Nyinyi ndo mtakaofanya Jf ifungiwe sio kwa mihemko hiyo, lakini kingine sisi watanzania tunaongoza kwa unafiki, kwani hata miaka ya nyuma watanzania hawa hawa walipiga kelele sana kwamba nchi imeuzwa kila mtu anachukua chake bora utawala unaokuja lichukue jeshi au itokee vita ndo akili zetu zitakaa sawa.
Sasa basi amekuja rais ambae anafanania uongozi wake na jeshi cha ajabu watanzania hao hao tunapiga kelele tena ooh rais gani hatufai rais dicteta kama si unafiki ni nini? Je kama kweli nchi ingechukuliwa na jeshi kama watu walivokua wanaombea mnafikiri tungekua katika hali gani au kungetokea vita kama watu walivokua wanaombea tungekua katika hali gani hapo ndipo utakapojua kua watanzania ni wanafiki kupitiliza hatujui tukitakacho, kila siku porojo za unafiki tu.