Naomba niwaambieni kwa wale wambao mnafikiri ndani ya CCM hapawezi kua na mabadiliko yeyote ni kujidanganya kwa ssbabu ya mazoea ya nyuma, kwa vijana mliokua juzi yawezekana hamjui kitu ndio maana mnajipa matumaini kwa msilolijua. Hamuelewi na hamwezi kujua.
Siasa sio ubabe wala vitisho bali ni ufundi wa mtu kulingana na utashi wake. Ndani ya CCM kuna wanachama wenye kadi na katiba ya chama, wameisoma katiba na wanaelewa yaliyomo ndani yake na yanayoendelea hivi sasa. Ili kuepusha mgogoro ndani ya CCM ya sasa ni bora watu waachwe wateme nyongo zao kiliko kutumia mabavu na kukaa na mambo nyoni.
Kwa msiojua ni kwamba haya ya utawala huu wa sasa ni kwa sababu ya siasa za Bernard Membe ndani ya CCM, anajua ni wapi alijisahau na aliteleza na sasa anajiweka sawa asirudie makosa. Katiba ya chama inamruhusu kufanya hivyo, hayo mengine ya mwenyekiti wa sasa kurudi kugombea tena ni taratibu ilizo nje ya katiba na sio lazima.Waliofikiri asingeweza sasa wameina ni bora ngekua yeye kuliko tulikofikia.
Vijana wenzagu mkae mkitafakari kua Bernard Membe haya mawazo ya kutaka kua kiongozi wa taifa hili 2020 sio yake peke yake,atakua ameshauriwa na wazalendo wakongwe ambao tayari hawaridhishwi na upepo wa siasa za sasa. Mtu wa aina hii kutajwa sana sio kitu kidogo, kutakua na msukumo Mkubwa sana tena wa watu wanaojua ni wapi tupo hivi sasa.