Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Bernard Kamillius Membe alizaliwa Novemba 9 mwaka 1953 mkoani Lindi. Ni mwanasiasa ambaye ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kuanzia 2007 hadi 2015. Pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.


Membe alisoma Shule ya Msingi Rondo-Chiponda na alijiunga na Shule ya Sekondari, Seminari na Namupa kwa ajili ya mosomo ya O-Level. Masomo yake ya A-Level alosoma katika Seminari ya Itaga (Itaga Seminary High School).


Baada ya kumaliza hapo alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo alisoma Sayansi ya Siasa (Political Science). Alisoma pia Uhusiano wa Kimataifa (International Relations) kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani mwaka 1990 hadi 1992.


Member alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika utumishi wa mwaka mmoja ambapo alikuwa katika Kambi ya Jeshi ya Oljoro iliyopo jijini Arusha.



Kuanzia mwaka 1978 hadi 1989, Bernard Membe alikuwa mchambuzi wa masuala ya usalama wa taifa katika ofisi ya Rais. Baada ya kumaliza masomo mwaka 1992 nchini Marekani, alipangwa kuwa mshauri katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Ottawa nchini Canada ambapo alifanya kazi hadi mwaka 2000.



Mwaka 2000 aligombea Ubunge katika Jimbo la Mtama mkoni Lindi ambapo alichaguliwa mfululizo hadi mwaka 2010. Akiwa Mbunge, Rais Dkt Kikwete alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya uchaguzi wa mwaka 2005. Kufuatia mabadiliko ya baraza la mawaziri mwaka 2006, Membe alitolewa wizara hiyo ambapo sasa aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini.



Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (sasa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki) baada ya aliyekuwa Waziri, Asha-Rose Migiro kuteuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.



Mbali na kuwa waziri na mbunge alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 2007 ambapo alichaguliwa tena mwaka 2012 katika mkutano mkuu wa 8 wa CCM, Dodoma.



Mwaka 2013 Membe aliwaambia wapigakura wake katika Jimbo la Mtama kuwa asingegombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2015, na hivyo kuzua minong’ono miongoni mwa watu wengi kuwa huenda alijipanga kugombea urais.



Moja ya skendo kubwa ambazo ziliikumba nchi Membe akiwa waziri ni skendo la ununuzi wa rada ya ulinzi ya Tanzania toka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza. Licha ya kuwepo kwa tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada hiyo, Edward Hosea, aliyekuwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mwaka 2012 iliripotiwa kuwa alisema hakuna mtanzania aliyehusika katika skendo hiyo.



Akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika kwa mwaka mmoja wakati Tanzania ilipokuwa mwenyekiti wa umoja huo mwaka 2008. Chini ya uongozi wake, uanachama wa Mauritania na Guinea ulisimamishwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea katika nchi hizo mwaka 2008.


Mwaka 2012 Membe aliitahadharisha Malawi kusitisha mara moja utafutaji wa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa (Malawi huliita Ziwa Malawi) hadi hapo mgogoro wa umiliki wa ziwa hilo utakapotatuliwa. Mgogoro huo ulitokana na mabishano ambapo Tanzania inadai mpaka wa nchi hizo umepita katika ya ziwa, huku Malawi ikishikilia kuwa mpaka upo upande wa Tanzania (ziwa lipo Malawi) kwa mujibu wa mkataba wa Heligoland–Zanzibar wa mwaka 1890.



Karibuni kuibuka kwa tetesi kuwa mwanasiasa huyo ana mpango wa kugombea urais mwaka 2020, na hivyo amekuwa akiendesha kampeni za chini chini ndani ya chama. Kufuatia hatua hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally amemtaka mwanasiasa huyo kufika ofisini kwake, kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
 
Yani watu wengine wapo siku zao wanaona humu ndio sehemu ya kutupia pedi.

Upuuzi mtu.

Membe for presidency!
 
Hatuna cha kupoteza kwasababu hata saizi hagusidiwi na chochote
 
Inawezekanaje?Binafsi Sijaelewa Kwamba Membe Anaweza Vipi kumkwamisha Mhe Rais Kwa Kuanza Mchakato Wa Kampeni Mapema Kabla Ya 2020.

Naamini Mhe Rais Anapendwa Na Kuaminiwa Na Sisi Wana CCM Wote Pamoja Na Wananchi Kule Kwenye Vyama Vya Upinzani Na Wale Wasiokua Na Vyama Kabisa
 
M
Mimi naamini hakuna binadamu asiye mbinafsi, Bashiru anaonekana kwa SABABU YA nafasi yake.jichunguze
 
Ugomvi ukitokea Kati ya watawala na walioonja utawala si ugonvi wa kuuchekelea, maana kitakachotokea kila mtu atajuta. NI wakati wa kuiweka nchi kwenye MAOMBI si wakati wa USHABIKI. Hapa Ndipo inapohitaji hekima na akili. USHABIKI wenu usituangamize.

Well said but viongozi pia wanapaswa kuweka tofauti Zao pembeni. Si kila jambo linahitaji nguvu kulitatua
 
CCM bila dola na bila Tume hii isiyo huru,hiki kiburi chenu kisingekuwepo na ndio maana mnakwepa swala la katiba mpya.
 
Inawezekanaje?Binafsi Sijaelewa Kwamba Membe Anaweza Vipi kumkwamisha Mhe Rais Kwa Kuanza Mchakato Wa Kampeni Mapema Kabla Ya 2020.

Naamini Mhe Rais Anapendwa Na Kuaminiwa Na Sisi Wana CCM Wote Pamoja Na Wananchi Kule Kwenye Vyama Vya Upinzani Na Wale Wasiokua Na Vyama Kabisa
 
Ko unajifanya hujui kama 2015 bao LA mkono ndo liliwabeba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…