Membe hatofanya miujiza maana CCM ni walewale..
ila yafuatayo;
1-Utekaji wa raia utapungua
2-Viongozi kuwatukana wananchi kutapungua
3-Ukanda, udini na ukabila utapungua
4-Watumishi kunyimwa haki zao kutapungua
5-Kesi za kipumbavu za kubambikiziana zitapungua
6-Sheria zitakazopitishwa hazitobeba hisia za mtu mmoja pekee kwa maslahi binafsi
7-Viongozi wenye phd kuacha facts na kutoa mipasho ya taarabu kutapungua
8-Viongozi wa kitaifa hawatowakimbia wananchi kwenye misiba
9-Kuhonga kodi ili uungwe mkono kutapungua
10-Ajira zitaongezeka
11-Askari wa Rwanda nchini watapungua
12-Mtanzania atakuwa na thamani zaidi kuliko mbwa wa polisi
13-Biashara zitakuwa maana unyonyaji utapungua
14-teuzi zitapungua
15-data za kupika zitapungua
16-kukurupuka kutapungua
17-hazina itaangaliwa na wale wote wenye mamlaka kisheria na sio mtu na mpwa wake pekee
18-watu watakuwa huru kufanya siasa, kutoa maoni
19-nchi itakuwa na jembe la uwakilishi nje ya nchi, haitakuwa tena tanzania ya kukimbiakimbia vikao vya wakuu wa nchi
20-njaa itapungua na furaha itaongezeka..
21-mawazo ya wasomi yatapewa nafasi yake