Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Kumpamdisha JPM kwa sasa ni kazi sana, kosa kubwa alilolifanya ni kuchagua kuwa kila mahali. Katika uongozi hilo ni kosa kubwa mno. Kila jema linalofanyika mahali popote nchini wapambe walishauri ionekane ni yeye kafanya, na yeye kwa kupenda sifa akakubali na ikaonekana ni vema. Lakini kinyume chake hakiwezi kuwa sahihi, kanuni inakataa. Walitaka kuaminisha Umma kwamba wanapoona mazuri kwao wajue yameletwa na JPM, watu wakashangilia, wakataka kuaminisha kwamba mkiona mabaya kwenu basi mjue hao ni wapinga maendeleo; Hapo ndo watu wameshituka baada ya matukio matatu yaliyofuatana:-
1.Wabunge wa kusini kutetea fedha za korosho kwa maslahi ya wakulima wao na karipio walilopata toka kwa JPM mwenyewe hadi kutishiwa kupigwa shangazi zake Majaliwa.
2.Kuporomoka kwa bei ya korosho na maigizo ya JPM kujifanya kuwa mtatuzi pekee wa tatizo kiasi cha kukataa hadharani wanunuzi waluotafutwa na PM. Kwa hili wananchi wanajua chanzo cha tatizo ni yeye.
3. 25% Pensheni ni kanuni iliyowekwa na serikali ya JPM yenyewe na bunge kupitia Spika Ndugai lilikanusha kuhusika na kwa Mara ya kwanza Ndugai akamsifu waziri kivuli anayetokana na upinzani Esther Bulaya eti kwa kutoa ufafanuzi uliptukuka kuhusu kanuni ya 25% pensheni mkupuo.
***
Ukiangalia matukio hayo matatu tu mbali nabkwamba kuna mengine mengi, lakini haya yamesaidia kuwafumbua macho wananchi wengi hata waliokuwa vipofu kujua kuwa yule anayewaletea mazuri (machache/madogo) ndiye huyohuyo anayewasababishia mabaya (mengi/makubwa).
Kiongozi wa juu hapaswi kujiweka kila mahali Bali anapaswa kuwekwa kila mahali. Wengi humu tumesoma angalau kufikia elimu ya sekondari, mnajua hali ilivyokuwa kwenye shule ambayo Headmaster/mistress anaonekana katika kila tukio. Yaani kila asubuhi yupo paredi, mazingira anakagua yeye, shambani ni yeye, uwanjani timu ya shule anapanga yeye, adhabu - fimbo anachapa yeye; Halafu ETI heshima yake iliendelea kuwa juu hata timu ya shule ilipofungwa, mazao yalipoharibika shambani au shule iliposhuka kitaaluma.
**YEYOTE ANAYETAKA KUAMINISHA WATU MAZURI KALETA YEYE, ASICHUKIE ANAPOAMBIWA MABAYA PIA KASABABISHA YEYE**
 
Same thoughts insighting his personality, actions and vision
 
Wala usipate shida
Humu kila mmoja mjuaji
Nikuwadharau tu
wanaenda na upepo unakopeleka
Hakuna wakumsumbua JPM kwa sasa wacha wajifurahishe
Uzuri nikuwa Ikitokea tofauti na vile Mtazamo wao wa Ukibendera utaona wanavyo potezea kimya kimya
Magufuli ndie Rais mpaka 2025
Labda mungu pekee aamue vinginevyo
 
Nimechukua neno " Ila asibezwe" Kwa hali ilivyo.....ila asibezwe ni nafuu kuliko Falsafa ya Bashitelism....bora aje aifyekelee mbali, maana Membe ni mzuri ktk Jino kwa Jino...Upanga kwa Upanga....Mengine tutavumilia kama tunavyovumilia sasa.....

Adui wa Rafiki yako ni Rafiki yangu...
 
 
tusimlishe maneno.
CCM ni chama imara chenye mfumo madhubuti, mihula miwili ya urais ni sehemu ya utaratibu wa kudumu na unaheshimiwa na kila mwanachama mtiifu wa ccm akiwemo BM kamwe hawezi kuwa muuasi labda awe nje ya ccm lkn sio ndani ya ccm
Unaishi kwa mazoea huo utaratibu wa kuwapokea wabunge wa upinzani na kuwapa vyeo ulikuwepo?
 
JPM ana hulka ya pekee. Kitakachomtokea BCM kitasimuliwa kwa miongo kadhaa ijayo. R.I.P Kassim Hanga!
 
Same thoughts insighting his personality, actions and vision
I think Tz is full of many fresh minds which can make this nation move forward like never before but the only problem is "uvyama fever"..

People say "we can replace JPM with January Makamba, Mwigulu,Membe"..whats so special about them, is it coz of being popular in the last general election or whatelse. Can they be compared to Zitto Kabwe or Tindu lissu for the contribution and influence they have in this country.. Yaani tunaenda kwa upepo ,sikatai mtu kutoka CCM but ni nani haswaa atakaeweza ,this is still questionable nd it got even worse coz the opposition parties are still under the verge of collapse
 
JPM ana hulka ya pekee. Kitakachomtokea BCM kitasimuliwa kwa miongo kadhaa ijayo. R.I.P Kassim Hanga!
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144]
 
Umemaliza mkuu
 
Ikiwa hatadhibiti makelele ndani ya chama anaweza kuema basi kazi ni ngumu. Tembo ana nguvu sana lakini kelele zinamtoa kwenye shamaba la maboga!
 
Unaishi kwa mazoea huo utaratibu wa kuwapokea wabunge wa upinzani na kuwapa vyeo ulikuwepo?
Utaratibu huo ulikuwepo hata kwa awamu zilizopita sema umesahau, mfano mbatia aliteuluwa kuwa mbunge na JK
 

Ipo siku mtaelewa kwa nini wahenga walisema...”Baniani mbaya kiatu chake dawa”
 
Ulikuwa miongoni mwa wajenga hoja humu JF lakini siku za karibuni uwezo wako umeshuka sana labda kwa vile uwezo wa ccm kujenga hoja pia umeshuka hivyo timu nzima kiwango kimeporomoka hakuna wa kumwinua mwenzake. Unaposema hakuna wa kumsumbua JPM kwa sasa wakati tetesi tu za kujitokeza kwa Membe zimemuibua Katibu mkuu wa CCM utabaki unachekesha walionuna. Kwa taarifa yako JPM anasimbuka tena anasumbuka si kidogo, na hapa BM hajatoa tamko rasmi na udikteta wa siasa za majukwaani bado unaendelea subiri zifumuke utajificha chooni.
Hapo mwisho umesema labda Mungu atende yake kuhusu JPM, nadhani ulimaanisha Mungu amchukue mja wake. Kwa taarifa yako na hili liko wazi tangu tupate Uhuru huyu ni Rais wa kwanza wa JMT kuombewa na wananchi wake ni "bora afe tuchague mwingine". Kiongozi mwingine aliyewahi kuombewa hivyo ni Rais wa Zanzibar kipindi hicho mzee KOMANDO Salmini Amour. Kama hali imefika hapo kwa huyo uliza hali ilikuwaje Zanzibar wakati wa Komando hadi ukafikia wananchi kuchukia uhai wa kiongozi wao?
 
Neno
Vijisenti alivyo navyo ndio hivyo amewapa chadrama mcharuko kwa ajili ya mitandao na nikikwambia visenti ni visenti haswa
Kuna watu aliwafanyisha kazi na ameshindwa kuwalipa, kwa kuwa uzee unamjia kwa kasi na watu walio mzunguka wanachukua kile kidogo alicho nacho
Mdhungu sio mjinga akisha ona unashindwa huwa ana kudrop kama hot potato,
Hata kama mpango ulikuwepo lakini huo mpango umekufa kifo cha milele, yaani amejimaliza kisiasa kabisa, self- elimination
Chadrama mcharuko watapiga debe kama kawaida yao, na watazimwa kama kawaida yao!
Hii ni drama ambayo ni predictable kabisa walahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…