Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Walikuwa wapigadili wacha waisome namba. Hakuna tena mambo ya dili
 
Haya yaliyofanyika Jana ya kuandaa maandamano ya kubumba ni aibu kubwa na fedheha .

Hii imetudhalilisha kama taifa, huu ni uthibitisho tosha kuwa tumeishiwa viongozi walio wabunifu na weledi katika mambo ya kidiplomasia.

Haingii akilini kabisa kuwa jambo liko mahakamani wewe huku unakwenda kushinikiza ubalozi uchukue hatua za kuingilia muhimili wa mahakama.

Pia huu ni uthibitisho tosha kuonyedha jinsi nchi yetu inavyo usigina utawala wa kisheria, tunayo fanyiwa humu kwetu (kupindisha pindisha sheria wanavyo taka wao kama watawala ) wanadhani kuwa yanaweza kupokelewa na mataifa mengine.

Kama serikali haihusiki katika hili basi ni mategemeo yetu kuona kuwa wale wahuni wote walio ratibu maandamano pamoja na waliohusika kuandamana wote wanasakwa na kuchukuliwa hatua Kali ili iwe fundisho.

Ila kama watakaa kimya tutajua kuwa ni mpango ulio pangwa toka ngazi za juu. Na hapo ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na watu walio bobea kwenye mambo ya kidiplomasia kama Membe ili watuondolee aibu kama hizi. Membe jiandae kuzoa kura nyingi 2020.

MUNGU IBARIKI TANZANIA ILI TUONDOKANE NA AIBU KAMA HIZI.
 
Acheni kujitoa akili watu waliandamana south africa kupinga tu kauli ya Makonda kuhusu ushoga hamkushangaa itakuwa sisi kuandamana kuhusu ndege
 
Jamaa tukomae nae tu ili akili zisogee maana watanzania akili zao zinahitaji watu wa namna hii.hakuna cha membe wala nani tukomae na jamaa hadi kieleweke G Clamp ikikazwa vizuri tutajifunza kuandamana au vipi wajomba.
 
2020 nini?baharia fafanua sisi wengine ni wakulima tupo bush huku
 
Kama ni upinzani ni kwanini? Je kama ni chama tawala ni kwa nini? Hebu wabobebezi wa masuala ya kisiasa njooni tuchambue kwa kina
 
Mambo yataeleweka tu. Mjomba nyoosha nchi tu. Umeshavuka wami bado kidogo tu chuma kilainike. 2020 ongeza 20 tena tiyari tutakuwa tumekuelewa. Hakuna membe wala pembe ya kukutisha
 
Mashabiki na waimba mapambio wengi wa mambo ya sasa hawapo kwenye utumishi wa umma. Kama wapo ni wale ambao wanakula
 
Labda kama mnatafuta sura nzuri lakini he is one of the most hopeless people i ever know.
 
Tunaenda na Magu mpaka 2022 ( Miaka 7 awamu ya kwanza) then anatuchukua awamu ya pili mpaka 2029 akimaliza hana cha kuongeza muda then ndio tunaanza kujadili wengine wa kumrithi
Moshi wa Ruangwa hauwezi kusubiria hadi huko
 
Tunaitaka Tanzania yenye furaha na amani, tunaitaka Tanzania ile yenye viongozi wanaoheshimu sheria na katiba ya nchi yetu, Tanzania iliyosifika kwa uimara wa diplomasia na Ushirikiano wa kimataifa , Tunaitaka Tanzania yenye viongozi wanaohezhimu wananchi wake, viongozi wanaoheshimu utu na faragha ya wananchi, tunaitaka Tanzania ile yenye viongozi wanaoheshimu haki za binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…