Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Hahaha hivi unafikili ni kwanini watu wameamua kumuunga mkono Membe?
Je Jiwe hakuna lolote alilolifanya..?
Je watu wameamua kumchoka mapema hivi kwanini?
Ajitathimini tu aone wapi anakosea....?
 
Membe,Lowasa, Makamba J....hakuna tofauti.

Tatizo la Magufuli ni roho mbaya yake tu.
 
Membe again?
The same Membe?????
Daaaah huyu jamaa mpeni jukwaa tupumzike kheeeeeee!!!!!?
 
Utani utani afu mwishowe inakuwa kama kampeni sasa. Na wanaccm wanavyomponda mwanachama mwenzao Utadhani anatokea upinzani, kumbe yumo chama tawala. Hivi akitoa tamko kuwa ni uzushi na fitina yeye anasapoti utawala uliopo na ataendelea kuusapoti mpaka 2025 itakuwaje? Mtaanza kumsifia? Maana wapinzani wao Wataanza tu kucheka sababu si mtu wao na hawana cha kupoteza maana ni mwana ccm na ni sawa akisapoti.
 
Wanaccm tuna kila sababu ya kumtaka member, kama makamanda nao wanatuunga mkono in vizuri ili turudishe umoja wa kitaifa
 
 
Wanaccm tuna kila sababu ya kumtaka member, kama makamanda nao wanatuunga mkono in vizuri ili turudishe umoja wa kitaifa

Kwendraaaaa kafie, chadrama mcharuko mkubwa wewe
 
Naona watu wanatokwa povu kishen.zi ! Hivi kama JIWE alichaguliwa hata Membe nae anaweza kuchaguliwa pia , haijalishi namna itakavyokuwa Judged ! Nchi hii hamna Rais ambae hajawahi kutu disappoint ! Membe Ana haki zote za kuwa Rais wa nchi hii kama walivyokuwa wengine
 
Membe hafai kabisa kuwa rais, sijui watu wanamtaka ili afanye nini. Magufuri yuko vizuri, akipunguza tu kidogo tabia ya kunyanyasa watu atakuwa super. Magu aache tu tabia ya kuona barabara ni bora kuliko binadamu, haiwezekani mstaafu umpige panga mafao yake halafu barabara ndo uziongezee hela ili zidumu zaidi.
 
Hata mkigongewa wake zenu mtailalamikia Chadema. Pambaneni na hali yenu Bana. Ebo!
 
Huko sahihi kabisa, lowasa alianza mapema sana kampeni zake. Ikatokea misuguano na wenye kuamua nani agombee urais. Kilichompata kila mtu anajua,namuona Membe tayari kaanza misuguano na wenye kuamua nani agombee urais.Anasuguana na Bashiru, Je atatoboa?UKWELI MCHUNGU NI MEMBE HATAKUJA KUWA RAIS WA TANZANIA hata siku moja kama ilivyo kwa LOWASA.
 
Wakuu pole na shughuli za kulijenga taifa.

Wikendi hii nilikuwa Bukoba, sasa ikabidi niende sokoni kununua vitu hasa Samaki nilikuwa nimewamisi kweli.

Sasa katika pitapita yangu sokoni, kila mtu alikuwa anamzungumzia Membe, chakushangaza ata watu kama bodaboda nao eti wanajadili siasa, yaani Rwamishenye, Kashai na Hamugembe kote Membe anazunguzwa tena sio kwa mabaya bali watu wanataka agombee uraisi eti wamechoka na JPM.


CCM tuwe wakweli JPM hapendwi kama zamani, watu wanamchukia balaa, sijui kwa nini.

Ukweli mchungu Membe amepata wafuasi wengi sana, apa Bukoba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…