Ili kukata mzizi wa fitina usio na jina, nimejitolea kusafiri kutoka hapa Mtwara hadi mkoani Lindi kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Jasusi Mstaafu Benard Camilius Membe kumuuliza bila kumliza. Nimepewa taarifa zenye kila aina ya sifa kuwa kwasasa hupatikana sana kwake Lindi. Pia, nitapitia Mtama kujionea 'maendeleo yasiyo na upendeleo' jimboni humo.
Nikifika kwake nitamuuliza: 'Wana baraka zako?'. Maana wanakutaja kwa haja na tija kila mara kwenye vyombo vya habari. Ghafla bin vuu umeletwa juu. Unasema kuwa ni mbadala wa aliyeko madarakani, tena ni 2020. Wapigachapuo wako wanachagiza habari zako na picha mbalimbali zinazoakisi jinsi walivyokumisi siasani. Nakuja tutete Benard.
Katika siasa, kwa uzoefu wangu wa chamani, Serikalini na kwenye vyombo vyetu, hakuna jambo la kulipuuza. Kila anayetajwa au kila kinachotajwa hupaswa kuchambuliwa na si kupuuziwa. Hupaswa kujadiliwa badala ya kudhihakiwa. Hupaswa kuchujwa badala ya kufujwa. Hupaswa kuzingatiwa badala ya kukataliwa. Benard, nakuja kusikia neon lako.
I hope, our meeting will be a memorable one. Stay tuned!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mtwara kwenye korosho)