Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
 


Kwa hiyo unaamini hizo ngome zake ndio zitamfanya ang'ang'anie madarakani. Hizo ngome zake ndio zimepelekea wengine kufufua ngome zao. Hakuna anayekaa kifala, usidhani ile 1.5t itatosha kumlinda. Subiri uone picha ndio utajua wizi wa kura haulipi.
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
 
Hizi nyuzi za Membe zitaishia kumvuruga tu jiwe huko aliko nimeona na gutter press ( vile vijarida vya Musiba) na vyenyewe vinamzungumzia. Nafikiri kuna watu wa jiwe wameanza kuweweseka.
 
Ila itakuwa kama ndoto kuona Magu akikatwa kwenye kura za maoni.Membe akaze buti.Yote yanawezekana.
 
Maandiko matakatifu yanasema hivi , " AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " kwa namna unavyoandika humu kila siku ni kama unamtegemea Magufuli kuliko hata moyo wako unaokusaidia kuishi , Magufuli , mtu ambaye yeye mwenyewe binafsi wala wazazi wake hawakuwahi kuijenga ccm ni nani katika ccm , hata isiwezekane kung'olewa ? kwa taarifa yako huyu aliyeua chama kwa kutegemea polisi anang'oka kirahisi mno , hana mizizi yoyote , haungwi mkono na wastaafu wala hata kanisa analosali .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…