Kwa heshima na taadhima napenda kuwakilisha mawazo yangu juu ya huu mjadala unaoendelea kati ya wanaotamani membe awe mgombea 2020 na wale wasiotaka kusikia hata kidogo kuhusu wazo hilo.nchi yetu tangu tupate uhuru imetawaliwa na Chama kimoja na Chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kuheshimu mazoea ambayo hayapo katika katiba yao lakini imekuwa kama sheria.Jambo la kwanza ni kuhusu dini ya mgombea hakuna katiba yoyote inayozungumzia kuhusu wagombea kupokezana kutokana na dini lakini kama utafuatilia vizuri utagundua kuwa Rais wa kwanza alikuwa mkristo tena mkatoliki,Rais wa awamu ya pili alikuwa mwislam,Rais wa awamu ya tatu alikuwa mkristo tena mkatoliki,Rais wa awamu ya nne alikuwa mwislam,sasa tuna Rais wa awamu ya tano ni mkristo tena mkatoliki,kwa mtiririko huo inaonyesha wazi kuwa kwa utaratibu huo uliojengeka si raisi kuwa na Rais wa awamu inayofuata mkristo.kwa vyovyote vile anatakiwa awe mwislam hapo 2025. Kutokana na hali hiyo ni vigumu sana kwa membe kuwa Rais baada ya Rais wa sasa kumaliza kipindi chake hapo 2025.
Jambo lingine ambalo halipo kwenye katiba ya Chama tawala lakini imekuwa ni mazoea ni kwamba Rais aliyemadarakani amekuwa akipewa nafasi ya kuwa mgombea wa Chama hicho ili kujihakikishia ushindi bila matatizo maana ni vigumu sana kwa Rais aliye madarakani kuondolewa au kushindwa kwa sababu hiyo ni Afadhali awe mgombea kuliko kuwa na mtu mwingine ambaye Chama hakina uhakika kama atashinda kwa sababu hiyo sioni namna ambayo ccm wanaweza kumwacha Magufuli na kumweka membe.ila wakiamua kukiua Chama Chao na kukiondoa madarakani basi wanaweza kufanya jaribio hilo la hatari sana kwao.wengi wa wanaounga mkono wazo la kuwa na membe 2020 ni wapinzani wa ccm ambao wanajua Fika kuwa ccm wakifanya uamuzi huo watakuwa wamejimaliza na kuondoka madarakani.
CCM sio wajinga kiasi cha kuamua kufanya uamuzi wa kijinga unaowaweka katika hatari ya kuondoka madarakani.Lakini vile vile wale wanaompigia debe Membe wamekosea sana maana wamemmaliza membe na napenda kuwahakikishia bila kuficha membe hatakuwa na wala haitatokea kuwa Rais kupitia ccm kwa sababu tayari amejengewa uadui mkubwa na watawala ambao ndio walikuwa na nafasi ya kumjenga.
Kwa sababu hiyo wale wote wanaopiga kelele kuhusu membe wanammaliza kisiasa kimya kimya lakini kwa hakika.