Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Hii mbinu ya UPINZANI kumchokonoa Yohana na kufarakanyisha Chama Tawala kitoke katika malengo yao ni ya aina yake!

Chama tawala kilianza kuwafarakanyisha CHADEMA humu kwa nyimbo za kumtia Mbowe katika Kiti, na kushindwa jamaa nao wamejibu kwa njia ile ile kuwafarakanyisha CCM na Mwenyekiti.

Wanajua Chair hana uvumilivu, atajibu na wao watakula alama!

Siasa bwana!....piga nikupige
 
Hiyo heshima imepotelea wapi au imetoweka kwenda wapi hadi airudishe huyo membe.

#histimehadpassedaway
 
Huyo jamaa sijawahi mkubali kuwa kiongozi wa nchi hata siku moja....nafikiri amekuwa over_rated mno
Amekuwa overrated kivipi? Kwani nafasi alizotumikia hakuzitendea haki?
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020

Hivi hizi Hela / Pesa ambazo Membe na Kikundi chake cha ' Propaganda ' anazowapeni hadi tokea juzi, jana na leo naona kila mara mnafurika tu hapa Kumuanzishia ' Threads ' kwanini asizikusanye zote na awarudishie Familia ya Hayati Rais wa Libya Muamar Gadhaffi? Mwambieni kabisa kwamba ile ' laana ' ya yule Balozi wa Libya nchini Tanzania aliyefia Ubalozini haitomuacha salama na ni bora aanze ' Kutubu ' kama siyo ' Kuungama ' mapema. Hata afanye vipi na aende wapi Bernard Camilius Membe hawezi na hana uwezo wa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ikitokea akawa basi kwa mara ya Kwanza Tanzania jiandaeni kushuhudia Kundi la Waasi litakaloongozwa na ' Shadow General ' au ' Warlord ' aitwae GENTAMYCINE na nina uhakika ' Utawala ' wake hautokaa / hautodumu / hautochukua muda mrefu na hatimaye sasa Watanzania wote mtakuwa chini ya Uongozi wa muda wa GENTAMYCINE ambapo nitaitisha Uchaguzi mpya na halali na Mshindi ambaye nitaona anafaa Kuwaongozeni Watanzania nitamkabidhi nchi na Mimi kurejea zangu Kutiririka na Kuserereka hapa Jamvini JamiiForums kama kawaida.
 
Naomba niwaambieni kwa wale wambao mnafikiri ndani ya CCM hapawezi kua na mabadiliko yeyote ni kujidanganya kwa ssbabu ya mazoea ya nyuma, kwa vijana mliokua juzi yawezekana hamjui kitu ndio maana mnajipa matumaini kwa msilolijua. Hamuelewi na hamwezi kujua.

Siasa sio ubabe wala vitisho bali ni ufundi wa mtu kulingana na utashi wake. Ndani ya CCM kuna wanachama wenye kadi na katiba ya chama, wameisoma katiba na wanaelewa yaliyomo ndani yake na yanayoendelea hivi sasa. Ili kuepusha mgogoro ndani ya CCM ya sasa ni bora watu waachwe wateme nyongo zao kiliko kutumia mabavu na kukaa na mambo nyoni.

Kwa msiojua ni kwamba haya ya utawala huu wa sasa ni kwa sababu ya siasa za Bernard Membe ndani ya CCM, anajua ni wapi alijisahau na aliteleza na sasa anajiweka sawa asirudie makosa. Katiba ya chama inamruhusu kufanya hivyo, hayo mengine ya mwenyekiti wa sasa kurudi kugombea tena ni taratibu ilizo nje ya katiba na sio lazima.Waliofikiri asingeweza sasa wameina ni bora ngekua yeye kuliko tulikofikia.

Vijana wenzagu mkae mkitafakari kua Bernard Membe haya mawazo ya kutaka kua kiongozi wa taifa hili 2020 sio yake peke yake,atakua ameshauriwa na wazalendo wakongwe ambao tayari hawaridhishwi na upepo wa siasa za sasa. Mtu wa aina hii kutajwa sana sio kitu kidogo, kutakua na msukumo Mkubwa sana tena wa watu wanaojua ni wapi tupo hivi sasa.
Hata Membe mwenyewe akiiona hii thread atashangaa ulikoyatoa haya! Anyway, kwa sisi tuliomo humu JF muda mrefu, hatushangazwi na hizi

Hata Membe mwenyewe akiiona hii thread atashangaa ulikoyatoa haya. Anyway, kwa sisi tuliomo humu JF muda mrefu, hatushangazwi na hizi "White Elephant Inventions" zenu.Mwaka2000 mlisema humu humu kuwa Mkapa atatolewa. Haikuwa!
Mwaka 2010 mlisema Kikwete atatolewa. Haikuwa!
Hivyo, tuna haja gani ya kushangaa mnaposema mwaka 2020 hatatolewa? Tuna haja gani ya kutoamini kuwa Rais Magufuli ataendelea hadi 2025 na zaidi ikibidi?
 
umeona jina membe tu umewashwawashwa. Tulia hii game haiitji hasira.
Wewe ndio unaleta hasira hili game kwangu la kitoto. Unajificha kwenye ujinga IQ hata unajifanya great thinker wakati ni mpuuzi kama mchuzi.
 
Amekuwa overrated kivipi? Kwani nafasi alizotumikia hakuzitendea haki?
...kwa hiyo wewe na akili zako kabisa unaamini Membe anaweza kuwa rais wa nchi hii mzuri ?!!.....hizo nafasi alizobebwabebwa ndio kipimo mnachompimia..?
....hamko serious kabisa
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020

Labda kupitia CUF,ACT-Wazalendo au CDM
 
Back
Top Bottom