Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
 
Mbona Membe ndiye domokaya kabisa. Kuna sehemu yoyote ya hotuba ya Membe ulishamuona Membe ameongea kitu chochote cha kukufanya umtofautishe na wengine wasio na sifa?
Kama alishindwa kuitumia nafasi ya zamani, hana tena ubavu huo.
Mbaya zaidi ni kuwa, Magufuli ameshatengeneza Kamati Kuu yake ambayo ni loyal kwake tofauti na Kikwete aliyezidiwa kete na Lowassa ambaye alifanikiwa kuingiza watu wake wengi kwenye Uchaguzi wa Chama mwaka 2012, kuanzia si kwenye Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu tu bali mpaka kwenye Kamati Kuu.
Mtasubiri sana.


Kwa hiyo unaamini hizo ngome zake ndio zitamfanya ang'ang'anie madarakani. Hizo ngome zake ndio zimepelekea wengine kufufua ngome zao. Hakuna anayekaa kifala, usidhani ile 1.5t itatosha kumlinda. Subiri uone picha ndio utajua wizi wa kura haulipi.
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
 
Hizi nyuzi za Membe zitaishia kumvuruga tu jiwe huko aliko nimeona na gutter press ( vile vijarida vya Musiba) na vyenyewe vinamzungumzia. Nafikiri kuna watu wa jiwe wameanza kuweweseka.
 
Membe asirudi nyuma,muhimu ni kuwa katiba ya CCM inaruhusu mwanachama yeyote kugombea 2020 kwa nafasi yoyote.

Binafsi namuona Membe akishinda kwa kishindo kura za maoni ndani ya chama na kupeperusha bendera ya ccm.

Ni vyema watu wa ccm wakajiandaa kisaikolojia kupokea mgombea mpya atakaeirudisha Tanzania kwenye medani za kimataifa
Ila itakuwa kama ndoto kuona Magu akikatwa kwenye kura za maoni.Membe akaze buti.Yote yanawezekana.
 
Una ajili sana. Nimefurahia komenti yako: "... na sanasana hizi thread zinampa Membe tabu sana huko aliko..."
Wameache apumzike mtu wa watu, kwa alivyoanguka akiwa na sapoti ya Rais, ataweza kurudi eti kwa sababu kuna baadhi ya wana-CCM hawampendi Magufuli?
Unawafahamu kweli Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, achilia mbali ile composition ya Kamati Kuu?
Fuatilia Kamati Kuu uone kama kuna sura ya kumuona Membe kama mbadala ifikapo 2025.
Maandiko matakatifu yanasema hivi , " AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " kwa namna unavyoandika humu kila siku ni kama unamtegemea Magufuli kuliko hata moyo wako unaokusaidia kuishi , Magufuli , mtu ambaye yeye mwenyewe binafsi wala wazazi wake hawakuwahi kuijenga ccm ni nani katika ccm , hata isiwezekane kung'olewa ? kwa taarifa yako huyu aliyeua chama kwa kutegemea polisi anang'oka kirahisi mno , hana mizizi yoyote , haungwi mkono na wastaafu wala hata kanisa analosali .
 
Back
Top Bottom