Mimi sihitaji kua ni lazima awe Membe au Lowasa, ninayotakata ni kiongozi atakayeheshimu makundi makubwa matatu yaliyoshikilia mustakabali wa usalama wa taifa letu, yaani Wakulima na Wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara.
Ni ukweli ulio dhahiri kua makundi haya yapo katika hali ngumu kupita kiasi, yamechoka sana. Huenda sio kwa kupenda lakini inawezekana ni kwa kukosa mbinu murua za kuwasaidia.
Binafsi ninachotaka tu ni utawala wa awamu hii umalizie miaka take 3 iliyobaki uondoke tu, hauna maslahi kwa taifa. Kila wanayofanya hakuna faida iliyoonekana kwa mtanzania, tunaambiwa eti ni kwa ajili ya vizazi vijajavyo, who knows kama sio uongo mnataka kutusotesha bure.
Haaa kama ni membe,Lowasa,Zitto, Lissu au mtanzania yeyote mwenye uwezo wa kuliongoza taifa. Huu utawala uliopo waliyofanya yanatosha, miaka 5 iwatoshe wasepe tuu.Sisi raia ndio wenye maamuzi kumweka mtu madarakani na ni lazima tuseme.