Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

tusimlishe maneno.
CCM ni chama imara chenye mfumo madhubuti, mihula miwili ya urais ni sehemu ya utaratibu wa kudumu na unaheshimiwa na kila mwanachama mtiifu wa ccm akiwemo BM kamwe hawezi kuwa muuasi labda awe nje ya ccm lkn sio ndani ya ccm
 
Bora CCM ile pamoja na rushwa na ufisadi mwingi, tulikuwa tunaigawana keki,mkubwa anapata kikubwa mdogo anapata kidogo,CCM hii ni mkubwa tu anapata keki,mdogo hapati kitu na hata akiokota masalia, mkubwa anarudi kumnyang'anya!!
Kodi ya visima,Pension 25%!!
WanaCCM kindakindaki Oyeeeeeeeeeee!!!
 
Hata kama hatoshi ila kwa hali ya sasa anafaa.
.
Screenshot_20181202-090007.jpeg
 
Povu hilo, na we umeshabaa hata unachokiandika hauna uhakika nacho maana unaaandika unafuta! unaandika unafuta. KAZINABATA...
Shukurani kwa maelezo maana wengine na mie ya haya ya chama chao na Membe tunayasoma tu.. kuwaelewa nini haswa kinawasukuma kupiga ramli sana siku hizi na ni wao kwa wao wa ndani ya chama chao.

Kingine ni zile pesa walizoea pia kutumbua hawazioni tena.. matumbo motoooo..

JPM labda nae anatimu humu na kwingine.. inabidi washambulie kuwashushua kwa kuwajibu inavyotakiwa kwa nondo.. maana wanayoandika timu Membe kuvutia watu.. yanaweza pingika kirahisiiiii na kufanya watu wasivutiwe nao.

Na kumpaisha JPM kwa sanaaaaaa
 
watanzania vichwa mbuzi inamaana nje ya ccm hakuna viongozi?
 
Ni mtazamo binafsi lakini wenye kuakisi ukweli... CCM inaandaliwa kuingia kwenye wakati mgumu tena, ni mtifuano wa ndani kwa ndani
. Urais 2020
. CCM asili dhidi ya CCM makinikia(mabaki)
. CCM kindakindaki dhidi ya CCM maslahi (wakuja)
Bernard Camilius Membe diplomat na jasusi wa muda mrefu, mshindwa wa kinyang'anyiro cha urais ngazi ya chama bado hajakubali kushindwa, bado ana ndoto ileile ya kukalia kiti kikubwa na amekamia hasa
Haiba ya Membe ni reincarnation ya haiba ya Kikwete (carefree) ni tofauti kabisa na haiba ya mzee baba KUKAZA hasa.... Membe ni expert mzuri sana kwenye mahusiano ya kimataifa, na pengine kwenye ushushushu lakini si kwenye siasa tena kukalia kiti kikubwa
Kipindi kile wakati wa kutafuta nafasi ya kuteuliwa, hakuonesha tofauti na wanaccm wengine, hakuongea cha ziada, wote walifanana... Hakutupa dira na maono ya tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.. Wote katika ujumla wao ndani ya CCM walifanya mahubiri ya kisiasa
Akiwa shina moja na JK, ana sehemu kubwa ya lawama nchi ilipokuwa imefikia kipindi kile, kumpa usukani na kuendelea kuchanja mbuga kuelekea maporini

Sasa basi kwanini nasemwa asibezwe?! Huyu ni tarumbeta ya kupaza sauti ya wanaccm wengi wanaougulia kimyakimya na kushindwa kuongea kwa uwazi, kwa sauti
Huyu ni sauti ya manung'uniko ya wanaccm wengi ambao hawaridhishwi kabisa na mwenendo wa chama kwenye kila kitu lakini kubwa kuliko yote ni kule kuwapa wahamiaji (haramu) madaraka na nafasi za upendeleo... Wanapatwa na hisia kuwa kuna CCM mpya inaundwa taratibu ndani ya CCM halisi (CCM ya mwenyekiti dhidi ya CCM ya wote)
Ni kupitia hayo kwa uchache ndani ya mengi chamani, Membe ananijenga kwa kasi ya ajabu, na harakati zake hizo zilianza mara baada ya uchaguzi mkuu.... Membe ana kundi kubwa nyuma yake.. Ni vigumu kumdhibiti kama walivyodhibitiwa kina Makamba Jr, Lameck, Nape nk.. Huyu ni kada mzoefu chamani na wa muda mrefu... Ametumwa...!!

2019 hiyoo bado siku chache tu, Membe yuko nje ya nchi anakotuhumiwa kupanga mambo yasiyowapendeza watu fulani.. Huku wengine wakiona ni sawa... Hapa ni swala la mizania.. Nani ana wafuasi wengi zaidi wa hiari...
Membe anarudi kukanusha/kujibu tuhuma,.. Anajipanga kisawasawa, ameshaanza kusafishiwa njia na timu zake mitandaoni .... Ni yeye tu ndio anasikika na kujadiliwa... Na kwa sehemu kubwa akisemwa vizuri na akitabiriwa vema... Hivi vitu havifanyiki kwa bahati mbaya... Ni mipango inayosukwa kwa ustadi sana..

Hivyo basi pamoja na kwamba hatoshi kukalia kiti kikubwa, lakini ni tishio kubwa... Akiamua (kwa nguvu ya wapambe wake) ataiteka December yote.... Atavuruga hasa... Atawavuruga.... Na CCM itaingia 2019 ikiwa mapande makubwa matatu
. CCM mwenyekiti
. CCM Membe
. CCM wengine
Ujumbe huo wa Nape unabeba siri kubwa nyuma ya kinachoendelea sasa chamani... Muda utasema.. View attachment 952923
Tuache unafiki nchi imekwama
 
Nionavyo mimi tuna safari ya kuelea Uganda, Rwanda na Burundi kwenda kuwasalimia
 
mimi si mfuasi wa siasa za Tz maana ndizo zimetufikisha hapa lakini lazma nitoe mtazamo wangu kwa hili.

Membe anaweza kuwa na haiba ya Kikwete ambaye kwa kipindi hicho naye alipwaya (japo anasafishwa kutokana na madhaifu ya aliyepo), lakini Membe hana uwezo ambao kikwete alikuwa nao.Wakati akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hakuwa fanya kitu cha mshangao na alipokuwa akihojiwa sikuona substance na charisma ya kiuongozi simply alibebwa na mfumo ila alikuwa na uwezo hafifu..

Akheri kwa sasa tunabanwa lakini kuna projects zinafanyika ambazo unaona dhahiri kizazi kijacho kitanufaika ila kumpa nchi Membe ni risk iliyopo dhahiri..

Kwangu mimi Rais ambaye anatakiwa kumrithi Magufuli ni lazma awe mafia yaani aweze kuwa economical diplomat(sio mambo ya kutabasamu hovyo na kusema hawa ni marafiki zetu toka uhuru), Strategist, atakayekubali katiba mpya , visionary, mwenye upendo na uchungu na nchi hii na kadhalika..

Vigezo vyote hivyo Membe hana hata kimoja zaidi ya uswahiba na kufananishwa na Kikwete
 
Back
Top Bottom