Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Kumpamdisha JPM kwa sasa ni kazi sana, kosa kubwa alilolifanya ni kuchagua kuwa kila mahali. Katika uongozi hilo ni kosa kubwa mno. Kila jema linalofanyika mahali popote nchini wapambe walishauri ionekane ni yeye kafanya, na yeye kwa kupenda sifa akakubali na ikaonekana ni vema. Lakini kinyume chake hakiwezi kuwa sahihi, kanuni inakataa. Walitaka kuaminisha Umma kwamba wanapoona mazuri kwao wajue yameletwa na JPM, watu wakashangilia, wakataka kuaminisha kwamba mkiona mabaya kwenu basi mjue hao ni wapinga maendeleo; Hapo ndo watu wameshituka baada ya matukio matatu yaliyofuatana:-Shukurani kwa maelezo maana wengine na mie ya haya ya chama chao na Membe tunayasoma tu.. kuwaelewa nini haswa kinawasukuma kupiga ramli sana siku hizi na ni wao kwa wao wa ndani ya chama chao.
Kingine ni zile pesa walizoea pia kutumbua hawazioni tena.. matumbo motoooo..
JPM labda nae anatimu humu na kwingine.. inabidi washambulie kuwashushua kwa kuwajibu inavyotakiwa kwa nondo.. maana wanayoandika timu Membe kuvutia watu.. yanaweza pingika kirahisiiiii na kufanya watu wasivutiwe nao.
Na kumpaisha JPM kwa sanaaaaaa
1.Wabunge wa kusini kutetea fedha za korosho kwa maslahi ya wakulima wao na karipio walilopata toka kwa JPM mwenyewe hadi kutishiwa kupigwa shangazi zake Majaliwa.
2.Kuporomoka kwa bei ya korosho na maigizo ya JPM kujifanya kuwa mtatuzi pekee wa tatizo kiasi cha kukataa hadharani wanunuzi waluotafutwa na PM. Kwa hili wananchi wanajua chanzo cha tatizo ni yeye.
3. 25% Pensheni ni kanuni iliyowekwa na serikali ya JPM yenyewe na bunge kupitia Spika Ndugai lilikanusha kuhusika na kwa Mara ya kwanza Ndugai akamsifu waziri kivuli anayetokana na upinzani Esther Bulaya eti kwa kutoa ufafanuzi uliptukuka kuhusu kanuni ya 25% pensheni mkupuo.
***
Ukiangalia matukio hayo matatu tu mbali nabkwamba kuna mengine mengi, lakini haya yamesaidia kuwafumbua macho wananchi wengi hata waliokuwa vipofu kujua kuwa yule anayewaletea mazuri (machache/madogo) ndiye huyohuyo anayewasababishia mabaya (mengi/makubwa).
Kiongozi wa juu hapaswi kujiweka kila mahali Bali anapaswa kuwekwa kila mahali. Wengi humu tumesoma angalau kufikia elimu ya sekondari, mnajua hali ilivyokuwa kwenye shule ambayo Headmaster/mistress anaonekana katika kila tukio. Yaani kila asubuhi yupo paredi, mazingira anakagua yeye, shambani ni yeye, uwanjani timu ya shule anapanga yeye, adhabu - fimbo anachapa yeye; Halafu ETI heshima yake iliendelea kuwa juu hata timu ya shule ilipofungwa, mazao yalipoharibika shambani au shule iliposhuka kitaaluma.
**YEYOTE ANAYETAKA KUAMINISHA WATU MAZURI KALETA YEYE, ASICHUKIE ANAPOAMBIWA MABAYA PIA KASABABISHA YEYE**