoto, na wanapoanza kukua wanakutana na vitisho vingi sana magonjwa, dhambi, mimba na vitu kama hivyo.
Pale atakapogundua vitisho hivyo vinaepukika au atakapokuwa haogopi tena vitisho hivyo ndio tatizo linapoanziaga, ni vyema kuwaelimisha watoto waone ni kitu natural ila kinahitaji ufike rika fulani ndio ufanye.

Ila suluhisho nikuoa asee au kuishi na mwanamke hii inamaliza tatizo kabisa labda uwe unajiendekeza
Ahsante. Lakini suluhisho siyo kuoa ndugu. Wapo watu ninaowafahamu walioamua kuoa au kuolewa kwa Sababu ya kukidhi matamanio ya Ngono.. Ila baada ya kuoa Hali Yao ni mbaya mno kuliko hata mwanzo na inapelekea migogoro mikubwa Sana katika mahusiano..

Mwanadamu ameumbiwa kitu kinachoitwa KUKINAI.. hivyo kama mtu alioa au kuolewa kwa kukidhi hamu ya Ngono. Itafika muda atamkinai huyo aliyeoa au kuolewa naye ataamua kubadili ladha kwa mtu mwingine ili kukidhi matamanio, hapo ndo shida huwa Kubwa zaidi.. Hili tatizo ni Kubwa mno kuliko watu wanavyolichukulia..

Kilichonisaidia Mimi ni Kuwa busy, yaani kufanya kazi kupitiliza na kuuchosha mwili kiasi kwamba ninaporudi nyumbani Sina hamu ya Ngono nahitaji kupumzika, Asubuhi nafanya mazoezi Sana, nikirudi naoga maji ya Baridi na kuanza mizunguko ya maisha, na nikipata Muda wa kupumzika najitenga na Simu yangu na kusoma vitabu hasa vya neno la Mungu Hasa Biblia.. Naweza maliza hata mwezi sijafanya Ngono na Niko normal kabisa. Na Niko kwenye Ndoa. Lakini awali nikimaliza siku 2 Bila sex nakuwa mgonjwa kabisa Sina Raha na viungo vya mwili vinauma..

Ninachoamini Mimi Akili iliyobweteka na mwili uliobweta Bila shughuli nyingi ni karakana ya Shetani.
 
Kutokua na hamu ya wanawake kwa sababu ya masturbation ni madhara ambayo watu wengi wakipata wanafikiri wamepungukiwa nguvu za kiume.
Punyeto ni aina mojawapo ya sex addiction na ni rahisi kuwa teja wa kujichua kuliko wa kufanya mapenzi ya kawaida.
 
Hii kitu ni common kwa watu wengi asee, hata usiyemtarajia au unayemuheshimu sana unaweza kukuta faraghani mwake ana maswahibu haya,
its like we are fighting demons.

Kwa mimi ishanitokea hii kitu mara tu nilipoanza kufanya hii mambo ya wakubwa nikiwa form 2, baada ya hapo I never stop thinking about TO to the extent ikawa kama inaniendesha. Nikatafuta njia mbadala kutokana na uwoga wa magonjwa ya zinaa nikajiunga chama la wana mchawi soap 😀
bila kujua huko nako nilikuwa napalilia tatizo lingine ambalo baadae nilikuja kugundua lina unafuu wa madhara la sivyo ngono zembe ingenipoteza mapema, wengi wanadai masterbation inapunguza nguvu ila kwangu sijawahi kukutana na hilo tatizo, madhara ninayoweza kuyakiri ni ya kisaikolojia kama vile kutokuwa na hisia na wanawake really tofauti na character wako wa masterbation na kuwa muoga kutongoza au kutokuwa na mazoea na wanawake kiujumla.

Kwa mtazamo wangu tatizo lipo hapa, jamii yetu ya sasa imelifanya tendo hili kuwa kama ni tendo la siri sanasana kwa watoto, na wanapoanza kukua wanakutana na vitisho vingi sana magonjwa, dhambi, mimba na vitu kama hivyo.
Pale atakapogundua vitisho hivyo vinaepukika au atakapokuwa haogopi tena vitisho hivyo ndio tatizo linapoanziaga, ni vyema kuwaelimisha watoto waone ni kitu natural ila kinahitaji ufike rika fulani ndio ufanye.

Ila suluhisho nikuoa asee au kuishi na mwanamke hii inamaliza tatizo kabisa labda uwe unajiendekeza
Ni kweli watu wapo na demons.
Pole mkuu lakini usi trade one addiction for another addiction. Usitibu uraibu wa ngono kwa kitumia uraibu wa kujichua.
 
Ahsante. Lakini suluhisho siyo kuoa ndugu. Wapo watu ninaowafahamu walioamua kuoa au kuolewa kwa Sababu ya kukidhi matamanio ya Ngono.. Ila baada ya kuoa Hali Yao ni mbaya mno kuliko hata mwanzo na inapelekea migogoro mikubwa Sana katika mahusiano..

Mwanadamu ameumbiwa kitu kinachoitwa KUKINAI.. hivyo kama mtu alioa au kuolewa kwa kukidhi hamu ya Ngono. Itafika muda atamkinai huyo aliyeoa au kuolewa naye ataamua kubadili ladha kwa mtu mwingine ili kukidhi matamanio, hapo ndo shida huwa Kubwa zaidi.. Hili tatizo ni Kubwa mno kuliko watu wanavyolichukulia..

Kilichonisaidia Mimi ni Kuwa busy, yaani kufanya kazi kupitiliza na kuuchosha mwili kiasi kwamba ninaporudi nyumbani Sina hamu ya Ngono nahitaji kupumzika, Asubuhi nafanya mazoezi Sana, nikirudi naoga maji ya Baridi na kuanza mizunguko ya maisha, na nikipata Muda wa kupumzika najitenga na Simu yangu na kusoma vitabu hasa vya neno la Mungu Hasa Biblia.. Naweza maliza hata mwezi sijafanya Ngono na Niko normal kabisa. Na Niko kwenye Ndoa. Lakini awali nikimaliza siku 2 Bila sex nakuwa mgonjwa kabisa Sina Raha na viungo vya mwili vinauma..

Ninachoamini Mimi Akili iliyobweteka na mwili uliobweta Bila shughuli nyingi ni karakana ya Shetani.
Ahsante kwa kutoa uzoefu wako. Hiyo kujiweka busy na kukaa mbali na vishawishi ipo very effective.
Naomba niulize, kwanini maji ya baridi yanasaidia? Manake kuna mtu mwingine na yeye kasema akioga maji ya baridi yanamsaidia.
 
Mkuu mimi nilipokuwa mdogo sikuwahi kabisa kujihusisha na haya mambo nilijizuia sana hadi nikamaliza kusoma na kuanza kufanya kazi.
Sasa nilipoanza kuzishika pesa ndio kama nimefungulia bomba na sasa hivi nimekuwa mraibu wa hii kitu.
Yaani kila mwanamke anayekatiza mbele yangu namtamani na nikiwa na pesa huwa napata kiburi fulani na kujiamini kunakuja automatic so huwa naamini mwanamke yeyote nikimtaka nampata hata bila kumtongoza.
Nikajikuta nimedate na wanawake wa kila aina,kila rika hata awe ni wa geti kali vipi,hata awe mke wa nani nikimtaka nampata na nimejikuta nimekuwa mzoefu wa saikolojia za wanawake bila kufundishwa.
Na hii hali imenifanya hata nisione umuhimu wa mke japo natamani kujenga familia.
Hii hali unaiongeleaje mkuu?na nitaiepuka vipi?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Pole sana.
Wewe shida yako ni kwamba unatumia sex kama namna ya kujiona kama wewe ni wa muhimu na una nguvu. Unatumia sex kama namna fulani ya kujimwambafy.
Unatamba na fedha, sex ni muendelezo wa kutamba kwako.
Kukusaidia sasa ndugu ni lazima utoe akilini kwamba wewe una maana pale tu unapofanya mapenzi na kila mwanamke.
Usitegemee ngono kama njia ya kujiamnini. Na imani kwamba mpaka hapo ulipofikia wewe ni mtu ambaye umefanya mengi mazuri yakujivunia na una watu wakaribu wanaokupenda. Hivi vitu vinavyoweza kukupa confidence, usipatie kwenye ngono.
Kwa vile wewe umezaliwa kiumbe hai na ni mwanadamu, una umuhimu. Umuhimu wako hautokani na kufanya kwako ngono.
 
asante mkuu,nimekupata vema.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Yah nililigundua hilo saivi nimejitwalia mwanamwali, hawa wa barabarani na waona kama sanamu hata wavae nguo za nusu uchi hata sishtuki najua ghetto uhakika
Hongera mkuu.
Ila usije ukamuona kama chombo cha starehe. Addiction itakuwa palepale na utakuwa hujafanya chochote kutatua tatizo.
 
Sex addiction is real.

Kuna jamaa nilikuwa nafanya naye kazi mkoa mmoja, alikuwa hawezi kupita weekend bila kufanya ngono, na harudii mwanamke.

Ratiba yake imetawaliwa na ngono tu, jumapili jioni anaenda kutafuta "nyama ya next weekend". Ataenda hata nje kidogo ya mji, kutafuta next "meat"; anarudi na namba zake kama 5 hivi [askari, wauza maduka, manesi; ili mradi ni jinsia ya kike] Kuanzia monday, ni kuchombeza atayeingia line ataliwa Friday mpaka Sunday. Mduara unarudi tena.
 
Yaani hii ni textbook example ya uraibu wa ngono. Sex addiction is very real.
Huyu mtu anatumia muda wake wote kwenye mambo yanayohusu ngono.
Yupo kama mraibu wa madawa anayewaza madawa muda wote.
Cha kusikitisha ni kwamba watu wengi wapo hivi na kwa wanaume inaonekana kama ni kitu cha kawaida, tena ni sifa haswa.
 
Exactly.... jamaa anaonekana kidume kiwembe lakini ukweli ni kwamba ana addiction mbaya sana. Kama ilivyo kwa mateja, jamaa juhudi kubwa kwenye maisha yake zipo kwenye kupata ngono, na mbaya zaidi, with different women.

Inamgharimu sana, bora ingekuwa mwanamke mmoja.
 
We are all sex maniac,we have the beast within ourselves sema ni ishu ya kujicontrol na ukiweza oa mapema utulie uepukane na magonjwa na utumiaji mbaya wa pesa.I'm still learning a lot from Arabs and Indians,the sources of being rich and financial stability
 
Nani alikwambia hao wanaume wa kiarabu wanajicontrol katika mambo ya sex.
Sema tu kinachowalimit ni mazingira yao ni magumu kukutana na mwanamke kirahisi lakini bado wanatamani wapate nyama mpya kila siku.
Ndio maana wakiwa mtandaoni wanasumbua sana dada zetu kuwapigia video call na kuwatongoza.
Lakini mazingira ya kwetu yamerahisishwa kila kona tunapishans na wanawake wamejiachia na nguo za nusu uchi kama ni mwanaume uliyekamilika lazima utaingia kwenye vishawishi.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo issue ipo sana pitia na hii thread

Hiyo issue ipo sana pitia na hii thread

Original post kwenye huo uzi imesema kitu cha ukweli.
Lakini kuna wadau wanatoa michango humo wana glorify haya mambo kitu ambacho ni hatari. Wanaona kama masihara tu.
 
We are all sex maniac,we have the beast within ourselves sema ni ishu ya kujicontrol na ukiweza oa mapema utulie uepukane na magonjwa na utumiaji mbaya wa pesa.I'm still learning a lot from Arabs and Indians,the sources of being rich and financial stability
Ndio lakini bado hutatatua shida ya sex addiction.
 
Dah yaaani mimi huu uraibu wa ngono naona siku zinavyozidi naona unazidi sana nataka nitiane asubui mchana jioni usiku at least nikipiga kilaji nyege zinakatika sema nako naogopa kuwa mlevi mbwa hii dunia ni tafrani tu nikiwa free bora nishinde ni lale tu some time nijinyime nisile ili hizi zisiwe zinanisumbua hivi vitu vingine ni mtihani sana
 
Duu pole sana, nimeona profile pic yako. Unaweza kufahamu nini kilisababisha? Au uraibu wako ulianzaje?
 
Back
Top Bottom